Nyerere hakung'atuka

Nyerere hakung'atuka

Mwalimu Nyerere kaondoka duniani miaka karibu 17 iliyopita lakini kila ninapozitazama zile clips za speech zake kichwani mwangu naona kama vile ameongea jana tu!. Genius. Ikulu ni mahali patakatifu, anayekimbilia ikulu tena kwa kutumia pesa ni wa kuogopwa kama ukoma, bora uwe uchi kimwli kuliko kuwa uchi kiakili. Watutsi na wahutu ni watu wa kabila moja kwani wanaongea lugha moja lakini wanauana!. Leo hii Rais ni mwenyeji wa Chato, Makamu wa kwanza anatoka visiwani, Waziri mkuu mwenyeji wa Lindi, mawaziri wote wanatoka kila kona ya Tanzania, yote haya yanatokana na falsafa za upendo na utu ambazo huwezi kuziongelea bila ya kumkumbuka Mwalimu Nyerere. Mungu amlaze pema peponi.
Tuliamini saana katika propaganda hizi kupitia RTD. Eti umoja na kaunganisha watu. Hawa watu kuanzia chama cha TAA walikuwa wanaunganishwa na nani? Kukaa na kujilinganisha na wahutu na watutsi, si kujitendea haki. Nchi hii ina makabila zaidi ya 100. Sio makabila mawili. Babu zetu tayari walikuwa wameoa kwenye makabila tofauti kabla hata ya Nyerere kupata uhuru. Yeye aliwaunganisha nini? Kwnini mifano ni Rwanda, Burundi na Kenye, wale wasiochapana wameunganishwa na nani?
 
Wwe una maruweruwe yako hadi unakera. umeota umaskini na failures ukaanza kutafuta watu wakumalizia hasira yako. Si ajabu hujaandika tu lakini umeshamlaani mama yako kwa kukuzaa.

No matter how the economy was na hata bila ya kuangalia sababu na mazingira yaliyokuwepo, naomba ujibu maswali yafutayo ambayo hayahitaji kumaliza la saba ili mtu ajibu.

1. Mwalimu alipoondoka kwenye uongozi, aliondoka kwa kuwa alishindwa kwenye uchaguzi??

2. Kuachia ngazi kwa mwalimu kulitokana na utashi wa katiba yoyote?

3. Alipinduliwa?

4. Kama siyo aliondokaje? Na kama ni suala la kutathmini na kuona yeye mwenyewe kwamba sasa ni muda wa kuachia uongozi mwingine, una mu accuse kwa kosa lipi hapo? Kama ni kawaida, mbona kikwete na mwinyi hawakujipima na kuona wanafanya uharibifu kwa taifa wakaachia kwa hiyari zao? Kikwete ambaye pamoja na kuipeleka nchi kwenye mauti bado analilia kubakia ikulu japo kwa mlango wa nyuma?

Unachogombana na uzalendo wa mwalimu wa kuamua kuacha mwenywe kwa ridhaa yake bila kusukumwa na sheria yoyote kama kina kikwete ni nini?

una vita gani na mwalimu/

Bila shaka hilo ni tatizo lako na frustrations zako za failures ambazo kwa nia safi naomba ziabaki kwako na wala usitake kulazimisha na wengine wakufuate. Failures zako hazina uhusiano na mwalimu. unaelewa wwe?
Ukiwa kiongozi wa nchi ni lazima ujadiliwe. Na ndio maana tunamzungumzia "baba wa Taifa". Kwenye mada nasema wazi. Nyerere hakutoa fursa kwa mawazo ya wengine. Aliamini katika ya kwake na alipoona hayatekelezeki akakimbia. Ukizungumzia katiba, yeye ndiye alikuwa muhusika mkuu wa muundaji wa hiyo katiba. Hakukuwa na demokrasia. Aliondoka kwa sababu his demise was inevitable. Alibisha saana mapinduzi ya sera za kiuchumi za mwanzoni mwa miaka 1980. Akang'ang'ania kutekeleza za kwake nchi ikawa haikopesheki na haiwezi kuzalisha na njaa ilikuwa kawaida. Nyerere akaondoka. Mbaya zaidi ukisoma Development Studies (DS) kwa mlimani, utakuwa na yenyewe imechachuliwa eti masharti ya World Bank na IMF.
 
