Nyama ya nguruwe yachangia ugonjwa wa kifafa – Daktari

Inside10

JF-Expert Member
May 20, 2011
26,060
23,941
nguruwepic.jpg

Aveline Kitomary – Dar es Salaam

DAKTARI Bingwa wa Ubongo, Uti wa Mgongo na Mishipa ya Fahamu kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Patience Njenje, amesema ulaji wa nyama ya nguruwe ambazo hazijaivishwa vizuri, umekuwa ukisababisha ongezeko la ugonjwa wa kifafa kwa asilimia 15.

Dk. Njenje amesema hatari ya ulaji wa nyama hizo inatokana na wanyama hao kuwa na minyoo aina ya tegu ambayo ina uwezo wa kusasabisha uvimbe kwenye ubongo.

Akizungumza wakati alipokuwa akitoa elimu kwa jamii jana Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kifafa Duniani, Dk. Njenje alisema sababu zingine za ugonjwa wa kifafa kuongezeka ni ajali.

“Sababu za kifafa ziko nyingi, ajali inachangia kwa asilimia 10 mpaka 15 ya wagonjwa nchini, ongezeko linakuja kutokana na kuongezeka kwa aina ya usafiri wa bodaboda ambapo ajali inapotokea mtu huweza kuumia kichwa na ukiumia kinachofuata ni ubongo kuwa na kovu, hivyo huko mbeleni unaweza kupata kifafa.

“Vivimbe ndani ya ubongo hivi viko vya aina nyingi, ila kuna viwili vikubwa. Kuna vivimbe vya minyoo na saratani, mfano ulaji wa nyama za nguruwe ambazo hazijaiva mtu anaweza akapata tatizo kwani ile kitimoto ina wadudu wa minyoo ambao wataingia ndani ya mwili na wataenda kwenye ubongo.

“Pia kuna minyoo kwa paka, kama kinga ikishuka wana uwezo wa kukushambulia na kupanda hadi kwenye ubongo, hivyo kupelekea uvimbe, kingine ni uzazi wa shida, hii inasababisha kifafa kwa asilimia 30, mfano mama akiwa na njia ndogo ya uzazi halafu mtoto akashindwa kutoka na hii huzuia hewa kwenye ubongo wa mtoto,” alisema Dk. Njenje.

Alisema utafiti uliofanyika hapa nchini unaonyesha katika kila watu 1,000 watu 37 wana tatizo la kifafa, huku zaidi ya watu milioni 60 wakikumbwa na tatizo hilo duniani.

“Kwa kila mwaka kuna ongezeko la watu 70 kati ya 100,000 duniani kote, hivyo kidunia ugonjwa huu una kasi kubwa, hasa kwa upande wa Afrika ugonjwa huu uko mbele mno ambapo katika kila watu 1,000 watu 50 wameathirika na kifafa, asilimia kubwa wanatoka Afrika.

“Tafiti zilizofanyika kama ule wa Mahenge, Morogoro wa ugonjwa wa kifafa kwa Afrika, Tanzania inaongoza, kwahiyo hili ni tatizo kubwa, wagonjwa wana hatari ya kufa mara sita zaidi ya mtu ambaye hana kifafa,” alibainisha Dk. Njenje.

Alisema kuwa asilimia 36 ya jamii wana imani potofu kuhusu ugonjwa huo, hali ambayo imesababisha wagonjwa wengi kutokufika hospitali kwa wakati au kutofika kabisa.

“Asilimia 50 ya jamii bado wanaamini kifafa ni ugonjwa wa kuambukizwa kitu ambacho si kweli, huku zaidi ya asilimia 75 ya wagonjwa wa kifafa wakienda kutafuta tiba kwa waganga waa kienyeji na viongozi wa dini wakiamini kuwa ugonjwa huo unasababishwa na mashetani.

“Kwahiyo tunapoteza watu ingawa katika jamii watu wamekuwa wakiishi kwa mazoea na kuwa na imani mbalimbali kuhusu kifafa, wengine wanaamini sio ugonjwa wa kawaida, wanasema ni kulogwa au majini,” alisema Dk. Njenje.

Chanzo: Mtanzania
 
Sawa tumekuelewa kumbe ni zile zisizoiva vizuri,ila kama imeiva haina shida, Ngoja mchana nikifika kwenye ile kona ya kitimoto ntamwambia muuzaji aichemshe vizuri kilo yangu na maji ya moto, halafu ikiiva aikatekate then aikaange rosti, aweke kachumbari nyingi, pilipili na chumvi kidogo kwa mbali na ugali,nadhani ntakuwa salama kabisa...
 
Kungekuwa na uwezekano wa kumhoji huyu Doctor ingekuwa ni vema sana,why analiongelea hili suala bila ya kuja na ukweli,JF always ina watu wanaosoma upande wa pili kujua ukoje ili FACTS zisipotoshwe,kula nyama ambayo ni mbichi au under cooked ya nguruwe hakuna tatizo la kiafya,UNLESS nyama hiyo ime kuwa infected with parasitic worms,au na Trichinella spirallis na hii itapelekea kuleta ugonjwa wa Trinchinosis na risk yake ni ndogo sana,na kuihusisha nyama hii na kifafa ni kuleta mihemko na kama mtaalamu anaongea kama wanasiasa wetu hapo ndipo utatambua kuwa nchi hii bado sana.ILA ni muhimu kuwa chochote unachokula jitahidi kiwe katika mazingira bora ya kuliwa,kama ni nyama hakikisha haijawa infected ndio maana kwenye mahoteli wateja wengine wanaagiza nyama yao iwe Rare(hii ni salama tu kama nyama nayo ni salama).
 
