Mkuu kbm, nadhani maelezo bado hayajatosha vizuri, ni asilimia 44 (44%) lakini ya watu wa ngapi waliopima?
Unajua inawezekana ni watu 100 tu, waliopima, Je, hiyo inatosha kusema asilimia "kubwa" ya jamii ya kitanzania(zaidi ya milioni 40) kuwa wana watoto/wazazi wasio wao?
..., hii inasikitisha sana kama upimaji huu wa DNA ni sahihi, basi inamaana 50% ya wapenzi au wanandoa wanamahusiano nje ya familia zao, na kwa maana hiyo itakuwa vigumu kwa njia na taratibu zote za kuthibiti VVU na Ukimwi kuweza kufanikiwa, kama watu bado wanajamiana hovyohovyo mpaka wanapatikana watoto nje ya ndoa. Mimi mwenyewe nimesikia habari hii kwenye kipindi cha magezeti yetu. Kweli inatiafedheha kwa wanafamilia, inabidi jamii yetu ibadilike.
mkuu, kufuatana tafiti zinavyofanyika' mara nyingi inachukuliwa namba ndogo ya majaribio (samples) na kuwakilisha idadi ya kitu kizima, ndiyo maana mkemia mkuu katoa % inayowakilisha watu wote waliopimwa, kwahiyo % iliyopimwa inawakilisha % ya watanzania wote.
DNA: mkemia mkuu' kasema kuwa asilimia 44 ya waliopima vinasaba kwa ajili ya kujua uhalali wa watoto kwa baba, wamethibitishiwa kuwa watoto hao sio wao. My take: kwahiyo nusu ya watoto wa kitanzania sio wa wababa wanaoishi nao au wanao walea. Kwa ushauri wangu ninapendekeza watoto wote wakitanzania wapimwe ili wakabidhiwe kwa baba zao. Au mnasemaje wanaJF?
Unajua Riwa wengine wanakurupuka tu bora kasikia kichwa cha habari kwenye gazeti hata asijue habari ya kin inasemaje yeye huyo kwenye kibodi, Mimi ikitokea manaume ananiuliza eti huyo mtoto wanasema sio mwanangu nitamuuliza kwani wewe nani kakwambia yule ba mkwe ni baba yako mbona mimi najua sio baba yako tena siku nyingi tu. Kama unaona nakudandanya nenda kamuulize mama yako ndie anaujua ukweli na mimi niliupata kwake! then hatarudia kama sio ndoa kuleta sokomoko.Mleta mada ANAPOTOSHA tafsiri ya hiyo takwimu...nianze kwa kusema ni kweli imekuwa published kuwa 44% ya watoto ambao wanaenda kufanya kipimo cha vinasaba (DNA) kwenye ofisi ya mkemia mkuu imethibitika sio wao (baba). Lakini hii haina maana kuwa kati ya watoto wote wa kiTanzania karibu nusu sio wa baba wanaoishi nao...hii ni 'mis-interpretation' ya hiyo takwimu.
Hapa Tanzania, kipimo cha DNA kutambua mzazi halisi wa mtoto, hufanyika kwa maombi maalum toka 'Mahakamani' ambapo huwa na kesi ya kutambua mzazi halisi wa mtoto, kwa hiyo tayari umeshasegment sample yako kwa watu ambao kwa sababu moja au nyingine hawaamini kuwa ni baba halisi wa watoto hao...tayari hapo kuna mazingira ya kutoaminiana, na hivyo takwimu hii tayari iko biased na huwezi kuigeneralize kwa population nzima ya watoto wa kiTanzania....kosa ambalo mleta mada umelifanya.
Ili kuweza kugeneralize takwimu ili kurepresent general population, itabidi ufanye sampling kwa kutumia techniques sahihi za sampling kupata kweli sample size inayorepresent general population kuweza kugeneralize results zako. Kwa hiyo iwapo ofisi ya mkemia mkuu, wangechagua population sample ya watoto kwa ukubwa unaoshauriwa na kuwapima vinasaba, then hapo waweza sema asilimia 44% ya watoto wa kiTanzania...in short of that, NO!
DNA: mkemia mkuu' kasema kuwa asilimia 44 ya waliopima vinasaba kwa ajili ya kujua uhalali wa watoto kwa baba, wamethibitishiwa kuwa watoto hao sio wao. My take: kwahiyo nusu ya watoto wa kitanzania sio wa wababa wanaoishi nao au wanao walea. Kwa ushauri wangu ninapendekeza watoto wote wakitanzania wapimwe ili wakabidhiwe kwa baba zao. Au mnasemaje wanaJF?
Hata hivyo mimi siku zote naamini kwamba mtoto ni wa mama maana yeye hawezi kusingiziwa. Lakini ninyi akina baba tusaidieni tu kwa roho safi kulea kwa kuwa kitanda hakizai haramu.DNA: mkemia mkuu' kasema kuwa asilimia 44 ya waliopima vinasaba kwa ajili ya kujua uhalali wa watoto kwa baba, wamethibitishiwa kuwa watoto hao sio wao. My take: kwahiyo nusu ya watoto wa kitanzania sio wa wababa wanaoishi nao au wanao walea. Kwa ushauri wangu ninapendekeza watoto wote wakitanzania wapimwe ili wakabidhiwe kwa baba zao. Au mnasemaje wanaJF?
Ndiyo maana mimi sijoa nasubiri nimpate mwanamke mwaminifu kama wewe ambaye atanifanya baba mzazi wa watoto wangu na siyo baba mlezi.Hata hivyo mimi siku zote naamini kwamba mtoto ni wa mama maana yeye hawezi kusingiziwa. Lakini ninyi akina baba tusaidieni tu kwa roho safi kulea kwa kuwa kitanda hakizai haramu.
Kuolewa napenda, lakini kama hiyo ndiyo picha yako kwenye avatar, mmmh siwezi. Labda dada Ciello anaweza kukubeba, mimi hapana kabisaaa.Ndiyo maana mimi sijoa nasubiri nimpate mwanamke mwaminifu kama wewe ambaye atanifanya baba mzazi wa watoto wangu na siyo baba mlezi.