Rwebangira
Member
- Aug 25, 2011
- 21
- 5
Mkandara,
Umeongea hoja za msingi sana. Kuhusu suala la u-dictator, Nyerere ni kweli alikuwa na hiyo element, but he wasn't a dictator per se, kwani hali ya udikteta means "expecting unquestioning obedience", this wasn't always the case; Nyerere hakuwa hivyo wakati wote, waliokuwa wanamwogopa ni wale waliokuwa na unafiki katika Ujamaa, otherwise kulikuwa na watu wanam challenge kwelikweli, and he liked it; Tumesikia mengi sana jinsi gani alivyokuwa anawatembelea wanafunzi wa UDSM mara kwa mara kwenda to debate with them kuhusu mambo mbali mbali ya ndani na nje ya nchi – kina Issa Shivji, Sitta na wengineo walikuwa wanapambana nae kweli kweli; Ugomvi mkubwa wa Mwalimu na UDSM wakati ule, Mh. Sitta akiwa ni mmoja wa vinara wa ugomvi ule, was sera ya kutumikia JKT kwa ulazima; Wengi wakiongozwa na Sitta hawakulitaka hilo; walikuwa na hoja, lakini ukiangalia mantiki ya JKT kwa miaka ile, haikuwa mbaya, kwani nchi nyingi mpaka leo kama Israel, Greece, etc, lazima mtu uende jeshini ikiwa sehemu ya kuwa raia madhubuti zaidi;
Daima mtu yeyote anayeshambuliwa na KIRUSI (VIRUS) cha ubinafsi hawezi kuielewa hoja yako ambayo kimsingi ni ya kweli na wazi na katika hali ya kawaida haikutakiwa utumie muda na nafasi kubwa kuyaeleza haya ila kwa kuwa tayari kirusi hiki kimeshika hatamu imekugharimu pole sana. Usichoke ni jukumu la kila mtz kupambana na KIRUSI CHA UBINAFSI kama vile ambavyo Yeye BABA WA TAIFA MWL NYERERE ambavyo hakuchoka.
Naona htuataki kuelewa au hujaelewa. Swali langu naliweka katika simple way. Kenya na Uganda ambao ni majirani zetu na tunamhusiano makubwa ya kijamii ambazo zilikuwa na free market kuanzia wakati huo zimefanikiwa kiasi gani ili tuweze kusema umasikini wa Tanzania kama zao la ujamaa ni mbaya zaidi ya ule wa Kenya.
Pili, lini nyerere alikataza watu wasilime kwa matrekta. Unakumbuka Azimio la Iringa na Moshi yanasemaje.
Jiulize miaka 25 baada ya Nyerere na 10 baada ya kifo kitu gani kinatuzuia tusiitumie ardhi hiyo ili hali ujamaa umekufa kabisa.
Kuhusu R& D ni nchi ipi inaweza kusema imewkeza sana na imefanikiwa miongoni mwa majirani zetu.
Labda nikudokolee kidogo, Tanzania leo hii ina jeuri ndani ya EAC kwasababu moja, nayo ni heshima ya kusimama kama taifa. Ungekuwepo mwaka 1977 wakati Kenya wanaua EAC na kuzuia kila kitu ungeelewa tunasema nini. Nchi ilikuwa haina kitu chochote.
Mwalimu akaitoa hapo na sasa tunasimama na kuwaambia wakenya hatuwategemei na tunaweza peke yetu.
Changamoto za vita halafu EAC na uchumi wa dunia kwa ujumla ungemkuta mpuuzi taifa hili lisingekuwepo.
Huu ni ukweli hata akina Kikwete wanaukubali ukiwauliza. Bahati nzuri yalitokea wakati wa Baba wa Taifa.
.......inaonekana Nyerere alikufa tangu 1985! what happened?
Mkuu Nyerere kwa alivyoiweka Tanzania anatakiwa awe miongoni mwa founding fathers
where is karume? au Nyerere ni baba wa taifa lipi, Tanzania au Tanganyika ambayo haipo?
