Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,405
- Thread starter
- #721
Unashindwa kuelewa kwa sababu umeamua kufanya hivyo ili ubadilishe hoja ya msingi; ambayo wewe na wenzako Pro-Nyerere mnaikimbia- nayo ni Efficiency.
Ujamaa haukuwa na effeciency ndiyo maana West walikataa kununua mazao. Lakini mnashindwa kuelewa vitu vya msingi vilivyosababisha hayo mazao kutaka kununuliwa kwa bei rahisi.
As Wajamaa mtaendelea kulaumu, na kusema wengine hawajui, lakini hiyo tactic ya Wajamaa haikuanza leo. hata Mzee Nyerere alikuwa nayo.
By the way unashindwa kuelewa kwa sababu unajump kwenye hoja nyengine bila ya kuanzia kwenye post za mwanzo.
West walikataa kunua mazao kwa sababu ujamaa haukuwa na efficiency? oh my goodness! Miaka ipi hiyo walikataa kununua mazao? do you think west had a choice kukataa kununua mazao? unaishi dunia yenye historia ipi? vita vya kwanza na vya pili vya dunia vilitokana na wao kugombania sources za such raw materials, then unadiriki kugeuza historia? West hawakukataa kununua mazao and they will never dare, watachofanya ni kuhakikisha wanayanunua kwa bei rahisi kupitia devaluation ya kulazimisha nchi maskini and other measures;
Vitu vilivyosababisha mazao yanunuliwe kwa bei rahisi ni Ujamaa kutokuwa na efficiency??? kilimo cha mkoloni na cha ujamaa mbona havikuwa na tofauti in terms of efficiency? at least for once, elewa hoja ya Mkandara juu ya hilo na kuweka suala la ushabiki pembeni, ile ndiyo knowledge ambayo utapewa na mtu yeyote mwelewa ambae hata sasa hivi ukienda mwamsha usingizini hata bila ya kumwambia juu ya mjadala huu JF, atakueleza;
Sijarukia hoja, nimekuwa naifuatilia sana tu, lakini nimeona hapa tuwekane sawa; your entire argument on that is fallacy;