Nyeusi kuitwa nyekundu

Nyeusi kuitwa nyekundu

Siasa za Tanzania zimekuwa kama mchezo wa mpira, league ikiisha usajili unaanza na hapo kila timu inafanya usajili. Sijui hili kwa wenzetu wa Ulaya na Marekani, nao huhama kutoka Republican kwenda Democratic au Labour ya Uingereza kwenda Conservative? Ninachojua ni kuwa UKAWA au coalition za namna hiyo zipo hata Ulaya, chama kikubwa kinajazilizia kutoka vyama vidogo. Kuna hili la ufisadi na usafi wa Lowasa, kwa kuwa wakati ule hatukuonyeshwa kila kitu huu ni wakati muafaka, tujue kama alikuwa fisadi au la tufanye maamuzi. Wakati mwingine upinzani hutoa tuhuma kwa ushahidi wa kimazingira unaoweza kuwa kweli au vinginevyo. Ila haya maneno "mheshimiwa Rais wangu, ulikuwa unajua kila kitu ...."
 
Wanasiasa wote wana njaa...wanawachota akili mnakua misukule yao...wote wezi hakuna cha tawala wala pinzani

watanzania wengi bado hawajawasoma vizuri wanasiasa,
 
Tanzania sanaa
duh
ingekuwa tunaweza mambo mengine km hz sanaa mbona tungekuwa mbali
mungu ibariki afrika mungu ibariki tanzania
 
Nguvu ya mabadiliko nilikuwa naiheshimu sana, ila kwa sasa niko nimeduwaaa tu sielewi cha kufanya.

Kweli tembelea Tz uyaone!!

Mwal nyerere huko uliko, fanya hata muujiza mmoja, maana hili jahazi linazama na hatuoni wa kutuokoa.
 
umenichekesha sana. Sasa ndiyo watu wataelewa kazi ya mabere marando ilikuwa nini hapo. bado mzee mzima apson! weye chezea serikali ya professor JK

Kazi ya Mabere Marando ilikuwa nini kwani?
Sijakuelewa bado
 
Na tatizo tunameza kila kinachosemwa na Wale tunaoita viongozi wetu bila ya kutafakali hata kidogo.

Tuna Safari ndefu sana.
Loh!!!!.....Hii safari sijui tuipe jina gani?
 
Nguvu ya mabadiliko nilikuwa naiheshimu sana, ila kwa sasa niko nimeduwaaa tu sielewi cha kufanya.

Kweli tembelea Tz uyaone!!

Mwal nyerere huko uliko, fanya hata muujiza mmoja, maana hili jahazi linazama na hatuoni wa kutuokoa.

kwa akili zako unafikiri nyerere alikua mkamilifu. mbona ujamaa ulidunda, uchumi ulipolomoka kipindi cha uyo unayemuona mungu wako
 
Najribu kufikiri kwa sauti.

Maajabu mengi hutokea Africa hususani Tanzania. Mlima mrefu kuliko yote baani Afrika uko Tanzania.

Fuvu la Binadamu wa kwanza liligundulikaTanzania. Na hata kikombe cha babu kilitokea TZ.

Kwa jinsi CCM ilivyo chafu hata aje malaika kutoka mbinguni naye atabadilika na kuonekana mchafu na kwa jinsi CHADEMA ilivyo safi hata akija Lucifer akagombea kupitia CHADEMA atabadilika na kuonekana msafi sana.

Fumbo mfumbie mjinga,mwerevu atakuumbua!

Mtaongea mengi ila ndio sikio la kufa,lowasa sasa yupo ndani ya Nyumba cdm
 
CCM ni chafu halikadhalika CDM,

wanasiasa badilikeni, tunawaona mnavofanya madudu yenu ,mnavojitahidi kupaka rangi penye uchafu,


Nyie cdm & ccm hamna lolote wote wachafu

Act nawaonea huruma maana hata udiwani hampati
 
kwa akili zako unafikiri nyerere alikua mkamilifu. mbona ujamaa ulidunda, uchumi ulipolomoka kipindi cha uyo unayemuona mungu wako

Labda hujamwelewa. Yeye hajasema Nyerere ni Mungu wake
 
Back
Top Bottom