Yaani jumla ya Tanganyika na zanzibar inaunda Tanzania yet baba wa taifa atoke tanganyika tu? ndio maana nikaweka founding father..
kwa sababu hiyo ..Huku kwetu visiwani hakuna anayemtambua Nyerere kama baba wa TAIFA. Nimekazania sana logic zaidi kuliko maneno, ila kwao karume sr ndiobaba wa taifa.
Kwa mtazamo wangu, baba wa taifa ina sound vyema kama katika taifa hilo race/kabila ni moja, siyo kwa taifa letu kama hili ambalo tuna makabila na dini nyingi. kwa stability ya taifa tulitakiwa tuwe na founding fathers. Nadhani unasikia kwenye mihadhara na wengine wanasema humu haiwezekani mkatoliki kuwa baba wa taifa!! hii itaendelea tu whether you agree with them or not.
cheers
Vijiji vya Ujamaa na Ubabe wa Nyerere
These and similar studies suggest that the failure of the Ujamaa scheme was predicated on a number of salient a priori and
empirical factors. Three of these factors are pertinent to this discourse. First is the argument that the initiative to start Ujamaa villages did not come from rural peasants. The scheme failed to gain the necessary ideological
acceptance among the vast majority of the peasantry. Right from the beginning, the dominant attitudes of the people ranged from skepticism and mistrust to outright resentment and opposition (Lofchie, 1978: 452). Secondly, the use of coercion to ensure mass villagization - from threats of forced transportation to short prison sentences under the pretext of tax arrears -
militated against the effective operation of Ujamaa villages. Finally, the efforts at building Ujamaa villages were greatly constrained by bureaucrats who held out government aid as incentives to peasants to move into villages.
Mkuu wangu wala hakuna sababu ya kumshusha Nyerere bali ni ukweli ambao hauhusiani kabisa na mapungufu. Mimi nitasema wazi sioni kabisa ubaya wa DIKTETA ikiwa unataka kufuata UJAMAA maana hapa Ujamaa unachukuliwa kama usafiri kulingana na sehemu unayosafiria. Huwezi tumia meli ktk usafiri wa mto, na haya mazingira tulokuwepo ndio wengi wanashindwa kutazama. Hivyo matumizi ya mashua (UJAMAA) was the right idea kabisa kutumia mashua (mtumbwi) na nahodha naye hupiga kasia akiwa nyuma ya watu wote kuongoza mashua tofauti na Ubepari ambao upo ktk bahari kuu matumizi ya Meli ni muhimu na nahodha hashiki usukani wala kupiga kasia..Sisi tulipata Uhuru tukiwa kati na nchi za mwisho na maskini duniani nadhani chini ya Haiti na E. Guinea kama sikosei, hatuwezi kuchukua Ubepari ktk hali ile hata kidogo...At least ninakuelewa sasa vizuri........ulichoandika hapa pro-Nyerere wengi huwa hawataki kusema wala kusikia. Kusema Nyerere alikuwa na element za u-dictator umeongea jabo la msingi sana.
Lengo si kumshusha au kudhihaki...kwenye ukweli tuseme ukweli, pazuri tuseme , pabaya tuseme....we learn from mistakes
Tukiweza kuwasema vibaya viongozi wote bila upendeleo utaona taifa taratibu linabadilika na kuwa na viongozi makini walio tayari kukosolewa....tukiweka wigo wa kutokosoana basi tutakuwa na viongozi malaika. Sina shida kumsifia na kumkosoa Nyerere na sitabadilika kwa hili...ila pro-Nyerere wengi humu wanachojua ni matusi tu!! simply kwa sababu walicheza chipukizi za CCM na gwaride na kushikana mikono na walimu..wengine simply kwa sababu eti waliimba wimbo siku ya uhuru! wanachojua matusi tu...wengi wameishazeeka na kupata magonjwa mabaya...Nashukuru wewe si mmoja wao!
