Nukuu 10 fikirishi na za hekima

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
NUKUU 10 FIKIRISHI NA HEKIMA

1. Ni heri kumheshimu mtu kwa juhudi zake kuliko kusibiri uje ujipendekeze kwake akiwa anakula mavuno ya juhudi hizo kwani huo Ni usakatonge hatari

2. Ni vema kumkosoa mtu usiyekubaliana na Mambo yake na kumpa mawazo mbadala angali hai kuliko kumngoja afe ama afeli ndipo uibuke kusema kwa jinsi ngoma alovyokuwa akiicheza nilijua kabisa kuwa hatoboi, huu ni unafiki mbaya Sana.

3. Ni vema kuamini yakuwa maendeleo yataletwa na Serikali itakayokuwa chini ya Uongozi Bora kuliko kusimamia kuwa maendeleo yataletwa na chama Fulani Cha siasa, kwamaana huo ni ufinyu wa fikra.

4. Ni vema kuamini katika nguvu ya Mungu kwetu kwamba Mungu anabariki wanaoambana kuliko kukaa kimya bila kufanya chochote huku ukijifananisha na ndege wa angani ukisubiri Muujiza Mungu atakuletea ugali na maharagwe, kwa maana huo Ni ufinyu wa fikra juu ya kwanini Mungu alikuumba kama ulivyo.

5. Ni Bora kufa kwa kupambana uovu kuliko kujilimbikiza Mali za uonevu na kufa kwa aibu na kuenda katika Moto wa milele.

6. Ni vema kuamini kuwa Elimu Ni ujuzi unaosaidia kupambana na shida za jamii Kama rushwa, umaskini, njaa, maradhi, unyonywaji, dhuluma na kupuuzwa; kuliko kuifanya elimu kuwa daraja la kupandia ngazi kuyaendea maisha mazuri haya Kama Ni kwa kuumiza wengine na kuwaacha ndugu, jamaa na jamii wakibaki na shida zao zilezile.

7. Kwa kiongozi wa umma Ni vema kutambua kuwa anayo nafasi hiyo kwasababu wapo watu wanahitaji msaada wa nafasi hiyo kuwatatulia kero zao na kuwafikisha katika hatua njema kuliko kuamini kuwa nafasi yake Ni ajira yake na anaweza kufanya anachotaka yeye na si watu wanachotaka.

8. Ni heri kwa mtu uliye juu ki siasa, uchumi ama kisanaa kumheshimu Kila mtu na kumuita 'mheshimiwa' kuliko kusubiri uje utumie nguvu utumie nguvu kubwa kuomba msamaha na kujishusha baada ya nafasi yako kukuponyoka na kujikuta wale uliowapuuza wanapanda pale ulipokuwa.

9. Unapokuwa na elimu kubwa ya darasani ni vema kuitumia kuwaasa wengine kuthamini elimu ili wavuke kuliko kuwa msomi na kurudi kuwaambia wale wasiokuwa nayo kuwa hakuna umuhimu wa kusoma wafanye shughuli zingine huku wewe ukisaka kwenda kuongeza elimu na watoto wako unawasomesha Ulaya na Marekani, huo ni ulaghai wa kibinafsi.

10. Ni vema kuamini ya kuwa kile uachokipenda Sana na kukiamini Kuna mtu hakipendi kabisa Wala hakiamini na kile usichokipenda Wala kukiamini Kuna mtu anakipenda Sana na anakiamini mno kwa maana kwa kuamini hivyo itakusaidia kujua jinsi njema ya kuishi na watu huku matakwa yenu yakiwa huru, binafsi na kutokuwafarakanisha

Think big be the best person you'd like to see, serve the Public interests.
👉❤️🇹🇿💪
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom