​na jamaa wa bagamoyo kampanga nani kuwa mrithi wake?
Jamani huu ni husia wa baba. Kasema black and white clear bila chengachenga.
Kama Chadema wako serious watauacha mchakato uwe huru na wa haki. Katika mazingira hayo yeyote anaweza kuibuka mshindi.
Mchakaato hauwezi kuwa huru na wa haki wakati tayari kuna mtu ana billions toka sehemu mbalimbali hata nje ya nchi (Kama Machali alivyoelezwa na Kafulila). Tuelezwe kwanza hao wanaompatia mapesa toka nje wamelenga nini. Quoting Mwalimu, akiingia Ikulu atayarudishaje hayo mapesa? Will he be different from Kikwete?Kama Chadema wako serious watauacha mchakato uwe huru na wa haki. Katika mazingira hayo yeyote anaweza kuibuka mshindi.
Hiv Watanzania kwanini tunaacha kufikiri, kazi kunukuu kila alilolisema Nyerere na kugandia hapohapo...
Tuna wasomi kibao, watu wenye akili timamu na wanaoweza kufikiri mawazo mapya na kuacha huu mgando wa mawazo eti ni kumuenzi mwalimu..
we chinja chinja vipi? Badala ya kuijenga ccm yenu unajifanya unamtetea zito. Acheni unafiki kujifanya mnamtetea zito kumbe udini na uchonganishi umewajaa. Na safari hii mmenoa. Kampeni yenu imeshindikana, mkitaka kumuweka mzenji ndo kabisaaaaa! Naona mnajaribu kete yenu kwa zito, hamtaweza na mtaendelea kuabika.
Kwani alichokisema mwalimu katika hili kina ubaya gani?
Tunafahamu woga walionao CCM kama CHADEMA watamsimamisha Dr. Slaa, kwahiyo juhudi zao na propaganda zao za kujaribu kuleta mfarakano ndani ya CHADEMA zinaeleweka, tunafahamu kwamba VIBARAKA mtatumika katika suala hili, mbinu zenu tunazijua na namna ya kukabiliana nazo tunafahamu, adhabu ya vigogo na vibaraka wao inafahamika, hata mfanye propaganda zipi ANGUKO LENU 2015 HALIKWEPEKI, nasikitika sana kwa ujinga unaowafanya vibaraka msaliti wananchi na ndugu zenu masikini, TAFAKARINI SANA, KWANI MUDA BADO UPO.
Chi boy inaelekea madarasa hayajatosha. Hv unaweza kufanya uchunguzi au kutaka kutatua jambo katika jamii bila kufanya marejeo ya wale waliokumbana na tatizo kama hilo au linalofanana na hilo. Mwl. Nyerere ni reference point yetu na hakuna kichwa chochote hadi sasa katika nchi hii kinachokaribia kichwa cha mwalimu. Tatizo la wana cdm ni kukifanya chama hicho kuwa cha kabila fulani na wasio kabila hilo (niwaite-koloni la kabila hilo) wanapiga debe la utumwa bila kujijua. Angalia trend hii! Lyatonga na NCCR_MAGEUZI(kabila hilo liko nyuma yake), Lyatonga na TLP(kabila hilo liko nyuma yake). Siri ilipofichuka kuwa kuna ajenda ya kikabila ilyoshindikana kushika nchi, ikawa hivi- Freeman na Chadema (kabila hilo liko nyuma). Ikashindikana kuchukua nchi, mpango ukawa huu.....
Kwishney! JK kaliangamiza taifa kwa udini. What next?