Nyerere day 14 oct 2012 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyerere day 14 oct 2012

Discussion in 'Jukwaa la Historia' started by Abunwasi, Oct 10, 2012.

 1. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #1
  Oct 10, 2012
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Ninafahamu kuwa humu ndani ya jamvi kuna hazina kubwa ya watu wenye uwezo, ujuzi na uzoefu wa mengi.
  Wazo langu ni kuwa kwa kuenzi siku hii kwa nini kwa wale waliokuwa wanamfahamu/kumjua etc tukajuzana alikuwa ni mtu wa aina gani??
  kama mtu wa kawaida tu,
  kama baba,
  kama mwanasiasa,
  kama raisi wa nchi
  ili vijana waweze kuelewa zaidi kwa nini tunamzungumza na kumuenzi hadi leo??? Nawasilisha.
   
 2. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Tarehe 14/10 Kila mwaka ni siku kubwa na ya kukumbukwa nchi Tanzania,ni siku ambayo Watanzania hawatoisahau kwa kuondokewa na aliyekuwa kipenzi chao na mtoboa siri mkubwa kwa mambo yaliyo nyuma ya pazia.Mwalimu hakuwa mnafiki,muoga wala mzandiki katika kuhakikisha ana simamia maslahi ya taifa.

  Mengi yamesemwa na yataendelea kusemwa kila kukicha lakini ukweli utabaki pale pale kuwa yeye ndiye father of the Nation.Kauli zake,vitendo vyake na nia yake vilitosha kumtofautisha na viongozi mbalimbali katika dunia hii.Mwalimu hakuwa na makuu na ndiyo maana siku hii ya kumkumbuka ilitakiwa iwe ni siku maalum ya kujichunguza na kujiangalia kama kweli tunasimamia yale aliyotuasa katika kusuma gurudumu la maendeleo mbele.

  Siku hii itakuwa na maana zaidi ikiwa tutatekeleza kwa vitendo vya ambayo mwalimu aliyaona yana tija kwa mustakabali wa maendeleo ya taifa letu.Ni zaidi ya muongo mmoja tangu atutoke lakini Tanzania imekuwa tofauti na hali aliyoiacha,utadhani aliondoka miaka 50 iliyopita.

  Rushwa imeshika hatamu,matajiri ndiyo walioukumbatia uchumi wetu.Matabaka yanaongezeka siku hadi siku pato la kima cha chini cha mshara ratio yake kwa wastani ni zaidi ya1:60.Mfumuko wa bei kila kukicha,hakuna wakumuogopa mtu,kila mmoja ana peleka mambo yake atakavyo ila mbaya zaidi wanao umia ni maskini walalahoi.

  tunakwenda kumuenzi kwa ushujaa mkubwailihali nchi imeuzwa kwa wageni,hata wale makaburu ambao tuliwaimba sana kama maadui wa haki za kibinadamu ndiyo walio shikiria uchumi wetu.Wameuza mpaka zile benki za makabwela na kuliulia mbali lileshirika letu la ndege ATC.

  Kumbukumbu hizi zingeleta tija pamoja na gharama za maandalizi yanayofanywa huko mkoano Shinyanga kama tungeyakataa yale yote ambayo ni adui wa maendeleo ya taifa letu.Mwalimu aliwahi kusema kuwa tunao maadui wakubwa watatu,njaa,maradhi,umasikini na ujinga.Lakini maadui wetu hao leo hii wamegeuzwa deal.Tunashuhudia madawa fake yanayotengenezwa na kiwanda chetu cha madawa,tumeona jinsi mbolea inavyochakachuliwa kwa mtindo maarufu wa mbolea za voucher.Mitaala ya elimu kila siku ina chakachuliwa hali iliyosababisha watoto wetu kupata bora elimu.

  Rushwa imegeuzwa takrima,nchi inaendeshwa kisanii lakini leo tunatumia kodi za wanyonge kuundaa sherehe kubwa zilizo chini ya mwamvuli wa kumuenzi mwalimu.Si ajabu ukichunguza ndani yake utakuta gharama hewa zimejaa katika maandalizi hayo.

