NUKUU ZA HASHIM RUNGWE

Massivve

JF-Expert Member
Jun 4, 2015
274
368
Hizi ni nukuu alizotoa Hashim Rungwe leo katika mahojiano na kituo cha EATV kwenye kipindi cha kikaangoni live:

1. "Waziri wa sheria na katiba asilazimizishe mawazo yake yawe sheria. Tunatofautiana kufikri, na TLS inaongozwa kwa misingi ya sheria na kanuni ilizojiwekea kwa hiyo aache wajumbe waamue. Yeye ana kura moja tu asiwalazimishe watu kumchagua kiongozi anayemtaka yeye"

2. "Huwezi ukaambiwa uoneshe vyeti halaafu unalia ovyo kwa wachungaji.., mwanaume halii hovyo. Kwani umeambiwa kazi ni ukuu wa mkoa tu???"

3. "Namshauri RC ambaye ni kama mwanangu, atoke azungumze ili kumaliza huu utata wa vyeti, asimsumbue Rais ana mambo mengi"

4. "Mimi kama Rais Magufuli akiniteua, nitamshukuru, halafu nitamuomba radhi na kumtaka atafute mtu mwingine"

5. "Prof. Lipumba anapaswa kuonesha uwezo wake nje ya CUF. Aoneshe nje ya CUF anaweza nini? siyo ang'ang'anie hapo"

6. "Waliofukuzwa CCM, tunawakaribisha CHAUMMA, waje kwa hiari yao, siwezi kwenda kuwabembeleza"

7. "Kura zangu ziliibiwa haiwezekani nipate kura 2000, halafu naletewa kura 200, hiyo sifuri moja imemezwa?"

8. "Ningekuwa Rais jambo la kwanza ningehakikisha wananchi wote wanapata chakula, wanashiba kwanza mengine baadaye. Watanzania wananjaa"

Umeipenda ipi?
 
Back
Top Bottom