NSSF wapigwa chini, Kiwira wapewa Wachina; Ngeleja abebeshwa lawama

Kama si wendawazimu, shamba la bibi au vingenevyo nashindwa kuelewa kwa nini tuendelee kuvumilia upuuzi huu:

1: Porojo na vijisababu vya kijinga kuhusu upungufu wa nishati ya umeme zimedumu zaidi ya miaka kumi sasa

2: Baada ya mitambo ya gesi Songosongo kukarabatiwa stori ya mgao ikabadilika na kwamba sasa makali yatapungua wiki hii hapo IPTL itakapopata shehena ya kutosha ya mafuta mazito kuendeshea mitambo yake na kwa hiyo kupatikana 90MW zaidi. Kwani walikuwa wapi siku zote hizi?

3:Symbion nao wataingiza 32.5MW zaidi kwenye gridi ifikapo August.
Cha ajabu ni kwamba jitihada za ununuzi wa mitambo hiyo wakati ikimilikiwa na Dowans kwa bei ya USD 60 million ulishindikana pale iliposemekana kwamba mitambo ile ni mitumba. Then ikaja Symbion na stori ikabadilika tena. safari hii tukasikia kwamba hali ya mitambo hiyo hiyo ni nzuri na hivyo wakainunua wao. Sasa mitambo hiyo inaiuzia TANESCO 80MW!!!

Kwa nini serikali igome kununua mitambo ya Dowans lakini iwe tayari kuikubalia TANESCO inunue umeme unaozalishwa na mitambo hiyo hiyo (sasa ya Symbion) na makapuni yale mengine (Independent Power Producers) yanayokamua 70% ya mapato ya TANESCO wakati nishati wanayozalisha ni 30%???
 
Tatizo la baadhi ya wabunge misimamo yao nje na ndani ya bunge hutofautiana. Hutetea maslahi binafsi badala ya umma. Heri wabunge hawa wasingezaliwa. Kweli wanatu-betray. Ndiyoooo huwa ndiyo lugha yao.
 
Acheni kumuonea Ngereja. Tatizo la umeme nii maono finyu ya wizara ya maji na nishati enzi ya rais Mwinyi. Walitakiwa kuwa na maono wakisaidiwa na viashiria mbali mbali vilivyokuwepo wakati ule kv. trend ya ukuaji wa idadi ya watu na shughuli baada kutoka uchumi hodhi kwenda uchumi huru. watu waliangalia watanufaika vipi na mabadiliko ya kiuchumi na hasa uchumi binafsi - kwao nishati ya dharura dharura ndo ikawa suluhu. Na bado tunao na wana nguvu ya ushawishi na utendaji kuliko Ngereja. Mwacheni kumuonea Ngereja bana!!!
 
Yetu macho sasa wameunga bajeti ya mkulo then wanatuletea kiini macho,hela itatoka wapi wakati bajeti ya mkulo tumeiona na imepita?siasa bwana kama karata unavyozichanga ndivyo utakavyofanikia.hatuna viongozi waliopo ni wasanii tu wa kuunga mkono na kugonga meza basi.
 
Ngeleja anadai tuvumiliane hivi kweli anajua watanzania wanavyosota na huu mgao!!!analeta hadith ya kulinganisha Japan na Tz.kwenye suala la Umeme
 
k aka acha kutetea ujinga. ngereja yupo wizarani hapo zaidi ya miaka 5 na tatizo la umeme


miaka 10 sasa . aliingia wizarani akijua changamoto zinazomkabili na kama alikuwa han jibu la Tatizo ni bora aachie ngazi kuliko kuendelea kulea uzembe. Tunahitaji waziri amabaye atakuja na suluhish na pale serikali itakapokataa ufumbuzi wake awe tayari kujiuzulu na sio wachumia tumbo kama ngereja

.
Acheni kumuonea Ngereja. Tatizo la umeme nii maono finyu ya wizara ya maji na nishati enzi ya rais Mwinyi. Walitakiwa kuwa na maono wakisaidiwa na viashiria mbali mbali vilivyokuwepo wakati ule kv. trend ya ukuaji wa idadi ya watu na shughuli baada kutoka uchumi hodhi kwenda uchumi huru. watu waliangalia watanufaika vipi na mabadiliko ya kiuchumi na hasa uchumi binafsi - kwao nishati ya dharura dharura ndo ikawa suluhu. Na bado tunao na wana nguvu ya ushawishi na utendaji kuliko Ngereja. Mwacheni kumuonea Ngereja bana!!!
 