  Wapi tunaelekea wapi ikiwa mwalimu hakuwa muumini wa haya yote yaliyojaa nchini mwetu kama kukithiri kwa ufisadi,rushwa kutamalaki na uwizi wa kimachomacho katika halimashauri zetu.Umoja wa kitaifa umepotea,leo watu wana jadili udini,ukabila na ukanda.Wananchi walijivunia Utanzania wao lakini leo watu wana jinasibu kwa dini na makabila yao.

  Familia imekuwa ndizo zina milki ikulu na hata kufikia kutoa amri kwa vyombo vya dola bila hata kuogopa,si ajabu leo ukasikia mtoto wa Kiongozi fulani ana toa amri kwa vyombo vya dola aidha kwa kuwa tu baba au mama ni kiongozi fulani ndani ya nchi.

  Taasisi za kibenki zinatishwa na wafanya biashara kwa kuwa wana mawasilianao na ikulu,lakini ikifika siku hii Watanzania wakiungana na viongozi wao wana kaa pamojandani ya uwanja mkubwa na kuthubutu kusema wana muenzi Mwalimu.Tanzania yetu itasonga mbele ikiwa tukiacha unafiki na sifa za kijinga ilihali hatutendi kutokana na sifa tunazo mtunukia kiogozi fulani
   
 3. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mwalimu hakupenda sifa za kijinga,alikemea pale panapostahili bila kujali ana wakwaza wengine ambao walikuwa mrengo wake wa kushoto.Hakuona haya kurekebisha makosa ambayo aliamini yana weza kuanagamiza mustakabali wa amani na mshikamano kwa Watanzania.

  Hakupenda kujikweza,alichukia ubwenyeye na kujilimbikizia mali ilihali wananchi wake wnateseka.Alikuwa muumini mzuri wa ujamaa na aliimba kijamaa na kucheza kijamaa tofauti na wenzetu hivi sasa wanaimba kijamaa ilihali wakicheza kibepari.

  Huyu ndiye mwalimu ambaye kila kukicha alipenda kuzungumzia kiongozi na sifa za kiongozi ambaye atayeweza kutuvusha kutoka lindi kubwa la umasikini.Cha msingi tunachotakiwa kujiuliza je tuna muenzi vipi mwalimu ilihali hatutembei ndani ya fikra zake.Nukuu zake hazitotusaidia ikiwa hatutakuwa wakweli.Ifike mahali tuache unduminakuwili na kuweka hisia zetu binafsi kuliko kumuenzi kwa kwa kuimba ilihali tunambeza kiuchezaji.
   
 4. p

  propagandist Member

  #4
  Oct 11, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nyerere ndio kitu .gani? kametulisha unga njano unaotoa wadudu, akumbukwe kwa hilo.
   
 5. s

  sendisha Member

  #5
  Oct 11, 2012
  Joined: Oct 11, 2012
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kila taifa lina historia na hatuwezi kuzungumzia historia ya Tanzania bila kumzungumzia nyerere na hatuwezi kupinga mawazo ya wengine wanaoona tofauti kuhusu mwalimu hata mahatma gandhi pamoja na kuipigania India lakini bado walimuua.
   
 6. s

  sendisha Member

  #6
  Oct 11, 2012
  Joined: Oct 11, 2012
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa kiasi kikubwa bado si kwa viongozi wala wananchi walio "commited" na kumuenzi mwalimu nyerere yani ni kama bado tunatania likija suala la kumuenzi huyu mtu.Nyerere alisoma alama za nyakati kipindi hicho na aliona kwamba watanzania bado hawastahili kuachiwa hii nchi bila ya yeye, kwa hiyo tukirudi ktk hoja kuu bado hatuenzi na hatusimami ktk yale aliyoamini mwalimu.
   
 7. kibol

  kibol JF-Expert Member

  #7
  Oct 11, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 3,135
  Likes Received: 378
  Trophy Points: 180
  jina lako linasadifu wasifu wako,asante kwa hilo mkuu.
   
Loading...