Nyalandu: Ripoti ya Lembeli uongo mtupu

Nyalandu: Ripoti ya Lembeli uongo mtupu

UZEE MVI

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2011
Posts
232
Reaction score
58
Nyalandu: Ripoti ya Lembeli uongo mtupu

nyalandu1-300x169.jpg


NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, ameilalamikia Kamati ya Bunge ya Ardhi, Mazingira na Maliasili iliyoongozwa na James Lembeli kuwa taarifa iliyowasilisha bungeni na kuwang'oa mawaziri wanne ilikuwa ya uongo.

Nyalandu alitoa kauli hiyo juzi alipozungumza na viongozi wa taaluma mbalimbali pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dodoma na Manyara juu ya mgogoro wa mipaka kati ya hifadhi ya taifa ya Tarangire, Pori la Akiba Nkungunero na vijiji vya jirani uliofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara.

Alieleza kutokana na taarifa hiyo Tanzania kwa sasa imeonekana kushuka kwa kiwango kikubwa katika utawala bora ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Alisema kuna taarifa ambazo zilionyesha kuwa wapo watu ambao walibakwa jambo ambalo halikuwa la kweli.

Hata hivyo, alisema kwa sasa Rais Jakaya Kikwete amekubali kuunda tume ya kimahakama ambayo itafanya uchunguzi juu ya kuwepo kwa matukio hayo na itakapabainisha kuwa kuna watu walipotosha ni wazi watachukuliwa hatua kali za kisheria bila kujali cheo cha mtu ambaye alihusika na uongo au ukiukwaji wa sheria.

Katika hatua nyingine, Nyalandu ametangaza kumsimamisha kazi ofisa wanyamapori mwandamizi katika pori la akiba la Maswa, Lawrence Kileo, kwa kutuhumiwa kupokea rushwa na kuwatoza faini wafugaji bila kuzingatia taratibu.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku chache tangu atangaze kusimamishwa kazi kwa watumishi 22 wa wizara hiyo.

Ofisa huyo anatuhumiwa kuwatoza faini wafugaji wanaoingiza mifugo yao katika pori hilo bila kutoa risiti za serikali, na hivyo fedha hizo kujinufaisha mwenyewe kinyume cha kifungu cha sheria namba 116[2]C cha sheria ya kuhifadhi wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009.

Nyalandu ametangaza kuanza kwa uchunguzi kwa Ofisa Wanyamapori wa Wilaya ya Kasulu, Benjamini Mkosamali, kabla ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa kuwaruhusu watuhumiwa wa ujangili kuondoka na nyara za serikali walizokamatwa nazo kabla ya kukamatwa tena kwa msaada wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Nyalandu alisisitiza kuwa serikali itaendelea kuchukua hatua zaidi kwa maofisa wote watakaobainika kujihusisha na vitendo vyovyote vile vya kukiuka maadili ya kazi yao.

Watuhumiwa hao wa ujangili mkoani Kigoma ambao walikamatwa wakiwa wamebeba wanyama aina ya tohe 12, madume watano na majike saba wakiwa pia na insha wanne aina ya Oribi ambao hawakupaswa kuwinda kwa mujibu wa leseni yao ya uwindaji namba B59921 iliyotolewa Kigoma.

Alisema awali watuhumiwa hao walikamtwa na kikosi cha doria cha Kampuni ya Friedkin Conservation Fund na kumuita ofisa huyo kwa ajili ya kuchukua hatua zaidi ambapo alipofika na kuzungumza na watuhumiwa aliwaruhusu kuondoka na wanyama hao.

Nyalandu alisema Benjamini akiwa na taaluma ya kusimamia wanyamapori huku akifahamu majangili waliokamatwa wamekutwa na nyara za serikali na wamekutwa katika kitalu cha uwindaji sehemu ya Kibenge, baada ya kupata taarifa kwa wahusika, aliamua kwa makusudi kuwaruhusu majangili hao kuondoka.

"Hivyo nimeagiza mamlaka husika kukamilisha uchunguzi na kumchukulia hatua za kinidhamu na za kisheria haraka sana ofisa huyo," alisema Nyalandu.

Alisema kuwa vita dhidi ya ujangili itaendelea kwa kasi na hata rais ameishaahidi kuwa operesheni ujangili awamu ya pili itarejea hivi karibuni baada ya kurekebisha kasoro zilizojitokeza katika awamu iliyomalizika.

Alifafanua kuwa kwa kipindi cha mwezi mmoja uliopita baada ya kusitishwa kwa operesheni hiyo, tembo 60 waliuawa na majangili hao kitendo ambacho hakitakiwi kuvumiliwa.

