Jodeny
JF-Expert Member
- Mar 26, 2012
- 201
- 25
Hili ndio tatizo la watanzania wengi na wavivu wa kufikiri na kuchanganua mambo. Katika mamlaka na taasisi nyingi nchini watendaji na hasa viongozi wameoza, lakini inapotokea waziri anapoamua kusafisha ili kuweka mambo sawa watu wanaanza kumshambulia na wengine kuweka hisia za uonevu na ubabe. Nani hafahamu Dk. Mwakyembe alivyoshambulia kwa kumuondoa Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Efraim Mgawe ambaye madudu yake yalikuwa yanatia kichefuchefu mbele ya dunia. Inaingilia akilini kwa TPA miaka yote wateja kulipia fedha dirishani? meli kukaa zaidi ya mwezi bila kupakua mizigo, wizi wa vifaa vya magari kama vioo, redio, power window na ilifika mahali hadi tairi zinazovuliwa bila hofu. Lakini yote hayo baada ya Mgawe kuondoka imekuwa historia sasa unaweza kuagiza gari ukaweka hata dola 100 kwa kuitegesha na ukaikuta ndani.
NOTE: Tuwe wakweli pale TTB kuna uvundo ambao kila mwenye akili anapaswa kuuondoa na si Nyalandu pekee. TTB inafanya kazi gani ya kutangaza utalii, tunasahau kashfa ya matangazo ya utalii nje ambayo mabilioni ya shilingi yalipigwa. Why Kenya na vinchi vingine vidogo vinatushinda kwa kuwa na idadi kubwa ya watalii kuliko Tanzania? Kazi yao kubwa ni kubebana na mahawara zao kwenda kwenye maonyesho ya kimataifa ulaya wakiwa wamebeba vipeperushi 50, tuache mambo ya ajabu ya kulea watendaji wabovu na wanaotufanya tuwe nyuma kimaendeleo muda wote. Bravo Nyalandu.