DOKEZO Nyaya zinazoshikilia nguzo zinaibwa zinatumika kufungia Linta!

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
kilimo ndo hicho cha kuangalizia mvua....
Mbona bibi yako mpk leo ni mkulima na halalamiki?

Hivi umekaa na kutafakari kwa nini uhalifu unaongezeka?
Twambie wewe uliyetafakari.

halafu dola hiyo hiyo inawaua watuhumiwa wa wizi....
Ulitaka wafanywe nn? Yaani sasa hivi ni mwendo wa risasi tu. Kama una ndugu mwizi mwambie aache atapigwa risasi tu.

Dola inahakikisha vijana wanakosa hata fursa ya kujiajiri
Kivipi? Acha kujilegeza wewe
 
Morogoro road, watu wameiba vifuniko vya midomo ya ku-drain maji ya mvua...

Chunguza barabara kuanzia Ubungo hadi Fire, utaona vifuniko vingi vishabebwa...
 
Ndugu Mteja

Tunashukuru sana kwa ushirikiano wako mzuri, tunaanza uchunguzi maramoja Kupitia idara yatu ya usalama (Security) tutafurahia zaidi kama utaweza kutusaidia mtu au eneo wanaofanya hivyo ili tuanzie hapo,
Na nyinyi wenyewe acheni kuibia watu, nguzo zinatoka hapo mafinga zinauzwa kwa bei yote hiyo?
Na bado zikinunuliwa zinabaki kuwa Mali ya Shirika?!

Bila rushwa kuunganishiwa umeme ni muujiza! Acha na nyinyi muhujumiwe mjue uchungu wake.
 
Sasa hivi hadi taa zinazotumia solar vibaka wanaiba batteries na hizo solar panels. Nchi imekuwa ya ajabu sana sijui tuna laana gani? Na muda si mrefu watamalizia na hizo nguzo kwenda kuuza scrapers.
Kufeli kwa mfumo au tusime total colapse of our system. Mambo haya huchangiwa na mambo mengi sana lakini source yake ni uongozi mbovu. Rais anaweza kutumia nguvu kuiba kura, watu wakadhani madhara yake yanaisha mara uchaguzi unapokwisha ´kumbe ndiyo yanaanza. Kwa kifupi kila ovu linalofumbiwa macho na uongozi au jamii linazaa maovu mengine, na yale maovu yanazaa mengine na mengine...
 
Kwahiyo solution ya hayo yoooote ni MTU kuwa Jambazi au sio ?

Haya endelea kuwa Jambazi ni Shaba tu

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
Acha kuwa short sighted wa ubongo mazee. ''Shaba tu'' ingekuwa inatatua matatizo kama haya basi dunia hii isingekuwa na kibaka hata mmoja. Watu kama nyie pengine ndiyo viongozi mnaoamua mambo ndiyo maana kila siku ijayo inakuwa afadhali ya jana. Unajaribu kutatua tatizo complex kwa njia ya mkato. Hutafanikiwa.

Kwa wale walikuja Dar siku nyingi watakumbuka kuwa panya road wamekuwepo siku nyingi na zamani walikuwa wanaitwa komandoo yoso na hawakuwa wameenea sehemu nyingi kama ilivyo sasa. Kuna kipindi waliuawa sana, tena na raia wenyewe lakini matokeo yake sasa hivi ''wamezaliana'' na kutapakaa Dar yote. Haya ni matokeo ya sera mbovu za uongozi na hayawezi kutatuliwa kwa ''shaba tu''.
 
Hao watu kwanini wasitusaidie kuangusha minara ya simu. Maana siyo kwa utapeli huu na wizi wanaotufanyia.

Siyo voda, tigo, airtel, halotel wote wanajichukulia tu pesa zetu.
 
Hao watu kwanini wasitusaidie kuangusha minara ya simu. Maana siyo kwa utapeli huu na wizi wanaotufanyia.

Siyo voda, tigo, airtel, halotel wote wanajichukulia tu pesa zetu.
Tatizo la utapeli wa vifurushi? Hili kuliondoa ni ngumu kwa sababu kunawa hakuna ushahidi wa wazi. Mfano unaweza kununua kifurushi cha mb 1000, kikaisha haraka sana lakini namna ya kuonyesha kuwa umeibiwa inakuwa ni ngumu.

Mambo kama haya yanaweza kuondolewa na post-paid payments, lakini kwa nchi yetu hili ni vigumu kulitekeleza kwa watu wote. Ingekuwa vizuri kuwe na mikataba ya muda na siyo MB. Kwa mfano tarehe moja unaambiwa lipa sh 10, 000 na mwezi mzima uwe na access ya internet.
 
Ndugu Mteja

Tunashukuru sana kwa ushirikiano wako mzuri, tunaanza uchunguzi maramoja Kupitia idara yatu ya usalama (Security) tutafurahia zaidi kama utaweza kutusaidia mtu au eneo wanaofanya hivyo ili tuanzie hapo,
Ushauri wangu ni kwamba. Nyaya ngumu za kushikiria nguzo ziwekewe madini ya kuditect hata zikijengewa unaweza kuzipata kirahisi. Nilisikitika sana Tanzania kufikiwa wizi huu kisa ughari wa nondo.
 
Wanaofanya hivyo ni watoto wetu, ndugu zetu, marafiki zetu, majirani zetu.

Wakikamatwa wakatwe viganja vya mikono ili hao wazazi wao, ndugu zao, marafiki zao, majirani zao wapate uchungu waanze kuwalea wezi wao.
 
Back
Top Bottom