Nyanya moja yauzwa kwa shilingi 300

radika

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
20,438
32,248
Nakumbuka miezi kadhaa ya nyuma wakulima wa nyanya walizimwaga na kulisha ng'ombe mkoani Morogoro wakilalamikia ukosefu wa soko la badhaa hiyo. Mambo ni tofauti tena bidhaa hiyo imekuwa adimu tena.

Mtaani kwetu nyanya moja inuuzwa kwa shilingi mia tatu hali ni tete na ukizingatia mvua kuna baadhi ya maeneo hazinyeshi huko tuendako kuna kiza kinene maisha kadri siku zinavyokwenda kuna baadhi ya bidhaa zinakuwa adimu achilia mbali suala la mzunguko wa pesa lilivyokuwa kugumu.

Unga wa sembe na mahindi havizungumziki navyo bei yake yazidi kupanda maradufu hali ikoje mitaani kwenu wadau?

Tuendelee kuliombea taifa letu baadhi ya maeneo wapate mvua za kutosha.
 
Jamaa yangu anaoiga heka ya hatari, ni mkulima wa nyanya hapa Mwanza. Kila siku nasikia anaimba jembe in Mali, madalali wanampa yeye 10% badala ya yeye kuwapa wao. Nyanya moja ya kawaida sh 300 na zaidi.
 
Nikiwa Tanzania sijanunuwa nyanya zaidi ya miaka mitano sasa, kuishi shamba raha sana.

Suala sio kuishi shamba, kujitambua na kutumia akili vizuri, mshukuru Mungu wewe unajielewa. Kuna watu wanaishi shamba na hauwezi kuamini wananunua kila kitu. Ubongo kufunguka ni kitu muhimu sana.
 
Ni juzi tu nyanya sanduku ilikua elfu 7, sasa kama imeadimika ni muda wa kupumzika kula nyanya, halafu hivi hamna wajasiriamali wanaoweza kuzikausha na kuzihifadhi ili kipindi kama hichi waiabalance bei ? Nyanya moja mia 3 kwetu uswazi mia 3 ni tembele 3 ugali unaliwa
 
Back
Top Bottom