Ndo maana nasema hivi, wanaomlaumu MWALIMU wajilaumu wao kwanza, alifanya yake kwa uwezo aliojaaliwa na Manani na amepumzika kwa amani na Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, Amina.
Alifanya ya kwake kumbe alitakiwa kufanya ya Taifa. Waulize kina Mtei na Kambona na wengineo. Ukitoa maoni kuhusu sera zake, unageuka adui.
 
Huo ni msemo na si kama unavyouchukulia wewe. Hakuna mkamilifu chini ya Jua na anayefanya mengi kwa ajili ya wengi basi hukumbukwa na wengi, bado Nyerere anaishi japo alishatangulia mbele ya haki. Mtei namjua na Kambona pia, niulize hata na Sarakikya kabisa, ila kumbuka ndani ya hii dunia hata ufanye mazuri mangapi huwezi kosa wapinzani, ni kwa hekma tu na busara na sometimes kaubabe kiduchu kinahitajika kuwa-nulify maadui zako, hasa wa ndani.
 
Mkakati wa kumfanya MTAKATIFU unaendelea.Na huwezi kuwa MTAKATIFU kama hujafanya kazi ya Kanisa.sasa hapa sijui iyakuwaje.
 
Kwahiyo ugumu wa kumjadili Nyerere unatokana na mkakati wa kumfanya Mtakatifu?
 
Naaam...hakuna haja ya kumjadili.Haitasaidia kitu chochote na ni kuntia doa ktk mkakati wa kumfanya Mtakatifu kwa kazi aliyoifanyia nchi.
 
Wwe una maruweruwe yako hadi unakera. umeota umaskini na failures ukaanza kutafuta watu wakumalizia hasira yako. Si ajabu hujaandika tu lakini umeshamlaani mama yako kwa kukuzaa.

No matter how the economy was na hata bila ya kuangalia sababu na mazingira yaliyokuwepo, naomba ujibu maswali yafutayo ambayo hayahitaji kumaliza la saba ili mtu ajibu.

1. Mwalimu alipoondoka kwenye uongozi, aliondoka kwa kuwa alishindwa kwenye uchaguzi??

2. Kuachia ngazi kwa mwalimu kulitokana na utashi wa katiba yoyote?

3. Alipinduliwa?

4. Kama siyo aliondokaje? Na kama ni suala la kutathmini na kuona yeye mwenyewe kwamba sasa ni muda wa kuachia uongozi mwingine, una mu accuse kwa kosa lipi hapo? Kama ni kawaida, mbona kikwete na mwinyi hawakujipima na kuona wanafanya uharibifu kwa taifa wakaachia kwa hiyari zao? Kikwete ambaye pamoja na kuipeleka nchi kwenye mauti bado analilia kubakia ikulu japo kwa mlango wa nyuma?

Unachogombana na uzalendo wa mwalimu wa kuamua kuacha mwenywe kwa ridhaa yake bila kusukumwa na sheria yoyote kama kina kikwete ni nini?

una vita gani na mwalimu/

Bila shaka hilo ni tatizo lako na frustrations zako za failures ambazo kwa nia safi naomba ziabaki kwako na wala usitake kulazimisha na wengine wakufuate. Failures zako hazina uhusiano na mwalimu. unaelewa wwe?
Mkuu usipate tabu na mleta mada. Huyu mtu ana ID mbili na mdini sanaaa!
 
