Nukuu 10 za Jenerali Mabeyo

Kwanini alishangaa CDF kushindwa kuwaamuru madaktari ili aondolewe Hosptal?

Yeye kama AMIRI JESHI kwanini hakutoa amri hiyo?

Je,ni kwanini alikuwa na uwezo wa kufanya maandalizi ya kifo? Au kuna kitu alikiona kisicho kuwa sawa alitamani kukiepuka lakini protocol za kitabibu zilimzuia?

Vyovyote itakavyokuwa Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
 
Jenerali Mabeyo anaielewa, anaifahamu, aliapa kuitunza, na ameitunza vilivyo Katiba ya JMT. Kwa hili Jenerali Mabeyo apewe maua yake!
Lakini tumesikiliza upande mmoja tu. Tungesikiliza na wengine waliotuhumiwa kwenye hili (si wapo?) tungepata picha kamili
 
Walijua ni mwanamke na upokeaji wake wa taarifa za msiba ungeweza usiwe na uvumilivu kama kwa wanaume!!

Kumuita na kumwambia leo mzee kaandaa sherehe ikulu! Halafu ndiyo anapewa ujumbe
Wakati alikuwa tanga? Au alirudi magogoni kwanza?
 
Katk yote sijaona naFas ya Jaji mkuu ambae ndio mratb wa maswala ya kiitifak na kikatba akipew nafas
 
Order zinafuata channels. Na kwa walio kuwepo mtu wa kwanza kupokea amri ni huyo venance. Ila kwakuwa magu alikuwa kitandani na hajiwezi hakuwa na namna hata kama angegomewa na DAS kuna wakati ukifika cheo mamlaka utajiri heshima nguvu vyote vinakuwa havina msaada kwako. Hata mwanao akitaka kukuzaba makofi anaweza na huwezi mfanya lolote
 
Bora angewasikiliza hI wenye maono nchi isingekuwa mikononi mwa mafisadi kama ilivyo sasa
 
Hii comment na mada,wapi na wapi! Kwa hiyo,wanaowahi kutoweka,wana dhambi? Kwamba we unaeandika, ni msafi huna dhambi! Haya,anaeongelewa hapa, unamaanisha dhambi zilifika wingi wake ndo zikamtoa uhai??
Imani nyingine ni ajabu sana.
 
Tatizo hata imani za mitume huenda zikawa ni imani potofu : hatujui imani sahihi ni ipi for sure . Unayodhani kuwa ni imani sahihi., kuna maeneo inaonekana ni imani za majini na uchawi.

Imani bora ni kuheshimu imani za wengine, mila na desturi zao.
Kama zimo,aelewe
 
Kuna watu watajisifia walikokaa,wengine watasifu, na wengine watalaumu.
Je, uliwahi kujiuliza kwa nini meza ya kikao cha mawazili au kamati ya raisi hua ni duala, na si mmoja anakaa nyuma ya mwenzake?

Unadhani mambo mengine yanayoonekana ya ajabu au ya ovyo,hao CDFs wanapopokezana,hawayaoni! Unadhani, hicho kiti wao hawatamani kukikalia?
Je, kwa nini hawajaribu! Unahisi nguvu ndo hawana!

Ila, kati yao na hivyo vitu kuna fensi.
Na hili jambo ukilifikilia kwa mapana, nyuma yake kuna mengi sana. Na hapo ndo kaongea kwa mafumbo,hakika wengi hawataelewa.

Kikawaida,si yo yeye alietakiwa kutangaza hizo taarifa.
Na kama alikuwa ameruhusiwa,basi hilo jambo lilienda kirafiki kuliko kikazi.

Enewe,ni mengi ya kuongelewa,na kila mtu ataongea ya kwake,ila,wale watu wa karibu,wanaokaa ile meza,ndo wenye majibu sahihi. Japo pia na wao hawatakwambia,maana hayakuhusu. Tujilie wali wetu,dona au sembe,tununue bando zetu, tuingie jf tuburudike,lakini mambo ya huko juu,hatuyawezi.
 
Kwa mujibu wa maelezo ya Mabeyo (vipengere 7-10) VIONGOZI WOTE WAKUU walikuwa hawajui muendelezo wa madaraka ya Urais (succession) ikitokea Rais amekufa au hawezi tena kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Katiba ya JMT.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…