Falsafa za mwalimu na mtizamo wake hata kama ulikuwa na makosa..hatuwezi kuishi kwenye makosa hayo. Nyerere alitambua alishindwa nchi na alikiri wazi na tena akatuusia kuwa tuchukue mazuri yake na tuache mabaya......KITU AMBACHO TAIFA LA TANZANIA LITAJUTA MAISHA YAKE YOTE NA HAPA PIA NITAMTUPIA LAWANA NYERERE NI KUTOMWEKA MRITHI WA CALIBER YAKE! caliber kwa maana visionary, msomi, na ambaye anaweza kuchukua nchi ilivyo akaibadilisha smoothly huku akilinda misingi ya utaifa. Mwinyi hakuwa mrithi sahihi wa Nyerere......hakuwa na legacy, hakuwa na maoni na hakuichukua nchi ilipokuwa na hali yake na kubdalisha mitazamo ya watanzania!
Mwinyi hakufit.....na Nyerere alikaa miaka mingi madarakani aliwaza nini juu ya Mwinyi..?? au aliweka boya ili yeye azidi kuonekana mzuri hata hii leo?? lets be honest viatu vya Nyerere vilikuwa vikubwa sana kumtosha Mwinyi........VIONGOZI WALIOYATARISHWA NA NYERERE WAKO WAPI? AKINA NANI? WAMEFANYA NINI? maana sifa ya kiongozi ni kutengeneza warithi......
Kama kwa wakati huo Nyerere alishindwa kuwa-inspire watu wake wa karibu wawe kama wewe na wakubali kuwa yeye ni mentor wao..then there was something very terrible kwenye tabia ya Nyerere! sitaki kusema kwa sasa
Mwinyi alikuwa kama anaanza taifa jipya kabisa na watu wapya kabisa.......inaonekana Nyerere alikufa tangu 1985! what happened?
Kwanza kabisa mimi sikubaliani na hilo "baba" wa Taifa, huo ni ukatoliki na hutumika kanisani kuwaita wachungaji "baba", kumuita "papa" "baba" mtakatifu.
Hii nchi Nyerere aliikuta ina watu wa imani tofauti na ameondoka ametuwacha watu wa imani tofauti, kwanini mtubambikie vyeo vya kikatoliki na Kikristo? hamuoni kuwa huo ni "udini" wa wazi wazi?
Hakuna "baba" wa Taifa, huo ubaba alipewa na nani na kwa ridhaa ya nani? msitujaze ujinga.
Alaa upo usingizini au? wewe kweli ni great sinker, huna chochote unachowaza zaidi ya udini?
Suala la udini, ukabila, muungano, na ubaba wa taifa nililielezea sana kwenye my original post; naomba pia nikuuize, hivi je, yule mwanaharakati John Okello mnamzungumziaje katika mazingira ya ubaba wa taifa zanzibar?
JAMANI KWA WALE TUNAOFUATILIA HISTORIA YA TANZANIA TUNAFAHAMU ZANZIBAR ILIPATA UHURU MWAKA 1963 CHINI YA WAZIRI MKUU MOHAMED SHAMTE SASA IWEJE LEO HII TUMSAHAU SHAMTE KIRAHISI TU WAKATI YEYE NDIYE BABA WA TAIFA?
On December 16, 1963, Prime Minister Mohammed Shamte, as the head of the independent and sovereign goverment of Zanzibar, delivered what was to be a historic speech to the United Nations General Assembly in New York.
Kwanza kabisa mimi sikubaliani na hilo "baba" wa Taifa, huo ni ukatoliki na hutumika kanisani kuwaita wachungaji "baba", kumuita "papa" "baba" mtakatifu.
Hii nchi Nyerere aliikuta ina watu wa imani tofauti na ameondoka ametuwacha watu wa imani tofauti, kwanini mtubambikie vyeo vya kikatoliki na Kikristo? hamuoni kuwa huo ni "udini" wa wazi wazi?
Hakuna "baba" wa Taifa, huo ubaba alipewa na nani na kwa ridhaa ya nani? msitujaze ujinga.
Waberoya,
..kwanini baba wa taifa awe ni Shamte na siyo Sultan Jamshid Bin Abdullah?
..Zanzibar was a Constitutional Monarch kama anavyoeleza bwana Shamte.
..hata walipopindua walisema wamempindua Sultani siyo huyo kibaraka Shamte.
Tuwe na utamaduni wa kumsifia mtu pale anapofanya mema na kumkosoa pale alipoteleza.