Tuliamini saana katika propaganda hizi kupitia RTD. Eti umoja na kaunganisha watu. Hawa watu kuanzia chama cha TAA walikuwa wanaunganishwa na nani? Kukaa na kujilinganisha na wahutu na watutsi, si kujitendea haki. Nchi hii ina makabila zaidi ya 100. Sio makabila mawili. Babu zetu tayari walikuwa wameoa kwenye makabila tofauti kabla hata ya Nyerere kupata uhuru. Yeye aliwaunganisha nini? Kwnini mifano ni Rwanda, Burundi na Kenye, wale wasiochapana wameunganishwa na nani?
unao uhuru wa kusema utakacho, ninao uhuru wa kufikiri na kuandika nitakacho, na ni tabia yetu wabongo kutopenda kuthamini vya kwetu hivyo siwezi kukushangaa hata kidogo, leo hii Magufuli anasifiwa na waandishi wa habari wa kimataifa lakini hapa hapa nyumbani watu wanakwambia hajafanya kitu! hivyo siwezi kukushangaa unapojaribu kujenga hoja kuwa nyerere hakufanya kitu, ni maoni na ni upeo wako unaokupa jeuri ya kuandika chochote utakacho, kwangu mwalimu nyerere atabakia kuwa mmoja wa viongozi halisi wenye vision waliowahi kutokea barani Afrika. Mataifa mengine yamezama kwenye udini, ukabila na majungu ya ukanda, nyerere alipiga vita uhayawani huo tangu miaka ya 60 mwanzoni, wewe unajaribu kuniambia kuwa hajafanya lolote la maana, jaribu uwe na shukrani japo inaweza isitoke moyoni.
 
Udini, ukanda na ukabila ni matokeo ya uhohehahe na ukosefu wa elimu unaowafanya wachache wajinufaishe kwa mitafaruku ya wengi. Historia za kikabila za nchi tunazozitaja kama mfano ni za muda mrefu kabla ya uhuru. Tuangalie nchi tulizopata nazo uhuru ziko wapi. Au nchi alizoiga nyerere Mfumo wa ujamaa na kujitegemea ziliishia wapi. Ni nini kilifanya nchi yetu isiwe hata na kituo cha television wakati zanzibar na Kenya wakipiga hatua. Yapo aliyofanikiwa kama TAZARA kushirikiana na China ila mengi yanaendelea kubaki propaganda.
 
Nyerere amefanya mengi hilo la TAZARA ni mmoja tu, aliua uchifu tangu enzi za uhuru, na faida zake ni kujenga hali ya umoja. Mchagga anakwenda kusoma A level kule Mtwara, Mgogo anakwenda kusoma A level kule Bukoba. Unajua kinachowatesa Nigeria mpaka leo hii?, ni kushindwa kuondoa uchifu katika maisha yao, leo hii Hausa halali nyumba moja na mtu wa kabila la Igbo, Muigbo halali nyumba moja na myoruba. Nyerere aliweka msisitizo wa umoja, aliweka msisitizo wa kuwatumikia walio wengi. Hakutaka watanzania wajisahau na kujikweza. Anabakia na udhaifu wa kibinadamu lakini kwenye hekima na busara yupo kwenye viwango vya juu sana, ukubali au uamue kukataa hiyo ni juu yako wewe na nafsi yako.
 
"Mimi nang'atuka lakini naendelea kuamini kuwa bila CCM madhubuti, nchi yetu itayumba" J.K. Nyerere 1987.

"HAPA KAZI TU"
 
Mwalimu Nyerere alipotangaza kukaa pembeni mwaka 1985 wengi walihuzunika. Yeye alidai anang'atuka. Kiuhalisia hali ya nchi kiuchumi na wakati vilimsukuma kando.

Siasa zake za ujamaa na kujitegemea za kunyang'anya watu mashamba na kuwarundika sehemu moja zilidhoofisha uchumi.

Utaifishaji wa mali za Watanzania wenye asili ya kiasia ambao hauna tofauti na kilichofanywa Uganda kuliondoa mtaji.

Nchi ilikwenda vitani kwa ahadi ya kurejea katika hali ya muda mfupi baada ya vita haikutokea.

Tukumbuke mwalimu Nyerere tayari alikuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 20 na nchi ilidorora zaidi. Kwahiyo wakati ulimsukuma Nyerere.
Mkuu nakushauri ukimbie tu., Ni vigumu sana kupata sapoti ya watu, kama hoja yako ni kumponda Nyerere.
 
Hayupo tena ktk mgongo wa ardhi.
Sadaqta! Kiwiliwili cha Nyerere ndio hakipo hai, lakini fikira ,udini, mawazo na JINAMIZI lake lipo palepale! linaendelea kututafuna tu
 
Back
Top Bottom