Watu wengine Bana! Eti amekashifiwa tena ? Kwani si tunaona kila siku watu wakitukanwa matusi ya nguoni humu?
Achana nayo hayo hayatusaidii humu sisi! Si tunadai uhuru wa kusema ? Waache waseme watakavyo nawe andika lako kwa mwengine . Tuachie sisi na raha zetu.
Yaani kumkashifu mtu, ama kumtusi mtu ndio uhuru wa kusema?!! Uhuru wa kusema una mipaka. sasa wewe unapata raha gani baba wa taifa lako anapotukanwa?
Yaani kumkashifu mtu, ama kumtusi mtu ndio uhuru wa kusema?!! Uhuru wa kusema una mipaka. sasa wewe unapata raha gani baba wa taifa lako anapotukanwa?
Ngekewa, unaweza kutafsiri unavyoweza neno '' Bangi'' sababu kila mtu ana uwezo tofauti wa kufikiri. kwangu mimi bangi inabaki kuwa bangi tu, kama ilivyo nyekundu itabaki kuwa nyekundu. sipo hapa kukuaminisha kwamba nyerere katukanwa ama lah!Unaposema Baba wa Taifa langu una maana gani zaidi ya sifa tu au heshima? Hata hivyo huyo Baba hakuwa Saint kwamba hakuwa na mabaya. Sasa tunaposema mabaya yake unasema katukanwa? Naam wewe unahisi Bangi ni majani lakini kwa wengine Bangi inaweza kuwa jambo jengine na hilo jambo pengine ndilo alilolikosea na kulaumiwa, sijui ni kashfa hiyo?
Ngekewa, unaweza kutafsiri unavyoweza neno '' Bangi'' sababu kila mtu ana uwezo tofauti wa kufikiri. kwangu mimi bangi inabaki kuwa bangi tu, kama ilivyo nyekundu itabaki kuwa nyekundu. sipo hapa kukuaminisha kwamba nyerere katukanwa ama lah!
Kwa hakika hii ni typing error. Tusibishane kwa ajili ya typing error. Nyerere alitaifisha shule ili Waislamu waweze kusoma. Mimi nimesoma katika shule ya Kikristu na Waislamu wengi. Waislamu wanasema zamani shule za Kikristu ndizo zilikuwa nyingi,Wakristu tu ndio waliokuwa wanasoma,Wakristu tu ndio waliokuwa wanapata ajira. Na Nyerere ndiye aliyerithi huo mfuom kutoka kwa Wakoloni,eyey ndie alikuwa kiongozi,kwa hiyo,unaweza kusema, kwa hali fulani,yeye ndie mwenye makosa.
Sheikh Kassim bin Juma alikuwa ansema,''Kila unapomuona mtu maskini Tanzania,more often than not,atakuwa ni Mwislamu,ndio maana tunasema hii nchi ina mfuom-Kristu,na hayo yote yameanza wakati wa Nyerere.......''
Sijakuelewa. fafanua zaidi
Kumkashifu!!!
Labda nikuulize wewe, mtu akisema ''Bangi la Nyerere'' hapo wewe unaelewa nini? kawaida kwa hali ya sasa na tamaduni za kitanzania, jamii inamchukulia mvuta bangi kama ni mtu ambaye ni mhuni, asiye na mwelekeo. bila kusahau pia , kwamba wagonjwa wengi wa vichaa na matatizo ya akili wanahusishwa na matumizi ya bangi ama madawa mengine ya kulevya. sijui, una maoni gani?
Kwani pale tunapomlaumu spika bungeni na wengine wakimsifu wewe unahisi vipi? Unachokiona wewe kizuri usimlazimishe mwenzio akione kizuri na yuko wazi kukieleza atakavyo. Hivyo wewe unafikiri sote Bangi tunaiona ni mbaya?
Kashifa kwa mimi ningeona kuwa ni matusi na sio mtazamo tofauti wa mtu juu ya fulani.