Nusura nijiunge CCM

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,222
25,696
Kwakuwa bado nipo kwenye utafiti na kutafuta chama cha kujiunga nacho,mwisho wa juma hili nilitaka kufanya uamuzi. Uamuzi wa kujiunga na CCM. Mimi nataka chama ambacho wanachama na viongozi wake wanaweza kusema ukweli bila ya kuangalia ukweli huo unaelekezwa kwa nani. Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Stephen Masele 'alipomkoromea' Balozi wa Uingereza kwa kuingilia mambo ya ndani ya nchi yetu nilifurahi na kuvutiwa.

Nikajua kuwa Balozi wa Uingereza 'atakiona cha moto' kidiplomasia na kinchi kwakuwa Serikali ya CCM haiwezi kuvumilia mambo yasiyo mazuri kwa mustakabali kwa Taifa. Nikajua kuwa CCM inaundwa na viongozi wathubutu na ambao wanaweza kuuelekeza uthubutu wao kwa yeyote na popote pale alipo. Nikajua ya kuwa kauli ya Masele ilifuatia utafiti wa kutosha na hilo lilikuwa 'onyo' tosha kwa Balozi wa Uingereza.

Kumbe wapi. Ilikuwa ni 'mikwara' yenye lengo la kisiasa tu. Lengo kuu lilikuwa ni kupitisha Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini na mambo mengine yaendelee. Ukweli umejidhihiri pale ambapo Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Yohana Sefue amenukuliwa na vyombo vya habari kuwa kauli ya Masele si ya Serikali na ni ya kwake. Kurukwa kwa Masele kuna maana kubwa kisiasa. Kwamba, usanii hutumika kupata jambo fulani.

Kanusho la Balozi Sefue limenikumbusha sakata la Balozi wa China. Balozi huyu wa China alivaa kofia ya CCM na kuhutubia pamoja na kushiriki ipasavyo mikutano ya CCM kule Kanda ya Ziwa. Balozi huyu wa China,baada ya kukosolewa na wapinzani,alitetewa kila kona ya chama tawala na Serikali hadi sakata hilo lilipopoa. Sasa ninaamini kuwa, kuna Mabalozi wa aina mbili: wanaopendwa kwa matendo yao na 'wanaopondwa' kisanii.

Kabla ya kanusho la leo, nilitumaini kuwa nasi twaweza kuutetea utaifa wetu kama auteteavyo Rais Mugabe wa Zimbabwe. Rais Mugabe anapambana na yeyote kwa lolote.Hajawahi kurudi nyuma katika mapambano yake kwa anachokiamini na kukisimamia. Hata Uingereza inamfahamu vyema Rais Mugabe! Sisi bado sana kwa jambo hilo. Labda tukapate mafunzo toka kwake.

Baada ya kadhia hii ya Balozi wa Uingereza, nimerudi hatua nyingi mno kujiunga na CCM. Imani yangu imeshuka kwa kasi kama joto la jangwani wakati wa usiku. Mimi sipendi sanaa na usanii.
 
Ccm ni taasisi pendwa hapa nchini. Kilichotoka kinywani mwa naibu waziri hakirudi tena
 
Hoja dhaifu sana mbona hukujiunga na CCM pale waliposema hakuna kashfa ya ununuzi wa rada na bunge la uingereza likasema kunaufisadi na chenchi ya rada ikarudishwa usiwe mtu wa matukio, kama una hoja dhaifu kama hii bora usipost kajadili kwenye vijiwe vya kahawa:embarassed2:
 
Hoja dhaifu sana mbona hukujiunga na CCM pale waliposema hakuna kashfa ya ununuzi wa rada na bunge la uingereza likasema kunaufisadi na chenchi ya rada ikarudishwa usiwe mtu wa matukio, kama una hoja dhaifu kama hii bora usipost kajadili kwenye vijiwe vya kahawa:embarassed2:

Hujanielewa.Soma tena Mkuu
 
Ccm ni taasisi pendwa hapa nchini. Kilichotoka kinywani mwa naibu waziri hakirudi tena
Tanzania ni nchi huru! Masele alikuwa yuko sahihi ILA kwakuwa mnaendekeza misaada lazima mtafyata FASTER kama ambavyo SEFUE ameliweka wazi kuwa hamko tayari kukataa mashart ua USHOGA...
 
Back
Top Bottom