Kwanza huyo Nyerere hakuwa na hata haya kutetea uongo ufanane na kweli. Alidai anawachukia makaburu, na hali alikuwa anajuwa kabisa, tulikuwa tunawauzia tumbaku, na wao wanatuuzia Land Rover, hata zile almasi za Mwadui wana hisa kubwa tu...!
Nje kwenye vyombo vya habari alijionyesha kama mpenda haki na mpigania uhuru, lakini kwa ndani alikuwa akifanya kinyume chake.
Nyerere ndani ya nafsi yake alijua kabisa kuwa yeye si mpigania haki, kwa sababu aliwanyima Watanzania haki ya kuyatoa mawazo yao.
Hivi wale wote leo wenye kuweza kupanua vinywa vyao na kuwasema viongozi wa serikali na chama tawala, enzi ya Mchonga wangethubutu?
Ndivyo alivyofanya Nyerere, na kuna watu watakuja hapa na kudai kuwa Nyerere alikuwa ni mzalendo.
Enzi hizo uzalendo ni kuwaweka watu kizuizini na kutunga sheria ya kuwashitaki wakati wako kizuizini.
X-paster uliyashuhudia haya,achana na hawa waliosimuliwa makanisani mwao.
Kwenye hadhara akisema udini mbaya lakini akiwa ikulu hujisifu kwa kusema sikumchagua huyu kuwa waziri kutokana na uwezo wake katika siasa bali kutokana na imani yake (ukatoliki).
Kaka hayo ndio mawazo yangu finyu na huyo ndio Nyerere.... aliye wanyima Watanzania haki ya kutoa mawazo yao...!Mi naomba nikupongeze kwa mchango mzuri. Mimi mtu kama X-plastaz huwa na shindwa kumwelewa na sina hakika kama amesoma na kuijua vilivyo historia ya nchi yake vizuri. Nampa changamoto moja then next time akija kwenye jukwaa la wasomi kama hili aje akiwa timamu. nakuomba X-plastaz kasome essays on socialism and Education for self reliance. Ndo utajua kama Mwl. aliweka misingi mibovu ama la, matatizo tulionayo leo yameletwa na baadhi ya watu wenye mawazo finyi kama yako,walio shirikiana na wazungu.
Na ilo ndio lilikuwa tatizo kubwa sana, aliwafumba macho wengi kwa kisingizio cha kutaifisha mashule ya dini, kumbe ilikuwa njia ya kuzipatia ruzuku toka serikalini, shule za kikatoliki zilifaidika sana kwa tendo ilo.Bahati mbaya sana kuna watu hawaoni kitu ila kwa kutumia kioo cha udini. Kama kuna watu waliosaidiwa sana na Nyerere enzi za utawala wake kwenye upande wa elimu walikuwa waislamu. Nyerere alitaifisha shule zote za madhehebu ya dini na kuzifanya za umma. Nyingi kati ya hizo zilikuwa za kikristo. Kwani Kikwete alisoma shule gani?
Alikuwa msemaji mzuri kweli kweli, na hotuba zake zilivutia haswa, na aliyeweza kuutetea uongo ukafanana na kweli.Alikuwa msafi na mkweli faraghani na hadharani!