Nyerere 1999 - 2009: Alipotuacha na tulipo

JoJiPoJi

JF-Expert Member
Aug 8, 2009
2,907
3,261
miaka 10 sasa tangu muasisi wa taifa letu mzee wetu mwl. JK Nyerere atutoke, katika kipindi hiki ambacho tunakumbuka miaka hiyo je viongozi wetu wanamuenzi huyu mzee kweli, au ndio ameondoka na fikra zake ambazo zingewasaidia hawa viongozi kuiendesha nchi ktk misingi imara.
 
Hakuna ubishi kwamba mwalimu ana mazuri mengi sana,lakini huyu alikuwa mwanadamu.Naomba mtujuze maeneo ambayo alikuwa akichemsha ili tuweze kujifunza kupitia makosa yake pia.
 
hakuna ubishi kwamba mwalimu ana mazuri mengi sana,lakini huyu alikuwa mwanadamu.naomba mtujuze maeneo ambayo alikuwa akichemsha ili tuweze kujifunza kupitia makosa yake pia.

kwanza alikuwa dikteta,hadi wakamwita baba haambiliki,,..
Pili alikuwayeye ndo serikali na serikali ndo yeye
alivunja katiba na kufukuza watu waliompinga.
Na mengine mengi......
 
Uzuri na ubaya wa hayati mwalimu mtafuteni James mapalala atawaelezea kiundani kama si Mzee Mtei nadhani na yeye ni memmer humu Please Changia mzee!
 
Uzuri na ubaya wa hayati mwalimu mtafuteni James mapalala atawaelezea kiundani kama si Mzee Mtei nadhani na yeye ni memmer humu Please Changia mzee!

Hivi huyu Mapalala na Fundikira wapo wapi?
 
Wakati wa Mh. Nyerere, Shule zilikuwa bure, Hospitali bure, dawa unapewa bure, wakati ule, mnapewa madaftari bure pamoja na vitabu, penseli, kalamu ya biki

Kaazi kweli kweli ......
 
wakati wa mh. Nyerere, shule zilikuwa bure, hospitali bure, dawa unapewa bure, wakati ule, mnapewa madaftari bure pamoja na vitabu, penseli, kalamu ya biki

kaazi kweli kweli ......

nyerere ilikuwa serikali inawamiliki wananchi,wakati inatakiwa
serikali imilikiwe na wananchi,,
 
Marufuku kusafiri.
Marufuku kununua gari,
kumiliki tv ni kuhujumu uchumi,
hakuna shule wala vyuo binafsi.
 
Hakuna ubishi kwamba mwalimu ana mazuri mengi sana,lakini huyu alikuwa mwanadamu.Naomba mtujuze maeneo ambayo alikuwa akichemsha ili tuweze kujifunza kupitia makosa yake pia.
Kama mpaka leo unatafuta elimu juu ya uchemshaji wa Mwalimu basi hakuna alilochemsha. Ni kama vile unatafuta sindano kwenye gunia la unga.
 
miaka 10 sasa tangu muasisi wa taifa letu mzee wetu mwl. JK Nyerere atutoke, katika kipindi hiki ambacho tunakumbuka miaka hiyo je viongozi wetu wanamuenzi huyu mzee kweli, au ndio ameondoka na fikra zake ambazo zingewasaidia hawa viongozi kuiendesha nchi ktk misingi imara.
Nyerere alikosea unintentionally while aiming at the good for the people. Viongozi wa sasa wanakosea intentionally to aim at their good!
 
na sisi wananchi kwa nafasi yetu kweli tunamuenzi kama muasisi wa taifa letu
 
kwanza alikuwa dikteta,hadi wakamwita baba haambiliki,,..
Pili alikuwayeye ndo serikali na serikali ndo yeye
alivunja katiba na kufukuza watu waliompinga.
Na mengine mengi......


wapumbavu bila udikteta kidogo hawaendi..
Je mafisadi walikuwa wapi enzi zake??
Mbona kina kingunge walikuwa waadilifu sana enzi za ticha m'bigi?
Utawala nyoronyoro kama huu wa sasa ni hatari kwa maendeleo ya taifa letu na vizazi vijavyo.
Leo tofauti ya kipato ni kubwa sana kati ya walionacho na wasionacho.
hakika tanzania kumpata kiongozi kama nyerere itatugharimu zaidi ya miaka mia moja.
tutamkumbuka daima
 
maendeleo yaliyokuwa Uganda wakati wa Iddi Amini mpaka leo hajafikiwa, maendeleo yaliyokuwa chini ya Hitler mpaka leo hayajafikiwa na wajerumani., nchi bila udikteta uwezi kuwa na umoja na maendeleo ya kweli, wachina wako advance kwa sababu hiyohiyo, huo ubepari unaozungumziwa marekani ni wa watu wachache mno ndio walioshika nchi na wanaomtaka awe raisi huwa (refer election Bush vs Gore)Nyerere kawasaidia sana watoto wa walala hoi, kama Nyerere angeruhusu huo uhuru watu walioumiss kipindi chake hii nchi isingekuwepo ilipo sasa, kama Nyerere angekuwa na sera kama za mwinyi,Mkapa na hata sasa JK hii nchi sasa isingekuwepo, watoto wote wa wakubwa wa serikali tulikuwa tunagombania nao vyakula pamoja mashuleni( nakumbuka tulikuwa Tambaza na watoto wa Gen Kiaro wakati huo akiwa mkuu wa Majeshi), lakini sasa hata mtoto wa katibu kata yupo nje ya nchi. Nyerere hakuwa mbinafsi, hao wote waliokuwa wanampinga hata kama wapo humu, walikuwa kwa maslahi yao binafsi
 
Nyerere alilinda mafisadi, kiongozi akiaribu au kuiba hashitakiwi anapewa ulaji mwingini, yeye ndo kaanzisha sera ya kulindana ndani ya CCM

hauitaji kuwa Economist kujua TZ chini ya Nyerere ilikua imeshaoza kuanzia barabara, hakuna vyakula nk,,,,,,,,,

Ilanampongeza kuamua kuachia ngazi mwenyewe, huu ndo uzuri pekee anaweza kusifika
 
nyerere ilikuwa serikali inawamiliki wananchi,wakati inatakiwa
serikali imilikiwe na wananchi,,

ndio maana,gari imenasa kwenye REVERSE GEAR


Hivi wabongo wapo tayari kulipa kodi kama Wamarekani ili kujenga nchi? Kila ukivuka darada unalipa toll, na sasa wanaweka tax kwa kila mile unayo endesha gari? Are we ready for that? By end of the year kutakuwa na tax ya clean air? Wakulu wabongo wapo tayari kulipa hizo kodi? Maana ile kodi ya maendeleo wakati ule, iliwafanya watu washindwe kutembea kwa sababu walikuwa hawana vipande! Mnakumbuka miaka ile ya late 80's?

It is easy to say certain things, but execution ndio mtasema kuwa Serikali inawafisadi.

Kitu kilicho ua Tanzania ni vita ya Uganda ya kumfuraisha Milton Obote. Kabla ya vita Bongo ilikuwa njema tu.
 
kwa kweli nyerere alikosea sana kulinda waliokuwa wanaharibu badala ya kufukuza. Mtu alikuwa anafilisi shirika hili anahamishiwa kwingine nako anafilisi lakini hakuna hatua zilizo kuwa zinachukuliwa.

Kwa upande wa mazuri makubwa, namshukuru nyerere kwa kutuondolea ukabila ingawa CCM ya sasa inataka kurudisha ukabila.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom