Kihesabu ni Kosa kubwa sana ulilolifanya hapo.
Nimemsifia kwa makubwa ambayo wewe hukuyaona,nikosoe kwa kufukuwa nisiyoyajua lakini yawe KATIKA HILI.
Habeeb Marhan
Kafanya kazi kubwa ipi...!?
Tuelezee sio wote wanafahamu...!
Mengi amefanya kupitia Mgongo wa Serikali na Wahanga wenyewe wa Ajali, hivi ni nani angeshindwa kufanya aliyo yafanya....!?
Au ni kwa kuwa yeye aliwahi tu....!!?
Anyway.....PONGEZI NYALANDU..
Sent using Jamii Forums mobile app
Sifa za utendaji mzuri unaoondoa shida za jamii ndiyo miongoni mwa sifa za kiongozi wa watu,sifa bora kwa mabadiliko na maendeleo ya watu.Habeeb anayemponda Nyalandu katika hili msamehe bure. Laiti mngelijua ushiriki wa Nyalandu katika hili. Lakini Kama sifa au kama mnavyoita kutafuta Kiki zinatafutwa kwa kufanya alichofanya Nyalandu basi ameipata na jamii inamkubali.
Mimi pia kama wewe,ila namsifu kwa mfululizo wa matukio.Mimi binafsi siomfuasi WA nyalandu ila kwahili nampongeza sana kaonyesha uzalendo(utu)kupita ninavyomfahamu
Salamu za jumapili kwa kila atakayesoma.
Nimeona nimpongeze Nyalandu kwa moyo wa dhati sana katika msaada kwa watoto walionusurika katika ajali ya LUCKY VICENT.
Mtaani watu wanaongea kama Nyalandu anatafuta sifa au mtaji wa kisiasa kwa jinsi alivyokuwa mstari wa mbele kusaidia matibabu kwa watoto walionusurika.
Mimi namtazama kama mtu mwenye huruma sana,mzazi mwenye uchungu,kiongozi asiye mbinafsi.Tukio halikutokra jimboni kwake lakini hakujali hilo,hapo anatafutaje kiki ya kisiasa?
Wapo wenye uwezo wa kuleta tofauti katika jamii kwa ushawushi wao tu(influence)lakini pasipo na jambo linalowaubganisha moja kwa moja huwa hawajitoi kufanya lolote,naamini NYALANDU angekuwa mbinafsi basi angekaa kimya tu,uwezo wa kula Jodari anao lakini hakuacha kufanya analoweza.
Hakufanya kwa maslahi ya kifedha,zaidi naamini atajuwa katika eneo fulani ametumia fedha zake,lakini wapo walionufaika na tukio lile.
Tuwatie moyo wenye moyo wa kujitolea,haki yake kumsifu kwa hili.
Naomba tumsifu pamoja,si lazima tueaze sawa,munaweza pia kuwaza muonavyo.
Habeeb Marhan
Hakuna mwanadamu aliyemkamilifu kama mungu,na hatatokea.Nachelea kutoa pongezi, bora tu nitoe.
Nyalandu ni Mbunge wangu toka 2000 hadi sasa,
Mengine ya jimboni kwake ambayo ni madogo au makubwa yanasikitisha sana.
Sitaki kuyasema humu bali nawapeni uwanja msifie.
NB: Si kila furushi(robota) kubwa la nguo lililopambwa kwa kila aina ya pambo juu ndani yake lina nguo nzuri, mengine unawezakukuta ni midoli
Samaki hukunjwa angali mbichi, na mtoto umleavyo ndivyo akuavyo, hao watoto wamejifunza kitu muhimu na kikubwa katika maisha ni umuhimu wa kujitoa kwa ajili ya wengine, labda kama nawe ni bunga hujui elimu kwa vitendokwa hili anastahili pongezi kwa kweli...kama huko ni kutafuta sifa ndio huko basi tunahitaji viongozi watafuta sifa........
ila alinishangaza alipowaweka watoto wake mbelembele kwenye shughuli ya kuwakaribisha watoto wale,
Pongezi Nyalandu kuwa mwenyekiti mwenza tuliache tuendelee kupongeza kama mtoa mada atakavyo.Nimelazimika kukubaliana na mtoa mada,Nyalandu kwenye hili big up/thumb up au vyovyote ikavyokuwa sawa.
Nilisikia kuwa ni mwenyekiti mwenza wa taasisi iliyoleta ndege ya kuwabeba.
HONGERA NYALANDU
Nongwa sasa hiyo!,nilimaliza kwa kusema "unaweza kufikiri tofauti",si lazima tufanane kwenye kuwaza mjomba,ila ukiacha kupongeza au kama huoni sababu basi unawrza kutujuza amekosea wapi.Pongezi Nyalandu kuwa mwenyekiti mwenza tuliache tuendelee kupongeza kama mtoa mada atakavyo.
Huyo siyo mgeni na wazungu,katika kusomasoma humu mtandaoni hadi nilikuta mahali mtu ameandika kuwa huyo ana DUAL CITIZENSHIP(sina uhakika),na pia ana marafiki wengi wazungu,Americans in particular.Jimbo lake lina matatizo ya kutosha, mbona hafanyi hivyo? sema siku hiyo ni wale wageni wakizungu ndiyo wamesababisha awe msitari wa mbele.
Nami nilishangaa kuona hilo. Utaratibu mzima ulikuwa wa ovyo. Watu walifika mpaka kwenye ngazi ikawa vurugu tu. Kwa nini wazazi/wababa hawakupewa haki yao badala yake wapewe watoto wa Nyalandu? Saying that haina maana hatumpongezi Lazaro kwa kushughulikia swala zima kama mtumishi wa umma. Hawakujiandaa kuwa na mkalimali wazungu wale walikuwa wanashangaa what's next kwenye kupewa zawadi. MC ndio kabisaaaaa ovyooo hata shule hawakuwa na utaratibu mzuri. All in all Tunamshukuru Mungu Watoto wamerudi wakiwa na afya njema thou Doreen bado ana safari ndefu Mungu azidi kumponya. Hivi waziri wa Afya hakualikwa Mbunge naye je?? Swali la kizushi!kwa hili anastahili pongezi kwa kweli...kama huko ni kutafuta sifa ndio huko basi tunahitaji viongozi watafuta sifa........
ila alinishangaza alipowaweka watoto wake mbelembele kwenye shughuli ya kuwakaribisha watoto wale,