Habari ya asubuhi ndugu zangu. Ninahitaji mbegu ya nyanya isiyo na bei ghali lakini inafanya vizuri na kutoa mazao bora.
Moja ya changamoto kubwa ya wakulima wa nyanya sasa hivi ni bei kubwa ya mbegu. Kampuni zinazozalisha mbegu sasa hivi zikiona mbegu yao inafanya vizuri tu wanaacha kuziweka kwenye package za uzito (gram/kg) na kuziuza kwa hesabu ya mbegu.
Wanauza mbegu 500 kwa Tsh. 30,000.00 mpaka 40,000.
Kwa mkulima anayetaka kulima kuanzia ekari 1 inayochukua miche kuanzia 12,000 ni changamoto kubwa sana kununua mbegu hizi. Kama unalima ekari 2 pesa ya mbegu tu unatakiwa kuandaa kuanzia Tsh.1,500,000.00 kwa ajili ye mbegu tu bado gharama zingine.
Naomba wale ambao wamelima mbegu tofauti za hybrid watupe uzoefu wao wa mbegu zinazofanya vizuri lakini hazina bein ghali sana.
Mbegu kama Kipato F1 inafanya vizuri katika mbegu zisizokuwa ghali lakini kuna uwezekano kuna mbegu uliyolima ikafanya vizuri ukaifurahia inaweza kuwa bora zaidi.
Karibuni.