Hashim Rungwe: Ningekuwa Rais ningehakikisha wananchi wote wanapata chakula wanashiba

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
Mwenyekiti wa chama CHAUMMA Mhe Hashim Rungwe yupo Kikangooni live anaongelea mambo mbalimbali.
"Kura zangu ziliibiwa haiwezekani nipate kura 2000, halafu naletewa kura 200, hiyo sifuri moja imemezwa?" -
Ningekuwa Rais jambo la kwanza ningehakikisha wananchi wote wanapata chakula, wanashiba kwanza mengine baadaye.

Ningefanya bei ya unga iwe shilingi 250, watoto shule wapate chakula, wapate uji, hawawezi kusoma na njaa.

"Chama Cha Mapinduzi hakina utamaduni wa kuwaheshimu watu wengine wenye uwezo ambao wanatoka vyama vingine.
"Namshauri RC ambaye ni kama mwanangu, atoke azungumze ili kumaliza huu utata wa vyeti, asimsumbue Rais ana mambo mengi"-
"Mimi kama Rais Magufuli akiniteua, nitamshukuru, halafu nitamuomba radhi na kumtaka atafute mtu mwingine" -
"Mgogoro wa CUF kwangu ni msiba maana tunarudishwa nyuma kwa ajili ya maslahi ya mtu mmoja" -
"Prof. Lipumba anapaswa kuonesha uwezo wake nje ya CUF, aoneshe nje ya CUF anaweza nini? siyo ang'ang'anie hapo" -
"Waliofukuzwa CCM, tunawakaribisha CHAUMMA, waje kwa hiari yao, siwezi kwenda kuwabembeleza" -
"Waziri hapaswi kuingilia mambo yetu ya TLS, kama ana maoni yake tunayaheshimu lakini asiyaingize kwetu" -
"CHAUMMA na UKAWA ni ndugu moja, wote tuna lengo moja, wakiamua kunipitisha mimi kugombea urais 2020 ni sawa tu" -

tmp_12144-IMG_20170315_151255266770277.jpg
 
Ninaamini pia usingeweza kuvumilia ma-RC waliofeli kuanzi darasa la nne hatimae kufoji vyeti.
pia vile vile asingethubutu kudhulumu hela za wahanga wa tetemeko na kwenda kuzijengea uwanja wa Ndege kijijini kwao badala yake angetoa nusu ya networth yake na kuigawa kwa kila muathirika.

Ila Huyu jamaa anaonekana yuko after humanity bhana anafaa sana sijui kwani hamkumchagua yeye nyie wabongo mkatuchagulia mtu wa ajabu ajabu.
 
Mkuu hata yule wengi hawakumchagua, lakini Tanzania bwana wanalotaka ndiyo linakua.
 
pia vile vile asingethubutu kudhulumu hela za wahanga wa tetemeko na kwenda kuzijengea uwanja wa Ndege kijijini kwao badala yake angetoa nusu ya networth yake na kuigawa kwa kila muathirika.

Ila Huyu jamaa anaonekana yuko after humanity bhana anafaa sana sijui kwani hamkumchagua yeye nyie wabongo mkatuchagulia mtu wa ajabu ajabu.
Asinge wakejeli wahaya kuwa, ukimwi nyie, tetemeko nyie, najua kwenu kuna katerero na mto ngono, "mwafwaaaa!
 
pia vile vile asingethubutu kudhulumu hela za wahanga wa tetemeko na kwenda kuzijengea uwanja wa Ndege kijijini kwao badala yake angetoa nusu ya networth yake na kuigawa kwa kila muathirika.

Ila Huyu jamaa anaonekana yuko after humanity bhana anafaa sana sijui kwani hamkumchagua yeye nyie wabongo mkatuchagulia mtu wa ajabu ajabu.
Pia asingeweza kusema wabunge wa chama chake ambao walienda kumtembelea Mbunge wa upinzani ni wasaliti wa chama
 
Mwenyekiti wa chama CHAUMMA Mhe Hashim Rungwe yupo Kikangooni live anaongelea mambo mbalimbali.

Ningekuwa Rais jambo la kwanza ningehakikisha wananchi wote wanapata chakula, wanashiba kwanza mengine baadaye.

Ningefanya bei ya unga iwe shilingi 250, watoto shule wapate chakula, wapate uji, hawawezi kusoma na njaa.

"Chama Cha Mapinduzi hakina utamaduni wa kuwaheshimu watu wengine wenye uwezo ambao wanatoka vyama vingine.

Kwahiyo angekutumia kanuni ipi kukokotoa mpaka unga uwe Ts 250...?? au anadhani ni rahisi namna hiyo kama anavyosema.
Nchi haiendeshwi kwa hisia na mihemuko bali kwa mikakati na mipango madhubuti ya kiserikali.

Kwani kwa mawazo haya atasema na sukari angefanya kg 1 iwe Tsh 100 tu na mkate ingekuwa tsh 20 ili tu watu wanywe chai na siagi.
 
pia vile vile asingethubutu kudhulumu hela za wahanga wa tetemeko na kwenda kuzijengea uwanja wa Ndege kijijini kwao badala yake angetoa nusu ya networth yake na kuigawa kwa kila muathirika.

Ila Huyu jamaa anaonekana yuko after humanity bhana anafaa sana sijui kwani hamkumchagua yeye nyie wabongo mkatuchagulia mtu wa ajabu ajabu.
Kati ya watu/wanasiasa ninaowaelewa na kuwakubali sana Mzee Hashim Rungwe ni mmojawapo. Akili, busara, utu, hekima, heshma na ujasiliamali hapa vimetamalaki.

Hii nchi ina bahati mbaya sana.
 
Mwenyekiti wa chama CHAUMMA Mhe Hashim Rungwe yupo Kikangooni live anaongelea mambo mbalimbali.

Ningekuwa Rais jambo la kwanza ningehakikisha wananchi wote wanapata chakula, wanashiba kwanza mengine baadaye.

Ningefanya bei ya unga iwe shilingi 250, watoto shule wapate chakula, wapate uji, hawawezi kusoma na njaa.

"Chama Cha Mapinduzi hakina utamaduni wa kuwaheshimu watu wengine wenye uwezo ambao wanatoka vyama vingine.

Lakini yeye siyo Raisi wa JMTZ!
 
Huyu mzee wengi huwa wanamuona kama ni type yakina Mrema ila kiukweli sio.

Jamaa huwa anaongea vitu vidogo lakini huwa vinabeba maana kubwa sana.

"Tutatue kwanza tatizo la njaa" Ukiwaza kwa mapana hii Sentensi utaiona kama ndogo lakini imebeba ujumbe mkubwa sana.

Njaa ndio inayowafanya watu washangilie kila kitu hata kama hakina maana.

Njaa ndio inaofanya watu kupiga makofi kila kitu kinachozungumzwa.
 
Back
Top Bottom