Nunda (22) Mungu amepotea.

Nunda (22) Mungu amepotea.

Mwiba

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
7,607
Reaction score
1,760
Baada ya tabia ya Nunda kuvuma mtaani kuwa ni mtoto asiesikia na mtundu na mjuaji kupita maelezo ,wazee wanunda walikaa na kutafakari tabia ya mtoto wao ,mama mtu akasikia kuwa yupo Padre ambae ni maarufu kwa kurekebisha tabia za watoto ,baba mtu akasema basi tufanye tumpeleke huko kabla sijaanza kumtandika mikwaju ,Si mbali na wanapoishi ,Nunda akapelekwa na kukabidhiwa Padre.

Padre : Nunda unajua Mungu yupo wapi ?
Nunda kimya ,
Padre kwa sauti ya mkazo kidogo : Nunda hivi unajua Mungu yupo wapiii ???
Nunda kimya na karudi nyuma na kujikunja kama aneogopa.
Padre akapandisha hasira kwa ukali huku akimnyoonyea kidole ,:Nakuuliza wewe sisemi na kivuli niambiae Mungu yupo wapi we mtoto ,hivi wewe Bubu ?

Nunda kuona hivyo alitafuta upenyo na kukimbia mbio hadi nyumbani kwao na kujifungia chumbani kwake ,mama yake alimuona Nunda akiingia kwa kishindo na spidi si ya kawaida kama anefukuzwa ,mama akaenda kwenye chumba cha Nunda na kumuuliza mbona amebadilika na kurudi kwa woga kumetokea nini huko ?

Nunda : Mama unajua nipo kwenye matatizo makubwa sana sana ,Mungu amepoteah !!! na yule Padre anafikiri mimi ndie nimemficha:shock:
 
hahahaaaaa,,,, umenifanya nicheke kwa sauti kwny msiba!
 
Back
Top Bottom