LOVI MEMBE
JF-Expert Member
- Mar 16, 2012
- 1,122
- 183
Wengine tumeshindwa kuifungua hiyo attached file.
Mkuu Kiranga, there you are!, jana nilipomsikiliza Nundu, nilimhurumia kujaribu kuzuia deal la ulaji kwa nia njema kabisa ili kuliokoa taifa, bila ya kujua who is behind!. Hao CCCC wameshaanzia juu!. Sasa huyu Nundu kutia kauzibe atageuzwa mbuzi wa kafara!.
Comonsense logic inalazimisha kuamini ile deal ya rada, gulf stream, richmond etc sio tuu zilikuwa na baraka kutoka juu, bali pia mgao ulitangulia na ndio final benefisharies wa ile tozo!.
Mkuu Kimbunga, mambo mengine wee acha tuu!.
Nimeuliza nani anaejua hao CCCC wamepatikanaje?, hakujatolewa tangazo lolote hata la EOI tuu achilia mbali tender!.
Laiti watu wangelimjua who is behind Mfutakamba, mtagundua Nundu ni mtu wa kuhurumiwa tuu!.
Nchi hii inajengwa na wenye moyo kama Nundu na inaliwa na wenye meno kama Mfutakamba!.
Mkuu kwa kweli hawa mawaziri wetu wanaweza kufanya maamuzi ya kijinga namna hii bila hata kuwa na woga?Sijapenda habari za kutoa bandari rehani kwa miaka 45.
Jamaa hawana huruma hata kwa watoto wao wenyewe! Sijui wanajiona wao ndo watawala wa mwisho wa Tanzania?
Kiranga, na bado watadai tuna chuki, tuna wivu na wavivu wa kufikiri.Mwana miaka 45 unaijua? Mie ujanja wangu wote sijaifikisha. Mtu anaweza kuzaliwa leo, akaenda shule, chuo, akawa rais na kuwa rais mstaafu ndani ya miaka 45!
Voyager imekuwa launched 1977 kufikia 2011, takriban miaka 34 (miaka kumi na moja kabla ya kufikisha miaka 45) ilikuwa inatoka nje ya solar system.
Hivi miaka 45 tunaielewa? Tangu uhuru wetu ndiyo kwanza tumefikisha miaka 50, tunataka kusaini mkataba wa miaka 45 kweli? Si tunarudi kwenye ukoloni tena tu hapa?
Sijapenda habari zao, kutoa bandari rehani kwa miaka 45.
Mutauana bure
Wewe una assume Wachina wanajali fairness ndiyo maana unashindwa kuwaelewa. Hawajali. Wanajali economic interests zao tu. Ndiyo maana wanawekeza popote pale, kwa Gaddafi, Mugabe, Al-Bashir, Ahmadinejad etc.Human Rights na fairness kwao si jambo kubwa.
Wachina hawana tatizo na kampuni ya kichina kutoa rushwa kwa mtendaji wa kampuni/ serikali ya Tanzania ili kupata tender kirahisi Tanzania.Sina hakika hata kama Wachina wana sheria za kubana makampuni yao yasitoe rushwa nje kama sheria za Kimarekani zilivyo kwa mfano "Foreign Corrupt Practices Act" Foreign Corrupt Practices Act - Wikipedia, the free encyclopedia (Wal-Mart wana scandal kwa kutoa rushwa ili wapate competitive advantage Mexico, rushwa imetolewa Mexico na Wal-Mart Mexico lakini kwa kuwa kampuni tanzu ni la Kimarekani wanataka kushtakiwa Marekani)
Ila kama unatoa rushwa kwa mtendaji wa Kichina ili kampuni ya Tanzania ipate tenda kirahisi rahisi China, ikijulikana huyo mtendaji wa kichina anaweza hata kupewa adhabu ya kifo.
Mambo ya mkuki mtamu kwa nguruwe kidizaini fulani hivi. Wanacheza rafu sana lakini hawataki kuchezewa.
Sijapenda habari za kutoa bandari rehani kwa miaka 45.