Mimi nitamsifia Nyerere kwa kujijenga kisiasa na kuiletea Tanganyika hishma kubwa kisiasa. Lakini tukitazama kwa upande wa Uchumi hapa alifeli kwa asilimia zote. Tatizo kubwa ni kuwa alikuwa haambiliki. Kwa wale wachache wetu ambao tulibahatika kufanya nae kazi watalijua hilo . Kwani kwake siasa ilikuwa mwanzo na taaluma baadae.
Nitawarudisheni Nyuma kidogo. Enzi za Nyerere aliweza ku identify maadui zake nao aliwasema hadharani kuwa walikuwa ni Ujinga, Umasikini na Maradhwi.
Na vile vile aliweka bayana kuwa ili Tanganyika iendelee ilihitaji vitu vinne. yaani Watu, Ardhwi, Siasa safi na Uongozi Bora. Suala la kujiuliza je aliweza kufanikiwa katika vita hivyo hususan katika kuinua uchumi wenu?
Sasa Mlipofikia Tz ni matunda ya misingi mibovu iliyowekwa na muasisi wa uhuru wa Taifa lenu Mwl Nyerere. Mpaka leo watu siasa nyingi sana lakini utendaji mdogo sana.
Poleni sana,
Mr. Right
Naomba tujudaliane kidogo labda tutaeleweshana; nimekusoma naona kuna kijichanganya kidogo; nimeona umesema wewe ni pro free market economy; mpaka hivi sasa tunapoongea free market economy ipo kwenye vitabu tu ni theory na utekelezaji wake ni mgumu naweza kukupa mfano mwaka huu Lockheed Martins walishinda tenda ya kutengeneza ndege za kujaza mafuta kwa matumizi ya jeshi la Marekani; ilionyesha dhahiri wao tenka zao ni bora na za gharama nafuu ukilinganisha Boeing; mara baada wizara ya ulinzi kuipa Lockheed tenda hiyo Bunge lilingilia kati na kuinyanga`nya Lockheed tenda kwa sababu za kuilinda Boeing kibiashara; ipo mifano mingi serikali ya Marekani imetoa tenda kwa makampuni kadhaa bila kuwepo kwa ushindani wa kibiashara, swali la msingi inakuwaje hapo kwenye free market pia kuna kulindana? Naamini umeshawahi kusikia vitu kama tarrifs, import quarters; hakuna hata nchi moja ya magharibi ambayo haina vitu hivyo je kwa nini wasiruhusu bidhaa zisitoke nchi moja hadi nyingine bila mikingamo? Ukweli hiyo free market wanaoyoihubiri sisi tuifuate wakati wao wenyewe wanaitekeleza kinadharia ; pia hakuna hata nchi moja ya kiafrika yenye uwezo wa kushindana na nchi za magharibi kwenye bidhaa za viwandani, wao walipolenga Afrika tuwe na free market lengo hasa ni kwa makampuni yao kuuza bidhaa zao Afrika.
Kwa nini Mwalimu Nyerere alikazania kilimo? Jibu ni rahisi wakati tunapata uhuru sekta viwanda ilikuwa duni kumbuka waingereza hawakuwa watawala walikuwa ni caretaker; waliwekeza zaidi kwenye makoloni yao kenye; Uganda na kwingineko ni kama vile unapopata jukumu la kumlea mototo wa jirani; mfano Kenya baada ya uhuru ilikuwa na miundo mbinu bora kuliko Tanganyika yote hayo si kuwa Mzee Jomo Kenyatta alifanya kazi ya ziada kuliko Mwl. Nyerere bali alirithi miundo mbinu bora.Kilimo ilikuwa ndio njia pekee ambayo ingeweza kutuokoa kiuchumi; na kutufanya tusiwe na tatizo la ajira; mpaka hivi sasa kilimo kinaajiri zaidi ya 60% za wakazi wa sub sahara Afrika; suala la vijiji vya ujamaa hilo labda nikueleweshe na nina uhakika Mkandara ama Mchambuzi waliligusia wengi walilipinga vijiji vya ujamaa lakini ukweli leo Tanzania imetengamaa kwenye kilimo kwa vijiji vya ujamaa ambavyo Mwalimu Nyerere alivianzisha kama vingekuwa vibaya basi wengi wangerejea kwenye utaratibu wao maisha kabla ya vijiji vya ujamaa.
