Nusu + Nusu = 1 Siri ya mafanikio katika mahusiano

Nusu + Nusu = 1 Siri ya mafanikio katika mahusiano

Himidini

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2013
Posts
5,534
Reaction score
4,190
Couple_kiss.sized.jpg
^^
Mahusiano yenye manufaa ndio ndoto ya kila mwanadamu. Hakuna anaependa uhusiano wenye ugomvi, chuki, mivutano n.k ingawa kwa upande wa pili mambo hayo hayana budi kutokea kwani tunaishi na marafiki, wapenzi wenye hulka na silika zilizo tofauti na zetu.
Lakini kwa nini Mahusiano mengi yameleta maumivu, uchungu na huzuni kuliko faraja, tumaini na nguvu mpya?
Bila shaka kuna sababu nyingi na moja kata ya hizo ni hii YA NUSU KUONGEZA NUSU UNAPATA MOJA. nitafafanua
.....

WAKATI WA KUJIDOGOISHA
Ni wazi kuwa wengi wetu hatupendi kujishusha na kuruhusu mapenzi yetu kwa wale tuwapendao yadumu. Tunaweka kinga nzito sana kwa vile tumesoma kuliko wapenzi wetu, tunatumia pesa kuwafuja wenzetu kama nguo mbovu, hatuambiliki kwa sababu madaraka ya ofisini hayaishii mlangoni bali mpaka chumbani. Ni jambo jema kijivunia mafanikio uliyoyapata pengine kwa taabu ya muda mrefu lakini linapokuja suala la mapenzi hapo hakuna mkubwa.. tujishushe na kuyatazama mambo katika uhalisia wake yaani kila mmoja anakuwa nusu ili muwe kitu kimoja
....

UPENDO NI SADAKA
Sadaka ni chochote unachotoa kwa hiari. Unatoa kwa sababu hiuna kingine zaidi cha kutoa bali hicho tu.
Ili mapenzi yalete maana Mwanaume na Mwanamke inabidi wajitoe sadaka. Kutoa upendo kwa hiari kwani ndicho walichobakiza kwenye hifadhi ya baraka zao. Mfano u mfanayakazi toa nusu ya pato lako nami nitoe langu tujenge maisha, unashida na pesa nakusaidia nawe nisaidie japo hii inaweza kuwa kinyume na sadaka lakini bado inaondoa upendo wa upande mmoja.
Jishushe nawe nione kijali kwako
....

UTIMAMU HULETA UKAMILIFU
Moja ya kushindwa kwa mahusiano mengi ni kuingia katika mahusiano ukiwa na utegemezi wa fikra, Mapenzi yanahitaji ukomavu wa akili ili ujue unaeungana nae anajua thamani ya mwili wako, moyo wako, vipaji vyako, au anajiona kuwa kwa kuwa anapendwa na wengi au ni mrembo sana atafanya apendavyo!! Unahitaji kuwa na mtu anaetambua kuwa pamoja na upendeleo wa kimaisha aliojaliwa yupo tayari kujishusha na kukubali kuongozana na wewe katika maisha.
....
KILA MMOJA NI WA THAMANI
Umewahi kuona mke na mume wakipigana mbele za watoto? Au mbele za majirani? Hapo kila mmoja anajaribu kuonyesha umuhimu wa thamani yake kwa mwenzake. Au katika uchumba unakuta mmoja anajitapa kuwa fulani nimemuweka kwenye kiganja au hawezi kuniacha? Huko ni kutotambua kuwa kila mmoja ana thamani na kuwa pamoja kuwa umependwa haina maana kuwa uache kujishusha, unahitaji kutoa sehemu fulani ya u-wewe ili muwe mwili mmoja na mwenzio
....
Sina maana kuwa ujinyime thamani, uumie katika mapenzi, ukae kimya tu hata unapokanyagwa HAPANA
Maana yangu ni kuwa uwe tayari kuleta mjadala na mwenzio juu ya tofauti zenu. Mfano unahisi unasalitiwa au unanyonywa pato lako au wewe tu ndio unajitoa kuliko mwenzio basi tafuta mahali palipotulia msemezane na mwenzako ili akubali kuwa nusu MUUNGANE MUWE KITU KIMOJA
^^
 
hapo kwenye kujidogoisha inakuwaje kwa wapenz ambao wote hawajasoma, hawanakitu, yaani wako sawa ktk kila kitu ispokuwa jinsia zao tu?
 
hapo kwenye kujidogoisha inakuwaje kwa wapenz ambao wote hawajasoma, hawanakitu, yaani wako sawa ktk kila kitu ispokuwa jinsia zao tu?

^^
Haiwezekani..mkalingana kwa kila kitu hata Mapacha (identical twins) hutofautiana.
Utakachobaini katika uhusiano wa aina hiyo ni kuwa kuna mmoja atatafuta ukubwa tu.
Mwanafalsafa mmoja amewahi kusema 'we are born selfish' hivyo hiyo hali itazaa tofauti.
^^
 
Ya kweli hayo kwani kwa ndoa kudumu ni lazima mume na mke wafanye kazi kuidumisha kama team na sio mmoja mmoja,well noted mkuu.
 
nimeelewa nitalifanyia kazi siku za usoni ikiwa Bwana atanipa kibali..

thanks best
 
^^
Haiwezekani..mkalingana kwa kila kitu hata Mapacha (identical twins) hutofautiana.
Utakachobaini katika uhusiano wa aina hiyo ni kuwa kuna mmoja atatafuta ukubwa tu.
Mwanafalsafa mmoja amewahi kusema 'we are born selfish' hivyo hiyo hali itazaa tofauti
.
^^

kwenye red ndipo nlipokuwa napatafuta. asante
 
Ahsante Himidini kwa uzi wenye mafundisho mengi..Ni matumaini yangu utakuwa ni wa manufaa kwa wengi..:smile-big:
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom