Nyerere hakung'atuka

bnhai

JF-Expert Member
Jul 12, 2009
2,824
2,381
Mwalimu Nyerere alipotangaza kukaa pembeni mwaka 1985 wengi walihuzunika. Yeye alidai anang'atuka. Kiuhalisia hali ya nchi kiuchumi na wakati vilimsukuma kando.

Siasa zake za ujamaa na kujitegemea za kunyang'anya watu mashamba na kuwarundika sehemu moja zilidhoofisha uchumi.

Utaifishaji wa mali za Watanzania wenye asili ya kiasia ambao hauna tofauti na kilichofanywa Uganda kuliondoa mtaji.

Nchi ilikwenda vitani kwa ahadi ya kurejea katika hali ya muda mfupi baada ya vita haikutokea.

Tukumbuke mwalimu Nyerere tayari alikuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 20 na nchi ilidorora zaidi. Kwahiyo wakati ulimsukuma Nyerere.
 
Last edited by a moderator:
inaonekana wewe ni mjukuu wa hao "watanzania wenye asili ya asia" pole sana.
 
Sijaelewa point yako hapa nini sasa? Kwanza kwa taarifa yako NENO kung'atuka hakulitamka wakati anaachia URAIS, neno hilo alilitamka wakati anaachia uwenyekiti wa ccm mwaka 1987! Usichanganye madesa.
 
inaonekana wewe ni mjukuu wa hao "watanzania wenye asili ya asia" pole sana.
Ukitoa hoja uko naye. Watu wanailaumu CCM ya miaka karibu 25 ilikuwa chini ya Nyerere. Viwanda vilikuwa vinakufa tayari kwa kukosa malighafi na vipuri. Maisha yalizidi kuwa duni na uhuru wa vyombo vya habari haukuwepo.
 
Sijaelewa point yako hapa nini sasa? Kwanza kwa taarifa yako NENO kung'atuka hakulitamka wakati anaachia URAIS, neno hilo alilitamka wakati anaachia uwenyekiti wa ccm mwaka 1987! Usichanganye madesa.
Sawa mkumbushaji, kwahiyo aliachaje Urais. Point hapa ni kuachana na dhana kuwa aliondoka kwa hiari bali ni kushindwa kuongoza nchi kulimng'oa. Foleni za kaunguza, sukari na sabuni za kuruka, foleni za misaada ya vyakula etc
 
Mnamuongelea mtu ambae mnajua hawezi jibu hoja zenu, Komaeni na mzee wa msoga, mana hachelewi kujibu mapigo
 
Sawa mkumbushaji, kwahiyo aliachaje Urais. Point hapa ni kuachana na dhana kuwa aliondoka kwa hiari bali ni kushindwa kuongoza nchi kulimng'oa. Foleni za kaunguza, sukari na sabuni za kuruka, foleni za misaada ya vyakula etc
Nyerere aliiacha nchi ikiwa na uzalendo wa hali ya juu, nakumbuka Enzi hizo tunasoma shule ya msingi walimu walikua wanajitolea kutufundisha hata Jumamosi bila kudai malipo yoyote ya ziada, madaktari hali kadhalika, mgonjwa anapokufa mbele yao unawaona wanavyosikitika. Madereva wa makampuni kama KAMATA, KAUMA, KAURU, RAILWAY (wengi walitamka Relwe) walikua wanajiona wanalo deni kufikisha mizigo na abiria sehemu husika on time ingawa barabara zilikua mbovu sana. Kwenye vita ya Idd Amini ambayo tulilazimishwa kupigana, wananchi pamoja na wanajeshi walionesha kwamba kweli wanaipenda Tanzania yao, wapo watu waliotoa Ng'ombe, vyakula na hata watoto wao (hawakua wanajeshi) kwenda kupigana na IDD Amini. Nyerere pia aliiacha watoto wakiwa wanasoma BURE from shule za vidudu (sasa chekechea) hadi nafasi ya u profesa bure na matibabu nayo bure. Hospitali za kulipia zilikuwepo (za makanisa na zilijulikana kama hospitali za mesheni). Kwa upande wa uchumi hali iliaanza kua mbaya hasa mara baada ya vita vya IDD Amini lakini kabla ya hapo mambo yalikua safi sana. Kitu kimoja kilicho haribu sana uchumi (Vita ikiwa ni sababu) ni ile sera ya kulinda viwanda vya ndani na hence kuzuia bidhaa kutoka nje zisiingie kwa wingi, uzalishaji wa viwanda vyetu kama vya Sukari, Sabuni, Mafuta ya kula na hata TIPER ulikua mdogo kuliko mahitaji ya Watanzania na huo ndio ukawa mwanzo wa foleni kwenye maduka ya Ushirika, Duka la Kaya na RTC. Mwinyi yeye akafungua mipaka na hivyo bidhaa kua bwerere madukani but ukawa pia ndio mwanzo wa viwanda vingi kufa. Remember, dunia ya wakati huo ilikua ina policy 2 tu za uchumi, is either uwe Bepari au Mjamaa; mwanzoni mwa miaka ya 90 Ujamaa ukafa duniani na hicho ndicho kilichotokea. Hayo tu kwa UFUPI.
 