Source:
Tanzania Daima (Tanzania Daima – Nyalandu: Ripoti ya Lembeli uongo mtupu)
 
Sidhani kama kuna uwongo kwenye ripoti hiyo,ila ni njia ya kujaribu kujiosha taka.namuone huruma sana kwani wakati wa kuwadanganya watanzania umekwisha.Pili viongozi wa serikali hawapendi kuambiwa ukweli na pia hawapendi kuona serikali inatupiwa mawe na ukweli ukajulikana.
 
Amuulize Bosi wake?Mi nashangaa kwanini bado yupo!kwani wizara zao si zimetenguliwa na JK....wanajifanya hamnazo
 
Nyalandu nae anatakiwa awe ameshaachia ngazi nashangaa anasubiri nini kwa sababu nae alikuwa ni kiongozi kwenye wizara ya maliasili.
 
Ni serikali ya wamu hii ndo naona utawala na Bunge marazote hawaaminiani, ripoti ya Bunge kutokuamini wa na Utawala siyo mara ya kwanza, nakumbuka ile ya Richimond, Ile ya mwaka 2012 iliyowang'oa akina Mige, Ngereja. Mimi sikubaliani na ripoti ya Lembeli kushindwa kuwataja Wabunge Majangili, Ndiyo yaleyale ya Lukuvi kutuaminisha kuwa tukiwataja wauza unga nchi itayumba badala ya kusema CCM ndo itayumba maana naamini wangekuwa siyo watu wa CCM, Lukuvi angewataja na hata Lembeli angewataja.

Tuajifanya kuficha UGONJWA lakini MADHALA/DALILI zitatuumbua. Ndovu wanaisha, vijana wanaishia kufungwa magerza za ughaibuni eti tunawalinda majangili na wauza sembe kama hawakichangii chama au ni marafiki zenu kwanini muwe na kigugumizi?
 

''Alisema kuwa vita dhidi ya ujangili itaendelea kwa kasi na hata rais ameishaahidi kuwa operesheni ujangili awamu ya pili itarejea hivi karibuni baada ya kurekebisha kasoro zilizojitokeza katika awamu iliyomalizika.''

Ripoti unaitaja kuwa ni ya uongo, halafu unatuambia utendelea na vita baada ya kurekebisha kasoro zilizojitokeza ambazo naamini umezibaini baada ya ripoti hiyo, sasa unatuambiaje tena kuwa ni ya uongo!!!!
 
Nyalandu ni mjinga, hafai kuwa kiongozi wa umma.
Kwa nafasi yake km naibu waziri wa serikali hapa amekurupuka
 
Nyalandu hajawahi kuwa sahihi tangu amekuwa waziri. Daima ni mbabaishaji
 
Nyalandu anatumia sana majungu kuukwaa uwaziri na km kikwete hajawa makini ataingizwa mkenge na huyu jamaa
 
Hebu wadau nidadavulieni. Je hii yaweza kuwa na ukweli fulani au ni yaleyaele?

Umewahi kujiuliza ni nani alipiga picha wakati yule jamaa ana...za mti? au ni wakati gani kwenye maeneo yote ya matukio picha zilipigwa na nani alihariri?
 
Kama anakanusha kwamba walibaka,basi anakubali kwamba waliua,swali langu ni kama waliweza kuua watashindwaje kubaka?
 
Porojo za nyalandu tu hizi. Alikuwa wapi mda wote? Hakuwepo wakati inasomwa? Mtaka vyeo huyu
 
Wajanja wajanja wa mjini na wapiga deal ndo wenye kuongoza maamuzi ya serikali. Who is Nyalandu,? Katokea wapi mpaka kufikia hapo alipo? Ni nani aliye nyuma yake? Na, je Ni juhudi zipi anafanya kujipatia nafasi anazozitafuta? Mimi sijui, ila nahisi naye Ni JANGA la Taifa.
 
kapalamsenga

Uko sahihi mkuu ila nadhani naibu waziri huyu alitakiwa aseme ina mapungufu badala ya kusema ni uongo mtupu.
Inawezekana Lembeli akawalinda wenzake kama alivyofanya Hosea wa akukuru kwenye issue ya richmond
lakini hapa mh.lazaro hakutakiwa kusema kuwa ni uongo bali alitakiwa ajazie pale penye mapungufu kama kweli yeye ni mkweli.
 
Last edited by a moderator:
Nlivyosikia anamsalandia Faraja kota nikajua kumbe na yeye ni mtu wa mabebez kama le big show!
 
Back
Top Bottom