Kampuni hii inashikilia kiwango kikubwa cha miradi ya makandarasi wazawa ktk ujenzi wa barabara, bila ya kuwa na matokeo mazuri. Kampuni hii ilipigiwa kelele wakati rais akiwa Bunda kwa kutofanyakazi vizuri. Walikimbilia huko na sasa hakuna kinachoenedelea tena. Ikapigiwa kelele kwa kandarasi za Halmashauri ya Temeke DSM. Wakakimbilia huko na kujidai kutibua barabara na sasa kimyaaa!
Takribani kazi nyingi za ujenzi na ukarabati wa barabara za mikoani kila sehemu ni Nyanza. Naomba kufahamu nani anamiliki kampuni hii, ambayo inaonekana kutoguswa na nguvu ya wanasiasa, pamoja na ubora duni wa kazi zao na wingi wa kazi zisizomalizika.