Nyerere alipostaafu alienda kijijini kulima wengine wanaandama kwenda ikulu

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
14,409
13,259
Baba wa taifa Mwl. J. K. Nyerere alipostaafu urais alirudi zake kijijini kwake Butiama kulima. Alikwenda Dar mara chache kama hasa nyakati za kuimarisha chama alipokuwa bado mwenyekiti na baadaye alipoachia akatulia zake kijijini mpaka alipougua na kwenda Uingereza kwa matibabu hatimaye Mungu akamchukua

Nimeshangaa baada ya rais wa awamu ya tano JPM kuingia madarakani kumekuwa na wimbi la marais wastaafu kuandamana kwenda ikulu kana kwamba kuna mizigo walisahau wakati wanaondoka. Mmoja ndio alitia fora alienda kuomba kazi kabisa eti yuko tayari kufanya kazi yoyote. Wa awamu ya 2 na 3 wao wamepotea mpaka njia za kwenda vijijini kwao walikoloa siko kwao kwa asili. Badala ya kwenda kushirikiana na wanavijjiji katika vijiji vyao kama alivyofanya Mwl wao wamehama kabisa labda mpaka siku wakifumba macho ndio waanze kurudishwa kwao. Aliyeomba kazi kapata ya kusuluhisha Burundi. Huyu mwingine naona kwasababu ya ukaribu wa kutoka kijijini kwake na ikulu naona anajisahau kama amestaafu hivyo mara anajikuta ameingia ikulu mara kwa mara. Taratibu atazoea. Wamwache JPM afanye kazi na kama nao ni majipu au waliacha vijipu vya pale State house wajue vitatumbuliwa!
 
Vicent Mshindi ataviweza vitu vy Dr. Slaa?
 
Back
Top Bottom