Nilikuwa musoma kweny msiba toka tar 24 hadi leo narudi hakuna umeme,watz wanaish kwa tabu sana,ukiwaka ni masaa 6 umekatka,jamani huu umeme ni tatizo kubwa,ila naona wenzetu wa kanda ya ziwa ni balaa..ngeleja must resign.
 
Amesemaa ,amesemaaaaa,akasemaaaaaaaaaaaaa,alisemaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa,atasemaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
Kutwaaaa ni porojo tuu,wakimaliza wanaweka mwongozo chini kishaa haoo wanaenda kula raha na kina anti ezekiel posho imeingia,
dawa yenu iko motoni nyie subiri tu
 
Kama nakumbuka vizuri Serikali na Tanesco walitaka kununua hiyo mitambo ya Dowans,lakini kelele za akina Mwakyembe na Sitta na wananchi walipinga.Serikali ikanywea.
 
Kweli hii inaumiza sana! tunaomba wana jf mnaoelewa vizuri jambo hili mtufafanulie vizuri kwakweli! kama tulikataa kununua mitambo kwanini tunanunua umeme wao? tumeuza baskeli tumenunua pampu.
 
halafu baada ya kununua pump tunakodi baiskeli...ambayo baada ya miezi michache hela tutakayolipa itakuwa kubwa kuliko hela ya kununulia
 
Mkuu wala ujakosea, huu umeme wao wa kuunga unga una wa cost sana na hii yote kwa vile kila mtu anatumia kama dili la kupata rushwa na sio kufikiria mbeleni.

Viongozi wanashindwa kutafuta long term solution badala yake wanaona bora wapate chochote wao binafsi kupitia madili ya short term kuliko kulipa taifa umeme wa huakika.
 
mkuu wala ujakosea, huu umeme wao wa kuunga unga una wa cost sana na hii yote kwa vile kila mtu anatumia kama dili la kupata rushwa na sio kufikiria mbeleni.viongozi wanashindwa kutafuta long term solution badala yake wanaona bora wapate chochote wao binafsi kupitia madili ya short term kuliko kulipa taifa umeme wa huakika.
kwa best practice, ni nchi gani zinafanya hivi pia?
 
From LEONARD MWAKALEBELA in Dodoma, 26th June 2011 @ 20:00
DAILY NEWS
THE Government has accepted China's offer to run Kiwira Coal mine and therefore ditching the National Social Security Fund (NSSF) to run the same.

The Minister for Energy and Minerals, Mr William Ngeleja, told journalists here on Sunday that the Chinese government would invest 400 million US dollars (about 600bn/-) under a soft loan arrangement.

The minister was briefing the media on current status of power generation in the country and measures taken by the government and Tanzania Electric Supply Company (TANESCO) in addressing the situation.

Mr Ngeleja mentioned several criteria used to accept the Chinese government's offer including timing of applications to run the mine and magnitude of investment. Kiwira Coal mine is projected to generate 200MW upon its completion.

He revealed that five organisations including NSSF applied to run the project but the government decided to accept Chinese offer.

"NSSF applied to develop the mine last December while the Chinese applied before and pledged to invest 400 milliom US dollars through soft loans.


"NSSF advanced several reasons to take over the project including the reason that former investors of the project owe them a lot of money, but the former investors owe various institutions including CRDB Bank," the minister explained.