Asante kwa taarifa muhimu kama hii.
View attachment 1355068
Aveline Kitomary – Dar es Salaam

DAKTARI Bingwa wa Ubongo, Uti wa Mgongo na Mishipa ya Fahamu kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Patience Njenje, amesema ulaji wa nyama ya nguruwe ambazo hazijaivishwa vizuri, umekuwa ukisababisha ongezeko la ugonjwa wa kifafa kwa asilimia 15.

Dk. Njenje amesema hatari ya ulaji wa nyama hizo inatokana na wanyama hao kuwa na minyoo aina ya tegu ambayo ina uwezo wa kusasabisha uvimbe kwenye ubongo.

Akizungumza wakati alipokuwa akitoa elimu kwa jamii jana Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kifafa Duniani, Dk. Njenje alisema sababu zingine za ugonjwa wa kifafa kuongezeka ni ajali.

“Sababu za kifafa ziko nyingi, ajali inachangia kwa asilimia 10 mpaka 15 ya wagonjwa nchini, ongezeko linakuja kutokana na kuongezeka kwa aina ya usafiri wa bodaboda ambapo ajali inapotokea mtu huweza kuumia kichwa na ukiumia kinachofuata ni ubongo kuwa na kovu, hivyo huko mbeleni unaweza kupata kifafa.

“Vivimbe ndani ya ubongo hivi viko vya aina nyingi, ila kuna viwili vikubwa. Kuna vivimbe vya minyoo na saratani, mfano ulaji wa nyama za nguruwe ambazo hazijaiva mtu anaweza akapata tatizo kwani ile kitimoto ina wadudu wa minyoo ambao wataingia ndani ya mwili na wataenda kwenye ubongo.

“Pia kuna minyoo kwa paka, kama kinga ikishuka wana uwezo wa kukushambulia na kupanda hadi kwenye ubongo, hivyo kupelekea uvimbe, kingine ni uzazi wa shida, hii inasababisha kifafa kwa asilimia 30, mfano mama akiwa na njia ndogo ya uzazi halafu mtoto akashindwa kutoka na hii huzuia hewa kwenye ubongo wa mtoto,” alisema Dk. Njenje.

Alisema utafiti uliofanyika hapa nchini unaonyesha katika kila watu 1,000 watu 37 wana tatizo la kifafa, huku zaidi ya watu milioni 60 wakikumbwa na tatizo hilo duniani.

“Kwa kila mwaka kuna ongezeko la watu 70 kati ya 100,000 duniani kote, hivyo kidunia ugonjwa huu una kasi kubwa, hasa kwa upande wa Afrika ugonjwa huu uko mbele mno ambapo katika kila watu 1,000 watu 50 wameathirika na kifafa, asilimia kubwa wanatoka Afrika.

“Tafiti zilizofanyika kama ule wa Mahenge, Morogoro wa ugonjwa wa kifafa kwa Afrika, Tanzania inaongoza, kwahiyo hili ni tatizo kubwa, wagonjwa wana hatari ya kufa mara sita zaidi ya mtu ambaye hana kifafa,” alibainisha Dk. Njenje.

Alisema kuwa asilimia 36 ya jamii wana imani potofu kuhusu ugonjwa huo, hali ambayo imesababisha wagonjwa wengi kutokufika hospitali kwa wakati au kutofika kabisa.

“Asilimia 50 ya jamii bado wanaamini kifafa ni ugonjwa wa kuambukizwa kitu ambacho si kweli, huku zaidi ya asilimia 75 ya wagonjwa wa kifafa wakienda kutafuta tiba kwa waganga waa kienyeji na viongozi wa dini wakiamini kuwa ugonjwa huo unasababishwa na mashetani.

“Kwahiyo tunapoteza watu ingawa katika jamii watu wamekuwa wakiishi kwa mazoea na kuwa na imani mbalimbali kuhusu kifafa, wengine wanaamini sio ugonjwa wa kawaida, wanasema ni kulogwa au majini,” alisema Dk. Njenje.
Msaada: Nyama ya nguruwe yachangia ugonjwa wa kifafa – Daktari | Mtanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukitaka ujue kama hio nyama ni haram, chukua hio nyama thn ingiza kwenye kibakuli alaf chukua Coca-Cola pure ichanganye after 45 maximum masaa mawili alaf njoo unipe mrejesho kitu utakachokiona

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ulikuwa unatafuta nini kufanya yote hayo???
Uliona nini ambacho huwezi kukisema mpaka na sie tukatumie muda na kuchanganya vyote hivyo,,

Kama haikuhusu kutokana na dini yako bora ukapita kimya kimya maana hizi sababu mfu hazituzuii kuendelea kula nguruwe

Coca nayo ni sumu hata mimba inatoa, msumari ukiuweka ndani yake unayeyuka kuwa kutu ndani ya muda mfupi tu

Tutamla leo kesho na hata milele,, ilmradi iive vizuri

HAMTUTISHI
 
Back
Top Bottom