Nusura nijiunge CCM

Nusura nijiunge CCM

Hata watoto wa chekechea wanafahamu kuwa wewe ni msukule wa mafisadi,unashinda jf kutetea wezi na wauaji bila hata soni.Ni aibu kubwa kuzaliwa taifa moja na kenge kama nyie!



Sijawahi ona Msukuma mshamba kama wewe
 
Nahisi mwalimu wako na wa Nyaronyo kicheere ni mmoja! Wadandiaji wa thread wengi hawatakuelewa! Big up and keep it up! I have enjoyed your message found between lines!!
Kwakuwa bado nipo kwenye utafiti na kutafuta chama cha kujiunga nacho,mwisho wa juma hili nilitaka kufanya uamuzi. Uamuzi wa kujiunga na CCM. Mimi nataka chama ambacho wanachama na viongozi wake wanaweza kusema ukweli bila ya kuangalia ukweli huo unaelekezwa kwa nani. Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Stephen Masele 'alipomkoromea' Balozi wa Uingereza kwa kuingilia mambo ya ndani ya nchi yetu nilifurahi na kuvutiwa.

Nikajua kuwa Balozi wa Uingereza 'atakiona cha moto' kidiplomasia na kinchi kwakuwa Serikali ya CCM haiwezi kuvumilia mambo yasiyo mazuri kwa mustakabali kwa Taifa. Nikajua kuwa CCM inaundwa na viongozi wathubutu na ambao wanaweza kuuelekeza uthubutu wao kwa yeyote na popote pale alipo. Nikajua ya kuwa kauli ya Masele ilifuatia utafiti wa kutosha na hilo lilikuwa 'onyo' tosha kwa Balozi wa Uingereza.

Kumbe wapi. Ilikuwa ni 'mikwara' yenye lengo la kisiasa tu. Lengo kuu lilikuwa ni kupitisha Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini na mambo mengine yaendelee. Ukweli umejidhihiri pale ambapo Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Yohana Sefue amenukuliwa na vyombo vya habari kuwa kauli ya Masele si ya Serikali na ni ya kwake. Kurukwa kwa Masele kuna maana kubwa kisiasa. Kwamba, usanii hutumika kupata jambo fulani.

Kanusho la Balozi Sefue limenikumbusha sakata la Balozi wa China. Balozi huyu wa China alivaa kofia ya CCM na kuhutubia pamoja na kushiriki ipasavyo mikutano ya CCM kule Kanda ya Ziwa. Balozi huyu wa China,baada ya kukosolewa na wapinzani,alitetewa kila kona ya chama tawala na Serikali hadi sakata hilo lilipopoa. Sasa ninaamini kuwa, kuna Mabalozi wa aina mbili: wanaopendwa kwa matendo yao na 'wanaopondwa' kisanii.

Kabla ya kanusho la leo, nilitumaini kuwa nasi twaweza kuutetea utaifa wetu kama auteteavyo Rais Mugabe wa Zimbabwe. Rais Mugabe anapambana na yeyote kwa lolote.Hajawahi kurudi nyuma katika mapambano yake kwa anachokiamini na kukisimamia. Hata Uingereza inamfahamu vyema Rais Mugabe! Sisi bado sana kwa jambo hilo. Labda tukapate mafunzo toka kwake.

Baada ya kadhia hii ya Balozi wa Uingereza, nimerudi hatua nyingi mno kujiunga na CCM. Imani yangu imeshuka kwa kasi kama joto la jangwani wakati wa usiku. Mimi sipendi sanaa na usanii.
 
Hahahaaaa, tuseme mkuu hujaelewa? Au umelewa supu inayotokana na bendera yenye alama ya jembe na nyundo?
Duuuuh unafiq ni sehemu ya maisha yenu...

we si chadema mkereketwa?? imekuaje leo
 
we ni mbulula sana ulikuwa unawaza kujiunga na ccm!? sijawai na sita kuja kuwaza kujiunga na ccm
 
Wale wa kusoma kichwa cha habari na kukoment naamini hawatakuelewa kamwe.Hili kundi la watu ambao hawatakuelewa mapema inawahusu pia divisheni five wote waliomo humu jf.
 
Nahisi mwalimu wako na wa Nyaronyo kicheere ni mmoja! Wadandiaji wa thread wengi hawatakuelewa! Big up and keep it up! I have enjoyed your message found between lines!!

Nimesoma naye Kitivo cha Sheria-UDSM lakini miaka tofauti ha ha ha ha ha
 
we ni mbulula sana ulikuwa unawaza kujiunga na ccm!? sijawai na sita kuja kuwaza kujiunga na ccm

mbulula mwingine umekuja? nimemwelewa vizuri tu, tatizo kwangu kutamka alikuwa anafikili kujiunga na ccm, mimi hii ni dhambi kubwa
Jitahidi tu kuelewa, kama bado hujaelewa rudia tena na tena! Ukielewa utagundua ya kuwa jamaa hajawahi hata siku moja kujiunga na CCM, ila ni mtu anaye 'iinjoy' CCm! Just read between lines!!!
 
Nimesoma naye Kitivo cha Sheria-UDSM lakini miaka tofauti ha ha ha ha ha

hujui elimu yangu na uliposoma wewe mimi nilipita siku nyingi, najua umeandika kimtindomtindo ishu ni kwamba unaweza kumsifu yesu kimtindondo kwa boko haram, kusema kuwa unafikili kuwa ccm wengine wanasoma vichwa vya habari tu wanaweza kufikili kuwa ccm
 
hujui elimu yangu na uliposoma wewe mimi nilipita siku nyingi, najua umeandika kimtindomtindo ishu ni kwamba unaweza kumsifu yesu kimtindondo kwa boko haram, kusema kuwa unafikili kuwa ccm wengine wanasoma vichwa vya habari tu wanaweza kufikili kuwa ccm


Mkuu Festory umekuaje tena leo? Mimi nilikuwa namjibu Mkuu muuza ubuyu. Naona umeniandama kweli.Yawezekana hukusoma fasihi kabisa katika elimu yako.Uwe unasoma kwa makini kabla ya kuweka maoni yako. Jioni njema!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom