Of all people Nyamlani hawezi kusema kwamba hatavumilia rushwa, mahakama ya Kinondoni Mh Nyamlani kupitia kwa mwendesha mashtaka wake Magoma (spelling sina hakika nazo) ndio wanaongoza kuchukua rushwa kubwa kupita wote.
Nina experience na hawa jamaa, Nyamlani nitamchukia mpaka naingia kaburini, ana Verossa yake hivi ukishamwona anaingia ujue cash imekutoka, halafu haheshimu muda wa watu, ana dharau sana huyu mtu.
Unaweza ukawa na kesi mnamsubiria yupo ndani hatoi maelezo yoyote labda muondoke mje saa ngapi, baada ya muda unamwona huyo anaondoka na Verossa yake, kurudi ni saa kumi na nusu au saa kumi na moja, sasa hata kama una kesi huna haki ya muda jamani! Sasa ukosee useme ngoja nitoke kidogo, akirudi ukaitwa haupo, wewe tena umelala ndani, kupata removal order ni Laki 3 mpaka 4 hapo.
Nyamlani? Nyamlani? Nyamlani? Naomba aje akiri kwamba anajirekebisha kwa hili la rushwa na kuheshimu watu kwanza, na yule mwendesha mashtaka wake Magoma! We waache tu.
Jamaa anajua fitina sana, ana roho mbaya, ndio maana walitaka kura ya ndiyo na hapana kule mwanzo.
NINA HASIRA NAYE, NAMWOMBA MUNGU ANISAIDIE HASIRA ZA ALICHONIFANYIA NYAMLANI ZIISHE, NIPATE MOYO WA KUMSAMEHE NA KUSAHAU KWA KWELI.
NB: Naomba kama kuna mtu anaweza kumtumia haya niliyo andika kwenye email yake afanye hivyo, ninaumia na ninaendelea kuumia kwa haki niliyodhulumiwa na Nyamlani, dharau aliyonifanyia na rushwa kubwa aliyoniomba, na mengine mengi ya kutojari muda wangu. Asnteni.