Hapa naona pumba tu hakuna hata mantiki kumuongelea Nyerere ambaye hayupo lakini akili yako na ya bibi yako mkizichanganya kwa pamoja hamuwezi kumfikia Nyerere yeye hayupo lakini maneno yake yanaishi
 
Naona wewe umezaliwa 1987 miaka 2 baada ya Mwalimu kung'tatuka. Hivyyo hujui kitu na bora unyamaze

Mwalimu Nyerere alipotangaza kukaa pembeni mwaka 1985 wengi walihuzunika. Yeye alidai anang'atuka. Kiuhalisia hali ya nchi kiuchumi na wakati vilimsukuma kando.

Siasa zake za ujamaa na kujitegemea za kunyang'anya watu mashamba na kuwarundika sehemu moja zilidhoofisha uchumi.

Utaifishaji wa mali za Watanzania wenye asili ya kiasia ambao hauna tofauti na kilichofanywa Uganda kuliondoa mtaji.

Nchi ilikwenda vitani kwa ahadi ya kurejea katika hali ya muda mfupi baada ya vita haikutokea.

Tukumbuke mwalimu Nyerere tayari alikuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 20 na nchi ilidorora zaidi. Kwahiyo wakati ulimsukuma Nyerere.
 
Sawa mkumbushaji, kwahiyo aliachaje Urais. Point hapa ni kuachana na dhana kuwa aliondoka kwa hiari bali ni kushindwa kuongoza nchi kulimng'oa. Foleni za kaunguza, sukari na sabuni za kuruka, foleni za misaada ya vyakula etc

Wwe una maruweruwe yako hadi unakera. umeota umaskini na failures ukaanza kutafuta watu wakumalizia hasira yako. Si ajabu hujaandika tu lakini umeshamlaani mama yako kwa kukuzaa.

No matter how the economy was na hata bila ya kuangalia sababu na mazingira yaliyokuwepo, naomba ujibu maswali yafutayo ambayo hayahitaji kumaliza la saba ili mtu ajibu.

1. Mwalimu alipoondoka kwenye uongozi, aliondoka kwa kuwa alishindwa kwenye uchaguzi??

2. Kuachia ngazi kwa mwalimu kulitokana na utashi wa katiba yoyote?

3. Alipinduliwa?

4. Kama siyo aliondokaje? Na kama ni suala la kutathmini na kuona yeye mwenyewe kwamba sasa ni muda wa kuachia uongozi mwingine, una mu accuse kwa kosa lipi hapo? Kama ni kawaida, mbona kikwete na mwinyi hawakujipima na kuona wanafanya uharibifu kwa taifa wakaachia kwa hiyari zao? Kikwete ambaye pamoja na kuipeleka nchi kwenye mauti bado analilia kubakia ikulu japo kwa mlango wa nyuma?

Unachogombana na uzalendo wa mwalimu wa kuamua kuacha mwenywe kwa ridhaa yake bila kusukumwa na sheria yoyote kama kina kikwete ni nini?

una vita gani na mwalimu/

Bila shaka hilo ni tatizo lako na frustrations zako za failures ambazo kwa nia safi naomba ziabaki kwako na wala usitake kulazimisha na wengine wakufuate. Failures zako hazina uhusiano na mwalimu. unaelewa wwe?
 
