Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 59,252
- 133,448
Mkuu Kimbunga, mambo mengine wee acha tuu!.Mkuu Pasco una maana beneficiaries walishachukua chao mapema hivyo PIGA GAUZA CCCC lazima wapewe na ili waweze kurejesha pesa walizotoa. Hata hizo za Mfutakamba ni sehemu ya hizo pesa. Watu wanachukua upfront Mkuu. Unaambiwa chetu mapema kabisaaa sasa Nundu anapoingia kuzuia ndipo yanapomkuta hayo yanayomkuta! Anapigwa dana dana, anabezwa na kushambuliwa toka kila upande!
Jana nilivyomuangalia kwenye TV nikaona ana siri kubwa moyoni hakutaka tu kutaja ila Naibu wake ametaja. Ustaarabu tu wa kikazi na kutawalana mahala pa kazi; hata kama Naibu Waziri anapata ruhusa toka kwa Waziri Mkuu lakini si inabidi umuage Waziri wako? Utaondokaje bila Waziri wako kufahamu? Mfutakamba alitumwa?
HUjaeleweka mkuu
Unasafishaje mtu kwa barua moja
Ninachokiona hapa waliopo nje wanapiga ''jaramba'' na ''mataulo'' na waliopo ndani wako bize kupiga ''tikitaka'' na mataulo !! .......... Sasa kunoga !!!Nimeshawahi kusema kwasasa Serikali ya JK nguo,zinaanza kudondoka mojamoja. Hatimaye itabaki uch *** hapo ndipo kwenye swali nani ataitupia TAULO Serikali ya JK ili isibaki uch***?
Sawa. Je, hao CMHC wakoje gharama zao? Na wakipewa Tender, CCCC watalipwa?Mkuu Kimbunga, mambo mengine wee acha tuu!.
Nimeuliza nani anaejua hao CCCC wamepatikanaje?, hakujatolewa tangazo lolote hata la EOI tuu achilia mbali tender!.
Laiti watu wangelimjua who is behind Mfutakamba, mtagundua Nundu ni mtu wa kuhurumiwa tuu!.
Nchi hii inajengwa na wenye moyo kama Nundu na inaliwa na wenye meno kama Mfutakamba!.
Ninachokiona hapa waliopo nje wanapiga ''jaramba'' na ''mataulo'' na waliopo ndani wako bize kupiga ''tikitaka'' na mataulo !! .......... Sasa kunoga !!!
Rushwa ilivyokithiri hujui nani mkweli kibaya zaidi tunaoathirika ni watanzania.
Chama
Gongo la Mboto DSM
Naomba kutofautiana na wewe Mkuu, wana CCM hawaathiriki kwa lolote kwenye hizi Rushwa zilizokithiri maana kwa mwanaCCM ni kwamba hii nchi uchumi unapaa na ilani ya CCM inatimizwa vyema kabisa, na kwenye ule uchaguzi wetu wa ndani hii inaitwa takrima.Rushwa ilivyokithiri hujui nani mkweli kibaya zaidi tunaoathirika ni watanzania.
Chama
Gongo la Mboto DSM
kuna haja ya kutengeneza flyer Za "accountability made simple" kwa ajili ya watu kama HALISI
Mkuu Kobelo, kwenye mikataba kuna mikataba inaitwa void na voidable, mkataba ukishakuwa void unaitwa "void ab initio" wakimaanisha hakuna mkataba hivyo kila mtu inakula kwake!.Sawa. Je, hao CMHC wakoje gharama zao? Na wakipewa Tender, CCCC watalipwa?
Kwanini hakubatilisha Tender na mkopo kutoka China Exim? Kuepusha mashtaka? Aliwasiliana na CCCC?
Hebu tusaidieni hizo nyaraka za Naibu Waziri alivyohusika. Maana kama alihongwa tiketi ya ndege na vijifedha, aliyesema hayo ni Nundu ambaye anataka kutuambia, Naibu alimzidi nguvu, sasa hebu tujiridhishe kabla ya kubeba maneno ya mwizi mtoto anayesema sikuiba peke yangu!!!
Kwa hiyo Nundu naye ni BANGUSILO tu.Endeleeni kumwaga nondo na mimi kesho nakuja na zangu!. Jee nani anajua hao CCCC walipatikanaje?. Jee kuna tenda yoyote ilitangazwa?!. Jee walijuaje TZ tunataka kupanua bandari?. Jee nani aliwapa kibali cha kufanya feasibility study?. Wangapi mnajua kuwa good practice ni feasibility study kufanywa na mwingine, funding kutafutwa kwa mwingine, construction company iwe nyingine na consultants ni wengine for checks and balance!. Jee ni wangapi mnajua feasibility study wanefanya hao CCCC, consultants ni wao wao CCCC wakaja na hiyo figure ya dola milioni 500 plus bila any independent verification na mkopo wakaomba hao hao CCCC kutoka Exim Bank?. Why?. Tangu lini unaomba mkopo alafu banker anakulazimisha usipofanya kazi na CCCC no mkopo!.
Mbona Mombasa wamejenga kwa 200 why sisi tujenge kwa 600?!.
Hivi mnajua kiburi na jeuri ya Mfutakamba inatoka wapi?. Mnamjua nani anampa ruhusa kwenda kuhongwa huko nje huku akimby pass boss wake?!. Nnajua aliandika recomendation ya kuifagilia CCCC na kuisubmit wapi bila kumuonyesha waziri?. Amini nawaambieni hao CCCC ni yule yule RA!. Kama Richmond tuu ila this time sio US ni China!. Hivi mnanuamini Serukamba?!. Mnaamini ni yeye ndie aliyeomba kuwa M/Kiti wa Kamati ile?. No amewekwa kama alivyo pewa ubunge!. Yeye ni remote tuu ya RA!.
Endeleeni kumwaga mboga kesho na sisi tunamwaga ugali wakose wote!. Kusema ukweli napandwa na hasira sana mpaka natamani nchi hii tungekuwa kama China, mafisadi wana kula bullets soonest possible na kusahaulika!.
Mchukua Nundu na Mfutakamba uwapime nani fisadi na nani sio!. Tatizo la ufisadi ni kubwa kuliko nilivyodhania maana mpaka humu jf vibaraka wao, wametamalaki sana!.
Mungu Ibariki Tanzania!. Nawahakikishia kama 2015 Watanzania wataamua kufanya kweli, kuna wenzetu humu humu watatafuta pa kutokea maana kwao pia ni kilio na kusaga meno!.
HUjaeleweka mkuu
Unasafishaje mtu kwa barua moja
Jamaa hawana huruma hata kwa watoto wao wenyewe! Sijui wanajiona wao ndo watawala wa mwisho wa Tanzania?