Ntapata wapi chanjo ya Surua kwa Mwanangu?

nyabhera

JF-Expert Member
Nov 25, 2011
660
729
Kwa zaidi ya miezi minne sasa mototo wangu alipaswa kupata chanjo ya Surua kama alivyopangiwa Wa wahudumu Wa afya.

Wauguzi katika zahanati ya umma ambako nimekuwa nikimpeleka kupata chanjo walinipangia yakuwa mtoto akifikisha miezi 9 nimrudishe apewe chanjo ya kinga ya ugonjwa wa Surua.


Mototo kafikisha miezi tisa tangu October 2016 lakini hafi Leo January 2017 kila nikienda apewe chanjo, nimekuwa nikijibiwa chanjo zimeisha nije siku nyingine.

Sasa nahitaji kujua hili tatizo la chanjo ni kwangu tuu au ni LA kitaifa.

Pili nisaidieni, hizi chanjo zinapatikana wapi tofauti na zahanati/hospital za umma. Kwa sasa napatikana Dodoma.
 
Pole,nahic huwa unachelewa tu ila chanjo zipo.huenda wanashindwa kutoa kichupa kizima kwa mtoto mmoja tu maana inayobaki itabidi imwagwe.jaribu kufika hapo kituoni saa2asbh siku ya chanjo uone itakuwaje.
 
Back
Top Bottom