Uchaguzi 2020 Nyalandu: CHADEMA tukiingia Ikulu tutaanzisha benki ya vijana

Nyanswe Nsame

Senior Member
Jul 9, 2019
158
175
NYALANDU: Chadema tukiingia Ikulu tutaanzisha benki ya vijana

Mtia nia wa kugombea urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Lazaro Nyalandu amesema endapo chama hicho kitampa ridhaa, atahakikisha anarudisha utashi na udhubutu wa vijana kuamini wanaweza.

Pia amesema atajenga mifumo imara ya uendeshaji wa nchi na kufufua ndoto za wananchi pamoja na kuandaa kijana wa kitanzania katika kumudu ushindani wa ajira katika soko la ajira ndani ya afrika.

Nyalandu anazungumza na wanafunzi wa vyuo mbalimbali ikiwemo Chuo Cha mtakatifu agoustino (Saut), chuo cha afya cha Tandabui, chuo cha biashara CBE, Chuo Cha Maendeleo ya Jamii na Chuo cha uhasibu (TIA).

Katika hatua nyingine, amesema kupitia chama chake wataanzisha benki ya vijana kwa kuwa vijana wengi wana ndoto za mafanikio lakini mitaji imekuwa ni tatizo ili vijana waweze kujiajili.

BY CHARLES MSETI
 
Hiyo benki itawapa pesa vijana au ni jina tu? Mbona zilianzishwa benki za wanawake na za kidini, kawaulize zimewasaidiaje?
 
Katika hatua nyingine, amesema kupitia chama chake wataanzisha benki ya vijana kwa kuwa vijana wengi wana ndoto za mafanikio lakini mitaji imekuwa ni tatizo ili vijana waweze kujiajili.

Huu ni upuuzi sio siasa

1. Mikopo yote Ina BIMA, kampuni gani ya bima itakayokua tayari kuudhamini mkopo wa mtu ambaye hana dhamana (mali isiyohamishika).

2. Wakisema Serikali ndio idhamini Serikali itaingia chaka kwani vijana ni asilimia 65 ya watanzania wote hivyo hiyo mikopo itarumia zaidi ya nusu ya pato la Serikali ambalo halina uhakika wa kurejeshwa.

3. Vijana wamejaa tamaa na kiufupi hawafai kupewa hela ambayo hawajaifanyia kazi.

Ahsante
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom