Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 977
- 1,965
Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii katika Serikali ya Awamu ya Nne, Lazaro Nyalandu, amesema kuwa safari yake katika mikoa ya Singida, Tabora, Kigoma na maeneo mengine kumnadi mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, amethibitisha kuwa hamasa ya wananchi ni kubwa, upendo wao ni wa dhati kwa chama na mgombea.
Akiwa mkoani Kigoma, Nyalandu, ameongeza kuwa umati wa watu wanaojitokeza si wa kulazimishwa bali ni uthibitisho wa imani na matumaini waliyonayo kwa sera na mwelekeo wa uongozi wa Rais Samia.
Kwa mujibu wa Nyalandu, hali hii ni ishara kwamba uchaguzi mkuu ujao wa Oktoba 29 utakuwa na kishindo kikubwa cha ushindi kwa CCM kutokana na mvuto mkubwa wa mgombea wake.