Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 61,204
- 99,943
Topic nzuri sana ILA vichaa wa CCM wanaiharibu, nawachukia sana sana
Topic nzuri sana ILA vichaa wa CCM wanaiharibu, nawachukia sana sana
Hahahaaaaaa.Nimekuelewa vizuri sana.Fasihi sijakutana nayo barabarani.You know me well Comrade. Do you believe my attempt? ha ha ha ha ha ha Cheers brother!
My point kujiunga na chama is not a single event issue leo maselle kasema hivi najiunga kesho fulani kasema hivi najitoa nadhani ni more that that thus why democracy is not flourishing in Africa
Jiunge act
Ndipo nilipo Mkuu
Akajiunge na wamwagia watu tindikali? Walisha watu sumu?
Una miaka mingapi?Kwakuwa bado nipo kwenye utafiti na kutafuta chama cha kujiunga nacho,mwisho wa juma hili nilitaka kufanya uamuzi. Uamuzi wa kujiunga na CCM. Mimi nataka chama ambacho wanachama na viongozi wake wanaweza kusema ukweli bila ya kuangalia ukweli huo unaelekezwa kwa nani. Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Stephen Masele 'alipomkoromea' Balozi wa Uingereza kwa kuingilia mambo ya ndani ya nchi yetu nilifurahi na kuvutiwa.
Nikajua kuwa Balozi wa Uingereza 'atakiona cha moto' kidiplomasia na kinchi kwakuwa Serikali ya CCM haiwezi kuvumilia mambo yasiyo mazuri kwa mustakabali kwa Taifa. Nikajua kuwa CCM inaundwa na viongozi wathubutu na ambao wanaweza kuuelekeza uthubutu wao kwa yeyote na popote pale alipo. Nikajua ya kuwa kauli ya Masele ilifuatia utafiti wa kutosha na hilo lilikuwa 'onyo' tosha kwa Balozi wa Uingereza.
Kumbe wapi. Ilikuwa ni 'mikwara' yenye lengo la kisiasa tu. Lengo kuu lilikuwa ni kupitisha Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini na mambo mengine yaendelee. Ukweli umejidhihiri pale ambapo Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Yohana Sefue amenukuliwa na vyombo vya habari kuwa kauli ya Masele si ya Serikali na ni ya kwake. Kurukwa kwa Masele kuna maana kubwa kisiasa. Kwamba, usanii hutumika kupata jambo fulani.
Kanusho la Balozi Sefue limenikumbusha sakata la Balozi wa China. Balozi huyu wa China alivaa kofia ya CCM na kuhutubia pamoja na kushiriki ipasavyo mikutano ya CCM kule Kanda ya Ziwa. Balozi huyu wa China,baada ya kukosolewa na wapinzani,alitetewa kila kona ya chama tawala na Serikali hadi sakata hilo lilipopoa. Sasa ninaamini kuwa, kuna Mabalozi wa aina mbili: wanaopendwa kwa matendo yao na 'wanaopondwa' kisanii.
Kabla ya kanusho la leo, nilitumaini kuwa nasi twaweza kuutetea utaifa wetu kama auteteavyo Rais Mugabe wa Zimbabwe. Rais Mugabe anapambana na yeyote kwa lolote.Hajawahi kurudi nyuma katika mapambano yake kwa anachokiamini na kukisimamia. Hata Uingereza inamfahamu vyema Rais Mugabe! Sisi bado sana kwa jambo hilo. Labda tukapate mafunzo toka kwake.
Baada ya kadhia hii ya Balozi wa Uingereza, nimerudi hatua nyingi mno kujiunga na CCM. Imani yangu imeshuka kwa kasi kama joto la jangwani wakati wa usiku. Mimi sipendi sanaa na usanii.
hahahhahhahaa nimeiweka pending kwanza, acha tuangalia picha nyingine kwanzaMkuu Elli, avator yetu tena iko wapi?
hahahhahhahaa nimeiweka pending kwanza, acha tuangalia picha nyingine kwanza