Nyalandu awatimua wamachinga wa kigeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyalandu awatimua wamachinga wa kigeni

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Ustaadh, Jan 7, 2011.

 1. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2011
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  [FONT=&quot]Wafanyabiashara ndogondogo ‘wamachinga' wa kigeni wametakiwa kuondoka ndani ya siku 30 ili kuacha watanganyika kufanya biashara hizo.[/FONT]

  [FONT=&quot]Naibu Waziri wa Biashara an Viwanda, Lazaro Nyalandu alisema jana wakati alipotembela soko kuu la Kariakoo jijini Dar kuwa wageni wote kutoka nchi za Asia na Afrika wanaojihusisha na biashara hizo waache ama wafuate taratibu za uwekezaji nchini.[/FONT]

  [FONT=&quot]Hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa wamachinga kutoka Mataifa mbalimbali ya Afrika na Asia kufanya shughuli hizo kinyume na vibali vyao,jambo ambalo linawanyima fursa wazalendo kufanya kazi hiyo.[/FONT]

  [FONT=&quot]Akizungumza baada ya kufanya ukaguzi kwenye soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam jana,Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Lazaro Nyalandu alisema kuwa, idadi kubwa ya wageni hao kufanya shughuli hizo kinyume na taratibu imesababisha serikali kukosa mapato.[/FONT]

  [FONT=&quot]Alisema,kuna baadhi ya wafanyabishara wameomba kibali cha uwekezaji,badala yake wameshindwa kufanya hivyo na kuanza shughuli za umachinga huku wakiwaita ndugu zao kinyume na taratibu, kutokana na hali hiyo serikali haitawaacha, itawashughulikia.[/FONT]

  [FONT=&quot]"Wale wote wanaofanya shughuli za umachinga kinyume na vibali vyao waache mara moja na kuondoka nchini kwao kabla yakuchukuliwa hatua za kisheria, kutokana na hali hiyo watendaji weote watapita kwa kila wafanyabishara kwa ajili ya kufanya ukaguzi,"Alisema Nyalandu.[/FONT]

  [FONT=&quot]Aliongeza watanzania ambao na wenyewe wamejifanya kuwa wao ni wenyeji wa wageni hao watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria ili Tanzania isionekane dampo la wafanyabiahsra wanaokwenda kinyume na sheria.[/FONT]

  [FONT=&quot]Alisema kuanzia sasa watendaji wa idara ya biashara watazunguka kwenye masoko yote kwa ajili ya kukagua vibali vya wafanya biashara hao na kuwaorodhesha ili waweze kubainika ni wa ngapi na wamekuja kufanya kazi gani.[/FONT]

  [FONT=&quot]Kwa mujibu wa Nyalandu,baadhi ya watu wanajifanya madalali wa kuwakaribisha wageni hao na kuwaingiza kwenye shughuli hizo kinyume na taratibu, jambo ambalo linasababisha serikali kukosa mapato, kutokana na hali hiyo watu hao watashughulikiwa.[/FONT]

  [FONT=&quot]Alibainisha, soko la kariakoo ni miongoni mwa maeneo yaliyojaa wageni hao, jambo ambalo limesababisha baadhi ya wazalendo kukosa nafasi ya kufanya bishara hizo.[/FONT]

  [FONT=&quot]Alibainisha,serikali kwa sasa inafanya mazungumzo na serikali ya China ili waweze kudhibiti baadhi ya wafanyabishara wasio waadilifu ambao wamekuwa wakiingiza bidhaa feki zinazohjatarisha maisha ya wananchi.[/FONT]

  [FONT=&quot]"Kuna mazungumzo kati yetu na serikali ya China kwa ajili ya kudhibiti bidhaa bandia, lengo ni kuiondoa Tanzania kuwa dampo la bidhaa hizo,kutokana na hali hiyo bidhaa zitakazokuwa zinaingia zitakuwa na ubora unaokubalika,"alibainisha.[/FONT]

  [FONT=&quot]Aliongeza kutokana na hali hiyo wananchi wanapaswa kuwa makini na wafanyabishara wa bidhaa bandia kwa akuangalia ubora wa bidhaa hizo na mahali ilipotoka.[/FONT]


  ............
  Je hatua hii itasaidia kumuinua mmachinga mzawa?
   
 2. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2011
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  kuzungumza kwa kupata popularity kwenye public na kutenda kwa maaana ya kufanyika kwa yale uliyozungumza ni tofauti, tusubiri vitendo kama kweli wataondolea maana nina imani yale yalikuwa kufurahisha baraza
   
 3. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2011
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Tunaomba na waziri wa kazi afanye kazi yake, wamejaa sana wahindi, wakenya, waganda na wengineo humu bila mpango wowote
   
 4. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Nasubiri waondoke nitoe pongezi kwa mwanzo mzuri...........
   
 5. K

  Kifimbocheza JF-Expert Member

  #5
  Jan 11, 2011
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 496
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Isije Ikawa hizo ni Ahadi kama ya Chama Chake


  Ahadi Nyingiiiiiiiii............ Vitendo Zero

  Wachina wanauza hado Karanga,Ice Cream na bidhaa nyingine pale Kkoo tena wanatandika chini kama Chinga wetu

  Unategemea Watz wenzetu wafanye nini

  Fukuza hao na nani kawapa kibali

  Hao waliotoa kibali Waadhibiwe kikamilifu
   
 6. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Wahindi na Wapakistan mbona kawaacha?
   
 7. Revolution

  Revolution JF-Expert Member

  #7
  Jan 11, 2011
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 567
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 60

  Jamani tudiscuss issues tuachane na hizi siasa! Hao wafanyabiashara waliingiaingia je? wakati mwingine msikubali kufanywa wanasesere....hii serikali ya ccm imejaa watu majinga kuanzia kwenye balozi zetu mpaka kwenye taasisi zake....hizi ni siasa tu....
   
 8. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #8
  Jan 11, 2011
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  ndo wawekezaji hoi...!!
   
 9. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #9
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Chip politiki hizi wawafukuze basi na Dowans
   
 10. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #10
  Jan 11, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Wewe mchungaji wewe unamaana mkuu wa kaya unataka afukuzwe? Astaghafillulah!
   
 11. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #11
  Feb 21, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  WaTZ walifarijika sana wakati waziri Lazaru Nyalandu alipotoa tamko lililowapa wamachinga wa kichina na watu wengine wanaofanya biashara na kazi kinyume na taratibu wawe wameondoka nchini kwa kipindi kisichozidi siku 30. Siku 30 zimemalizika na hakuna utekelezaji wowote wa agizo la waziri linaloonekana. Wengi tuliokuwa tumeshamwona Mh. waziri kama Shujaa wa kipindi hiki tunajiuliza kulikoni au baada ya kuonana na balozi wa China amefyata mkia kama kawaida?

  Kama waziri alikuwa amefanyia utafiti tatizo la wachina naamini tamko hili alitoa akiwa na data nyingi za kumwezesha kulitatua na haswa kutekeleza agizo lake lakini kama alikurupuka na kulitoa ili awafurahishe wafanya biashara pale kariakoo atakuwa amechemsha sana. Hii itatufanya tuanze ku question uwezo wake wa kuongoza na misingi ya utekelezaji wa kazi zake za kila siku pamoja na malengo ya muda mrefu ya Wizara yake. Kama tamko lake litaishia hewani sitasita kumwona kama waziri asiye makini sawa tu na wa kizazi kilichopita.

  Nililifikiri Waziri huyu ambaye naamini ana damu changa na mawazo mapya pia ana mechanisms na mikakati ya kisasa na siyo ya kisiasa ya kutatua kero za Wananchi kwa njia itakayoleta matokeo zaidi (RESULT-BASED).

  Watu walimsifu waliposikia akitoa tamko kali na pia wale waliokwisha gongwa na nyoka hawakuacha kushtuka wakijua ni yaleyale na walikuwa wa kwanza kuulizia habari za Nyalandu humu jamvini.