Last edited:
Mwalimu Nyerere alipotangaza kukaa pembeni mwaka 1985 wengi walihuzunika. Yeye alidai anang'atuka. Kiuhalisia hali ya nchi kiuchumi na wakati vilimsukuma kando.

Siasa zake za ujamaa na kujitegemea za kunyang'anya watu mashamba na kuwarundika sehemu moja zilidhoofisha uchumi.

Utaifishaji wa mali za Watanzania wenye asili ya kiasia ambao hauna tofauti na kilichofanywa Uganda kuliondoa mtaji.

Nchi ilikwenda vitani kwa ahadi ya kurejea katika hali ya muda mfupi baada ya vita haikutokea.

Tukumbuke mwalimu Nyerere tayari alikuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 20 na nchi ilidorora zaidi. Kwahiyo wakati ulimsukuma Nyerere.
Una haki ya kutoa mawazo yako, Lakini baadhi yetu, na tunakuthibitishia kuwa tupo wengi, Mchango wa Nyerere kwa nchi hii haupimiki. He is the father of the nation. Nyere alileta umoja wa kitaifa, mtu unaweza ukaenda Tabora ukitokea Songea ukaishi bila matatizo. Alijenga taifa ambapo sasa tunajiita watanzania, aliweka misingi mizuri ya uchumi kwa kuleta viwanda vinavyoongozwa na watanzania wenyewe. Watoto wa maskini walisoma bure mpaka chuo kikuu. Mimi nilisoma wakati wa Nyerere na mzee wangu hakuwa na uwezo mkubwa. Nilisoma sekondari bure, nilisoma chuo kikuu bure... Kule Mlimani Enzi hizo tukienda cafeteria kulikuwa na mabomba ya maziwa..mtu unakunywa 'tani' yako. Nikiwa sekondari tulikuwa tunakwenda na sanduku tu na nguo zako. tulikuwa tunapata vitabu vyote bure pamoja na madaftari bure. Kulikuwa hakuna wizi wa vitabu kwani kila mtu ana vitabu husika. shuleni tulikuwa na swimming pool. tunaogelea na kujidai. Shuleni tulikuwa na vviwanja vitatu vya mpira wa miguu, kiwanja kikubwa cha riadha, viwanja vya netball, viwanja vya volleyball, hockey na kadhalika. Tulikuwa na indoor games nyingi tu. Wakati wa likizo tukiwa sekondari tulikuwa tunasafiri kwa kutumia travel warrants na tunapewa chakula cha njiani. Ajira ilikuwa nje nje, makampuni na mashirika mengi. Uzalendo ulikuwa mbele.

Maisha yalikuwa mazuri ila mambo yakaanza kuharibika baada ya vita vya Uganda vya Oktoba 1978...kwa hiyo debate ya Nyerere inaweza kuleta kuleta mjadala mzito kwa baadhi yenu na hasa wale wasioijua historia ya nchi hii. Hivi baadhi yenu mnafahamu kuwa before independence nchi hii ilikuwa na machifu wakitawala maeneo mbalimbali na katika makabila mbalimbali nchini mwetu? Hali hii ilifutwa after independence na nchi ikawa moja.

Kama watanzania tungekuwa makini na yale aliyoyapanga Nyerere nchi hii ingekuwa mbali mno. Vijiji vya ujamaa alivyoanzisha Nyerere vilikuwa na uzuri wake ingawa ni kweli utekelezaji wake ulikuwa na walakini. Ni katika vijiji vya ujamaa ambapo huduma muhimu kwa wananchi zilizogezwa kama elimu (shule), afya(dispensary), maji na kadhalika. Wakati wa Nyerere watu wengi wakiwemo wazee walijua kusoma na kuandika, hali ilifikia almost 90 per cent. lakini ni kweli kulikuwa na mabaya wakati wa ujamaa. Enterpreneurship ilitoweka, uvivu uliongezeka tukiamini kuwa kila kitu kitaletwa na serikali...hali ndio inayoendelea mpaka sasa ambapo watanzania tukiwa humu ndani ni wavivu tukitaka serikali ifanye kila kitu... Nidhamu nayo imetoweka.. mtu umejenga kwenye hifadhi ukibomolewa unataka serikali ikutafutie kiwanja...wabunge nao wakiwa bungeni kila mara wanalia ...'tunataka serikali ifanye hiki...'.

