Nunua "Majeruhi wa Mapenzi" Support JF!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nunua "Majeruhi wa Mapenzi" Support JF!!!!

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Mzee Mwanakijiji, Jul 5, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jul 5, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  [h=6]Mpendwa msomaji,

  Kitabu cha "MAJERUHI WA MAPENZI" tayari kimeshachapwa - japo kimechelewa kuliko tulivyotarajia - na sasa tunaanza kuprocess orders za watu mbalimbali. Ikumbukwe kuwa lengo letu katika toleo hili la kwanza ni kuweza kukifikisha kitabu hiki mikononi mwa wasomaji bila kulazimika kutumia maduka ya vitabu kwanza (na hivyo kupunguza gharama kwetu). Njia ambayo tutatumia zaidi ni kufanya pre-order ambapo mtu anaagiza na kulipia huku akitupatia:

  a. Uthibitisho wa malipo hayo - namba ya risiti kutoka M-Pesa
  b. Kutuambia alipo Mji na Mkoa (ili kuweza kujua watu wangapi wanaagiza kutoka wapi)

  Nasi tutakapoanza kusambaza kitabu tutatumia njia za "couriers" hasa wale ambao tayari tunashirikiana nao katika magazeti. Lakini kwa maeneo maalum kama Dar, Mwanza, Mbeya na Arusha tutakuwa na "contacts" wetu huko ambao tutawafikishia kitabu chako nao watawasiliana nawe ili kuweza kupanga jinsi ya kukupatia. Kwa mfano Dar kwa vile inaonekana wengi wanaagiza kutoka mpango wa awali ni kuwa na "points of distribution" ambapo wale walioagiza na kulipia na wale ambao wanataka kununua kwa fedha taslimu wataenda kupata vitabu vyao.

  Kwa sasa hivi ni njia ya M-Pesa na fedha taslimu tu tunayoweza kutumia: Ukitaka kuagiza kwa kutumia M-Pesa fanya ifuatavyo:

  Jinsi ya Kutuma kwa kutumia simu yako ya Voda

  1. *150#

  2. Bonyeza 4 (Pay Bill)

  3. Bonyeza 1 (Enter Business Number)

  4. Weka 888888

  5. Enter Reference No. (Hapa andika "MAJERUHI" )

  6. Enter Amount (Weka kiasi unachotaka kutuma): Kabla ya Julai 7, 2012 utaweza kununua kwa 15,300/- ambayo ni punguzo ya 15%; Kama unataka kuchangia 1000 kwenda JF nunua kwa full price ya 18,000/

  7. Weka password yako na kisha utume.

  Ukishafanya hivi tuma risiti number kwenda "rockcitym@gmail.com" na kiasi ulichotuma.[/h]
   
 2. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #2
  Jul 6, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Kama nataka 1,000/= iende JF basi bei ingebidi iwe 15,300 + 1,000 = 16,300/=, na sio 18,000/=. Vinginevyo ni kama unakuwa punished kwa kuchangia 1,000/= kwenda JF, manake unalipa 2,700/= zaidi!...hahahahhahaa

  Halafu mchakato wenyewe wa kununua kitabu ni complicated utadhani unanunua manual ya ku enrich Uranium! Mwanakijiji umekaa nje muda mreeefu lakini bado haijakusaidia, mteja hatakiwi kupata ki stress cha kichwa wakati ananunua, we ushapokea hela ya mtu halafu unataka akutumie risiti ndio utoe mali ya mteja, kwani hela yako hujapata??? Wewe ndio unatakiwa utoe risiti ukipata hela yangu, sio mimi mteja nikupe wewe risiti!!!! Mambo ya biashara za Kiswahili hizi...aaaah!!!
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Jul 6, 2012
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  angalia mdau, wadanganyika watakwambia una kijicho..
   
Loading...