  Zaidi ya 30 baada ya tamko la Nyalandu tulitaka tupewe feedback ya zoezi la kuwaondoa wachina na wazamiaji wengine ila naona mabo bado ni kimya .

  Kwa wanaojua kinachoendelea tujuzeni jamani.

  WaTZ imefika mahali ambapo lazima viongozi wawajibike kutekeleza ahadi na mipango wanayoipanga kimatendo na wawe fair tunapowauliza maendeleo ya utekelezaji wa mipango hiyo. Watanzania hawataki kusikia porojo bali wanataka waone kinachosemwa kikitekelezwa bila kuweka usanii.

  Ninaamini Mkuu Nyalandu ujumbe huu utamfikia na ataweza kutupatia hints za kinachoendelea isifike mahali tukakuona umenyamazishwa na badala ya kuwa HERO tukakuona 21st century COWARD  Ni sisi unayetutumikia
   
 12. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #12
  Feb 21, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,422
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  mhhhhhhh kweli!
   
 13. d

  dotto JF-Expert Member

  #13
  Feb 21, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  What is the meaning of nyalandu!!
   
 14. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #14
  Feb 21, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  thanks mvumbuzi kwa kufuatilia... he went for a cheap popularity
   
 15. Chief Isike

  Chief Isike JF-Expert Member

  #15
  Feb 21, 2011
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Watu wengi hawajui kilichoko au kilichokuwa nyuma ya pazi kuhusu move za huyo naibu waziri aitwaye Lazaro Nyalandu na hasa kwa tamko hilo dhidi ya aliyowaita wamachinga wa Kichina akiwa na mwenzake Meya wa Ilala, Jerry Slaa.

  Mbali ya kuwa Nyalandu ni mtu anayetafuta cheap popularity, aonekane anafanya kazi sana, lakini pia kulikuwa na nguvu ya ziada, ikichagizwa na wafanyabiashara wa Kihindi, ambao inadaiwa kuwa wanakwazika sana na jinsi wachina walivyoteka soko lao.

  Hao Wahindi wasingeweza kupitia kwa Waziri Chami kuwatisha Wachina kwa sababu wanamjua ni man of principle, wanamjua vzr tangu akiwa naibu waziri katika wizara hiyo hiyo, hivyo wakampata kijana huyo Nyalandu wakamwingiza kingi mapema, akawafanyia kile walichotaka akiwa pamoja na Meya wa Ilala, ambaye naye he looks to be of the same calibre, monger for cheap popularity.

  Kwa sababu issue ya wafanyabishara wa Kariakoo, si issue ya kuwatarget Wachina, ukifanya hivyo utasababisha madhara makubwa sana, kiuchumi, kidiplomasia (uhusiano ambao unahusisha mambo yote, siasa, uchumi na jamii), achilia mbali hali ya Xenophobia kama ile iliyojitokeza Afrika Kusini mwaka wa juzi, wa wenyeji kuwavamia na kuwaua wageni, kwa sababu za namna hiyo hiyo.
   
 16. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #16
  Feb 21, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  2MINE... ongezea, na JErry Slaa ni mtu wa kuangalia sana
   
 17. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #17
  Feb 21, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Huyu waziri kijana ni mapepe tu. Anatafuta umaarufu kwa ngazi ya wamachinga.
   
 18. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #18
  Feb 21, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Product ya Mama Mkapa, atakuwaje na mawazo mapya??? Ni fisadi mnyamazifu anayekula nyama kimya kimya.
   
 19. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #19
  Feb 21, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280

  Nataka niamini usemayo bila ubishi kwani nimjuavyo huyu Bwana tamko alilotoa limemzidi si tu umri bali hata uwezo. na nilikuwa makini kuona jinsi huyu bwana ninayemfahamu kuwa hana uwezo wa kukemea atakavyogeuka kutoka COWARD kuwa HERO. NA NILIJUA NI NGUVU YA SODA
   
 20. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #20
  Feb 21, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,947
  Likes Received: 1,507
  Trophy Points: 280
  Huu wimbo tumeuchoka kwani umeimbwa siku nyingi,sijui idara ya Uhamiaji inafanya kazi gani
   
Loading...