Mjadala wa Nyerere ni pana lakini kwangu mimi mazuri ya Nyerere ni 90% na mabaya ni 10%.
 
Sijaelewa point yako hapa nini sasa? Kwanza kwa taarifa yako NENO kung'atuka hakulitamka wakati anaachia URAIS, neno hilo alilitamka wakati anaachia uwenyekiti wa ccm mwaka 1987! Usichanganye madesa.
Uko sahihi, tatizo kuna watu wananzisha mada juu ya jambo la kusimuliwa. Sasa hasara gani kwa operation vijiji, lengo ilikua huduma za jamii kuzifikisha kirahisi, Shule, maji, barabara, Afya na huduma nyingi ambazo ni mahitaji ya jamii ambazo ni ngumu kumfuata mtu mmoja mmoja.
 
Ubinadam Wa baba wa Taifa hauna tofauti na ubinadama wa binadam yeyote wa leo ila mchango wake kwa Taifa hili ni mkubwa sana, ana mazuri yake meeeengi sana aliyoyafanikisha na hakika tunapaswa kujivunia sana kwa kua na baba kama huyu, pia kuna mambo aliyoshindwa kuyatekeleza kwa ubinadam wake na hatupaswi kumlaumu ama kutungia hoja maana hata tukipewa leo hayo majukum hatutaweza kuyakamilisha Asilani. Alienda kwa amani na Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi amina.
 
Mwalimu Nyerere kaondoka duniani miaka karibu 17 iliyopita lakini kila ninapozitazama zile clips za speech zake kichwani mwangu naona kama vile ameongea jana tu!. Genius. Ikulu ni mahali patakatifu, anayekimbilia ikulu tena kwa kutumia pesa ni wa kuogopwa kama ukoma, bora uwe uchi kimwli kuliko kuwa uchi kiakili. Watutsi na wahutu ni watu wa kabila moja kwani wanaongea lugha moja lakini wanauana!. Leo hii Rais ni mwenyeji wa Chato, Makamu wa kwanza anatoka visiwani, Waziri mkuu mwenyeji wa Lindi, mawaziri wote wanatoka kila kona ya Tanzania, yote haya yanatokana na falsafa za upendo na utu ambazo huwezi kuziongelea bila ya kumkumbuka Mwalimu Nyerere. Mungu amlaze pema peponi.
 
Hoja kwamba aling'atuka kwa sababu za kiuchumi haina mashiko. Mbona tunao kina Mugabe na Nkuruziza ambao wanatawala nchi zilizo hoi kiuchumi lakini wao wameng'ang'ania madarakani. Nyerere alikuwa muungwana sana.aliona bora amuachie mwenye fikra mbadala... yeye abaki kama mshauri. Hiki nacho ni kipaji alichojaaliwa..kujua nchi ichukue muelekeo gani wakati wa msukosuko wa kiuchumi. na sio kusababisha nchi iingie katika vita ya wenyewe kwa wenyewe kisa unataka ubaki kuwa Rais wa maisha.
 
Ubinadam Wa baba wa Taifa hauna tofauti na ubinadama wa binadam yeyote wa leo ila mchango wake kwa Taifa hili ni mkubwa sana, ana mazuri yake meeeengi sana aliyoyafanikisha na hakika tunapaswa kujivunia sana kwa kua na baba kama huyu, pia kuna mambo aliyoshindwa kuyatekeleza kwa ubinadam wake na hatupaswi kumlaumu ama kutungia hoja maana hata tukipewa leo hayo majukum hatutaweza kuyakamilisha Asilani. Alienda kwa amani na Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi amina.
Can you imagine..unapewa uongoze nchi iliyokuwa koloni la mwingereza..huna uzoefu wowote wa kiutawala zaidi ya kuwa mwalimu na mpigania uhuru tu...huna hata wasomi wa kutosha. waliowengi elimu zao ni kama za akina Bibi Titi..kajaribu hata kuunda Jamhuri ya Muungano bila hata ya kumwaga damu ..Niambie ni nani anaeweza kuyafanya haya katika kizazi hiki cha dotcom.
 
Back
Top Bottom