Umekuwa ukisema eti Mwalimu Nyerere alifeli huo ni mtazamo wako nikiangalia nchi za sub Sahara Afrika Tanzania ya Mwalimu Nyerere ilikuwa bora zaidi ya nchi nyingi sijui kama umewahi kutembelea nchi za kiafrika na hapo ndipo utapoona matunda ya ile sera ya Mwalimu maendeleo mikoani; alijaribu kuhakikisha kila mkoa unakuwa na sera ya maendeleo. Lengo kuu la Mwalimu ilikuwa kuhakikisha tunakuwa ya wakulima na wafanyakazi. Mwalimua alipigwa vita sana na nchi za magharibi kwani alikuwa anahatarisha maslahi yao na hiyo ndiyo iliyopelekea kuhitilifiana na vyombo kama IMF na WB.
Kila mfumo una matatizo yake hata kwenye nchi zilizoendelea kuna matatizo ya mfumo wa kibepari si kila mtu anauafiki; je ni kwanini Taifa kubwa kama Marekani linapigania kuwepo kwa middle class? Kwa nini hawapiganii kila mtu awe milionea? Ama labda nikuulize nchi za kipebari kama Spain na Italy uchumi wao umeanguka kwa kiasi kikubwa ni kipengele gani kilichopo kwenye msahafu wa ubepari ambao hakikufuatwa?
Hili somo ni linahitaji fikra pevu ukirupuka Nyerere Nyerere hutatalielewa; ichukulie JF kama ni uwanja wa kuelemishana na si lazima tukubuliane katika kila jambo ila njoo na hoja.
Chama
Gongo la Mboto DSM
Okelo mwanaharakati kivipi??
Sio Ujamaa matatizo ni watu. UK nasikia sera ya kijamaaa ya afya. Obama naye kachukua.Ineefficiency yetu iko weye ubong si sera ya ujamaa wala ubepari.
Ni watu wachache au wengi kwenye system ya ujamaa ndio waliukwamisha . kusema hivyo sio kwamba tungekuwa na ubepari tungekuwa na nafuu No. tungekuwa na nafuu ndogo tu tena kwa wachache. Chukulia mfano wa US Vs Norway . kwa sera y ubepari Tanzania ingekuwa na matabaka kuik hata yale ya Kenya
Naona htuataki kuelewa au hujaelewa. Swali langu naliweka katika simple way. Kenya na Uganda ambao ni majirani zetu na tunamhusiano makubwa ya kijamii ambazo zilikuwa na free market kuanzia wakati huo zimefanikiwa kiasi gani ili tuweze kusema umasikini wa Tanzania kama zao la ujamaa ni mbaya zaidi ya ule wa Kenya.
Pili, lini nyerere alikataza watu wasilime kwa matrekta. Unakumbuka Azimio la Iringa na Moshi yanasemaje.
Jiulize miaka 25 baada ya Nyerere na 10 baada ya kifo kitu gani kinatuzuia tusiitumie ardhi hiyo ili hali ujamaa umekufa kabisa.
Kuhusu R& D ni nchi ipi inaweza kusema imewkeza sana na imefanikiwa miongoni mwa majirani zetu.
Labda nikudokolee kidogo, Tanzania leo hii ina jeuri ndani ya EAC kwasababu moja, nayo ni heshima ya kusimama kama taifa. Ungekuwepo mwaka 1977 wakati Kenya wanaua EAC na kuzuia kila kitu ungeelewa tunasema nini. Nchi ilikuwa haina kitu chochote.
Mwalimu akaitoa hapo na sasa tunasimama na kuwaambia wakenya hatuwategemei na tunaweza peke yetu.
Changamoto za vita halafu EAC na uchumi wa dunia kwa ujumla ungemkuta mpuuzi taifa hili lisingekuwepo.
Huu ni ukweli hata akina Kikwete wanaukubali ukiwauliza. Bahati nzuri yalitokea wakati wa Baba wa Taifa.