HASHIM RUNGWE: NCCR-Mageuzi inahitaji mabadiliko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

HASHIM RUNGWE: NCCR-Mageuzi inahitaji mabadiliko

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Wateule, Nov 6, 2011.

 1. W

  Wateule Senior Member

  #1
  Nov 6, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 181
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 60

  [​IMG]

  Ndg. Hashim Rungwe  Na Alfred Lucas – Imechapwa 19 October 2011


  HASHIM Spunda Rungwe hajachuja kwa tambo. Anatamba bado angali na maarifa ya uongozi adilifu.

  Akiwa ni mwana NCCR-Mageuzi aliyebeba bendera ya chama hicho kugombea wadhifa wa urais wa Tanzania uchaguzi mkuu uliopita wa Oktoba 2010, anasema anafikiria kugombea uongozi wa juu katika chama.
  Haamini kama kuna mgogoro ndani ya NCCR-Mageuzi, lakini anasema wazi chama kinakabiliwa na watu wenye mawazo mgando; hawataki kusikia mawazo mapya.

  "Watu wameona kwamba mkuu wao ni dhaifu. Uenyekiti sio kama baba kwenye familia kwamba maisha atabaki kuwa baba. Katika siasa mambo hayako hivyo. Hapa cheo ni dhamana. Unakabidhiwa na ukishatumika unapaswa kuachia wenzako," anasema.
  Katika mahojiano maalum na MwanaHALISI yaliyofanyika wiki iliyopita jijini Dar es Salaam, Rungwe anasema utamaduni wa baadhi ya viongozi kuzigeuza nafasi za uongozi wa kisiasa kama ni ajira zao milele, hauna nafasi tena katika zama hizi.
  Ingawa hataki kueleza kwa ufasaha hisia zake, Rungwe anazianika hamasa za mabadiliko anaposema, "Ndani ya chama kuna tofauti ya mawazo… mimi sioni kuna mgogoro."

  Rungwe, mwenye umri wa miaka 62, anasema mawazo ya mabadiliko ni jambo jema linalolenga kujenga chama chao na taifa kwa jumla.
  Anasema chama hakina mgogoro kama wengine wanavyoeleza, isipokuwa anasikitika kuona wapo wasioelewa vizuri mantiki ya mawazo ya mabadiliko.
  "Katika siasa mawazo ya kubadilisha viongozi si mgogoro. Ni changamoto inayopaswa kufanyiwa kazi kwa utulivu na kisayansi. Tatizo wapo viongozi wasioelewa mantiki yake," anasema.

  Rungwe anaamini harakati za chama haziendi vizuri ndio maana angependa kuona utamaduni wa watu kubadilishana madaraka katika chama ambao ndio hupata viongozi walio tayari kuwajibika.
  "Hatuwezi kubaki na watu wanaofanya kazi kwa mazoea… uongozi kama huu wa mazoea tunaona unavyoimaliza CCM. Sisi hatutaki kufika huko na huu ndio wakati wa kurekebisha kasoro hizi," anasema.

  "Watu wako pale wameganda tu. Hawasemi chama hakionekani kama kipo, na wakiambiwa kuhusu mabadiliko wanatetemeka. Akili zao zinawatuma kuona wadhifa wa chama ni ajira. Lazima ifike hatua watu wakubali mawazo mapya," anasema.
  Rungwe anasema kuna wakati mnapochagua au kuteua mtu wa kuongoza eneo fulani, mfano awe mkuu wa mkoa, lazima awe mtawala. Lakini, akaongeza, utaona watu wanateuliwa au kuchukuliwa tu na mtu kuwa mkuu wa mkoa au wa wilaya.
  "Unamteua mtu kama huyo analeta nini," anauliza. Wizara inayohitaji wataalamu fulani kama ujenzi unamteua mfano mtu kama mwalimu, atawezaje kukagua barabara?"

  Anasema masuala ya siasa sasa yanatakiwa kuendana na weledi ili chama kikabili changamoto zilizopo katika kuwaletea maendeleo wananchi.
  Rungwe anasema amejifunza kwamba katika sekta nyingi za maendeleo nchini Tanzania, kuna ukosefu wa viongozi wanaoweza kuziongoza kwa ufanisi na akaonya vyama vya siasa vinavyoshindwa kusimamia mahitaji ya watu, vitapotea.
  Anasema Watanzania hawastahili tena kuachia nchi yao ikibaki nyuma kimaendeleo wakati inaadhimisha miaka 50 ya uhuru kutoka kwa wakoloni.
  "Hapa ndipo vyama vyetu vinapotakiwa kuingia na kusimamia sera zinazovutia uchumi wa nchi kukua sambamba na uchumi wa familia mojamoja," anasema.

  Rungwe anatoa mfano wa tatizo la mgao wa umeme unaosababishwa na mipango mibovu ya viongozi waliokabidhiwa dhamana ya kuongoza taasisi zinazosimamia sekta ya nishati.
  Anasema katika hali kama hiyo haikubaliki chama kama NCCR-Mageuzi kikabaki kimya kama vile hakuna matatizo yanayokabili nchi.
  "Kuna mgawo wa umeme na kuna tatizo kubwa la bei za vyakula na bidhaa nyingine kupanda kwa kasi, na kuna hujuma za utoroshaji sukari nchini. Halafu mtu anakaa kimya hatoi tamko lolote. Zaidi utasikia anasifia CCM. Ni matamko ya kuibeba CCM tu, sasa huo upinzani uko wapi?
  "Wenzetu wanajitangaza na kuzungumzia shida za wananchi… sisi tupotupo tu. Mimi nasema lazima tukubaliane suala hili la kukaribisha watu wenye mawazo mapya washiriki kujenga chama ili wananchi wajenge imani nacho na kukiunga mkono," anasema.
  Kwa hapo, Rungwe anajitoa akisema ana nia ya kuingia katika kinyang'anyiro cha uongozi wakati utakapofika.
  "Nitagombea nafasi ya juu chama kitakapotangaza uchaguzi. Lazima nichukue fomu."

  Baadhi ya watu wanadai kwamba malumbano ya sasa baina ya viongozi NCCR-Mageuzi, yanahusiana na fedha za ruzuku. Rungwe anakataa.
  "Hapana bwana mdogo… tuna tatizo la uongozi dhaifu ndio maana nasema wanachama wanaibuka na kuhoji, wala hawana ubaya kwa chama, wanakipenda."

  Rungwe ambaye kitaaluma ni mwanasheria akitumikia uwakili kwa zaidi ya miaka 30 Mahakama Kuu, anasema hajafuta nia yake ya kugombea tena urais wa Tanzania katika uchaguzi ujao mwaka 2015.
  "Nikiwa na afya njema na kama chama kitanipitisha, nitagombea tena ili nionyeshe uongozi au namna ya kusimamia kitu. Mimi nina maarifa, nina mipango na hakuna kikwazo kwangu kuingia ikulu isipokuwa fedha tu," anasema.

  Anasema kuna vyama vya siasa vyenye mawazo mazuri kwa ajili ya ujenzi wa uchumi wa nchi, lakini havina nafasi kwa sababu havina fedha za ruzuku.
  "Kati ya vyama 18 vilivyopo nchini, vipo vinavyofanya kazi kama kibaraka wa chama tawala, nadhani sheria ingebadilishwa kuvisadia vyama imara. Sisi NCCR hatuna fedha lakini tuna sera nzuri.

  "Mimi nasema nikiingia ikulu, kazi yangu ya kwanza ni kuifuta sheria kandamizi ya vyama vya siasa. Sheria hii ya kutoa ruzuku kwa vyama tawala na kuvipa nguvu ya maamuzi inadhoofisha mawazo ya vyama vingine ambavyo vina ilani nzuri, mawazo mazuri lakini ambavyo havisikiki kwa sababu havina fedha."

  Rungwe aliibuka wa tano kati ya wagombea saba wa kiti cha rais akipata kura 20,638 sawa na asilimia 0.31 ya kura zote halali za wagombea.
  Alipitwa na Rais Jakaya Kikwete wa CCM (kura 5,276,827 (asilimia 61.17); Dk. Willibrod Slaa wa CHADEMA (kura 2,271,941 (asilimia 26.34); Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF (kura 431,314 (asilimia 5.2); na Peter Mziray wa APPT Maendeleo (kura 96,933 (asilimia 1.12).
  Katika ilani yake, alihakikishia wananchi kwamba msisitizo wake utakuwa Mtanzania Kwanza katika harakati za kumiliki njia kuu na ndogo za uchumi wa taifa.

  Huu ndio sisi wanamageuzi tunaouita UWEZESHAJI, yaani, popote litakapozungumzwa suala la uwekezaji, kanuni yetu itakuwa; MTANZANIA KWANZA. Katika hili tutawahimiza watanzania kutafuta kwa bidii fursa zozote za kiuchumi hapa nchini na kushiriki kuzimiliki, alisema katika hotuba aliyoitoa mara baada ya chama chake kumteua.

  Source: MwanaHalisi
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Nov 6, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 32,250
  Likes Received: 15,065
  Trophy Points: 280
  Muondoeni kwanza mwenyekiti shoga aliyewekwa na Chama cha Mashoga CCM
   
 3. i

  ibange JF-Expert Member

  #3
  Nov 6, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mbatia hafai tena kuwa Mkiti lakini pia Rungwe hana uwezo
   
 4. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #4
  Nov 7, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,082
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Moto unaanza huku, mzimu wa kufukuzana hautawaacha nyie harafu eti mnataka mpewe nchi ili mtumie masaburi kufikiri.
   
 5. JOASH MUSSA

  JOASH MUSSA JF-Expert Member

  #5
  Nov 8, 2011
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 492
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mbatia chama kimemshinda na anatakiwa apishe kwa amani, sio vibaya ila NCCR wakijipanga vizuri watafanya vizuri uchaguzi ujao ila wawe makini
   
 6. o

  oldonyo JF-Expert Member

  #6
  Nov 8, 2011
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 554
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ivi nini tofauti kati ya Nccr ya Mrema na Nccr ya mbatia?
   
Loading...