Ulukolokwitanga
JF-Expert Member
- Sep 18, 2010
- 8,396
- 7,968
Kwa mshangao wangu waziri Nyalandu anaitangazia dunia kuwa Zanzibar iko salama hivyo watalii waendelee kuitembelea Zanziba na serikali itawahakikishia usalama. Je utalii ni suala la Muungano? Je wazanzibari hawana msemaji hadi mtu wa Tanganyika aitangazie dunia. Hivi sisiemu mnanufaika nini na muungano hadi mnawabana ndugu zetu wa visiwani kama luba. Nyalandu uwaziri wako wa utalii huku Tanganyika haukupi uhalali wa kuisemea Zanzibar kwa kuwa wanaye waziri wa utalii, kauli yako inawapa kichwa wale WAHUNI wanaofanya vurugu na kuona ZnZ yao ni dili kwa sisi wabara