Remark
JF-Expert Member
- Aug 15, 2015
- 447
- 856
Hawa jamaa wanadharau sana.
"Huenda zaidi ya nusu ya ardhi katika Kaunti ya Mandera nchini Kenya kudhibitiwa na kundi la Al-Shabaab la Somalia
Habari zinasema, kundi Al-Shabaab la Somalia limefanya mashambulizi mfululizo katika Kaunti ya Mandera, nchini Kenya na kusababisha vifo vya watu na uharibifu mkubwa. Athari za Al-Shabaab zimeenea katika Kaunti ya Mandera na maeneo ya karibu ya Banisa, Lamu, na Takaba, hivyo kuleta wasiwasi mkubwa na pia kusababisha maswali kuhusu maandalizi ya kupambana na ugaidi.
Awali, kiongozi wa Kaunti ya Mandera, Ali Roba alionya kuwa wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab walidhibiti zaidi ya nusu ya kaunti hiyo na barabara nyingi.
Naye mratibu wa Kanda ya Kaskazini mashariki mwa Kenya Nicodemus Ndalana pia alikiri kwamba wapiganaji hao wameingia katika kaunti hiyo, na wameweka kambi ndani na karibu na Kaunti ya Mandela, na pia wanafanya biashara ya dawa za kulevya, hivyo kusababisha hali ya usalama kuwa mbaya zaidi."
Habari zinasema, katika miezi mitatu iliyopita, wapiganaji wa Al-Shabaab wamethibiti msikiti wa eneo hilo, kukusanya ushuru kutoka kwa wauzaji wa ndani, na kuharibu vifaa vingi vya mawasiliano.
Serikali ya Kenya imepanga kukutana na wakaazi wa eneo hilo ili kupanga mkakati wa kupambana na kundi la Shabaab.