Mr Ngeleja noted that the government also considered other factors including capital, technology and expertise of applicants in power generation.

He further revealed that the government also took into consideration long relations between Tanzania and China.
(Aaaaarrrggggghhhhh :( )

He, however, appreciated the NSSF's offer, welcoming the Fund to invest in other projects such as development of natural gas projects.


The minister also urged private entities and individuals to invest in power generation as the Electricity Supply Act of 2008 had opened doors for private entities to generate power.

Mr Ngeleja said that the government was still pondering on whether to unbundle TANESCO in generation, transmission and distribution separate entities or not.

"Let me remind you that transmission of electricity is a very sensitive issue. But the private sector is allowed in power generation and they should seize the opportunity to generate power instead of insisting privatisation of TANESCO.


"People should not mislead the public that the government is entertaining TANESCO's monopoly, I wonder why private entities have not joined hands to generate power while they're allowed by the law," he stressed.

Speaking on the status of power supply in the country, the minister attributed the current power rationing to drought that had forced hydro power plants to operate below capacity.

He, however, expressed optimism that the situation would be addressed soon following conclusion of agreements between TANESCO and Agrrieko and Symbion in which the two firms would generate a total of 212.5MW.

Mr Ngeleja also stated that Treasury had pledged to release funds by this week to enable ITPL to generate 100MW.
He rubbished claims by some people that the government and TANESCO had not been doing enough to address power woes, adding that some people are orchestrating such claims to meet their political interests.

 
Sikio la kufa halisikii dawa. Tunaendesha kwenye one way lakini tukielekea kule ambako wenzetu wanatoka.
 
*Awalaumu wanasiasa kuhusu umeme
*Adai wanatafuta umaarufu kujadili mgao
*Awataka wananchi wawadharau, wawabeze
*Bwawa la Mtera hatarini kufungwa

Na Maregesi Paul, Dodoma


WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja amesema wanasiasa wanaobeza utendaji kazi wa Serikali na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wanafaa kubezwa na kudharauliwa.

Amesema ingawa mgao wa umeme nchini unawakera wananchi wengi na Serikali yenyewe, mgao huo haufai kujadiliwa kwa ushabiki kwa kuwa Serikali iko katika jitihada za kuutatua katika kipindi hiki cha awamu ya nne.

Ngeleja aliyasema hayo jana mjini hapa alipozungumza na waandishi wa habari kueleza jitihada za serikali za kukabiliana na mgao wa umeme unaoendelea nchini.

"Kwa vile mgao wa umeme ni janga la kitaifa linaloathiri shughuli za uchumi na jamii kwa taifa.

‘Kwa vile Serikali na TANESCO zina mipango ya kukabiliana na na mgao huo kupitia miradi mbalimbali, tunawaomba wananchi waivumilie Serikali na TANESCO kwa sababu inaendelea kutekeleza miradi iliyojiwekea.

"Tunawaomba wananchi wapuuze kabisa dhihaka, kejeli na kebehi zinazotolewa na watu hao wasiothamini juhudi na jitihada za kweli zinazofanywa na serikali kumaliza tatizo hilo nchini kwa sababu Serikali inaamini watu wote wanaopuuza na kubeza jitihada hizi wakati wakijua historia liliyopitia shirika hilo la umeme, wanafanya hivyo kwa makusudi na kwa masilahi yao binafsi kutafuta umaarufu wa siasa.

"Tatizo la mgao wa umeme katika nchi yetu ni tatizo halisi kama tatizo lililoikumba Japan kwa sasa baada ya nchi hiyo kuathiriwa na tetemeko la ardhi lililoharibu mitambo ya nyuklia ambayo ilikuwa ikizalisha umeme nchini humo kwa kiasi kikubwa kama ilivyo kwetu ambako asilimia 55 ya umeme wetu unategemea maji.

"Suluhu ya kumaliza mgao wa umeme katika nchi yetu siyo kubeza jitihada zinazofanywa na serikali bali ni kuunganisha nguvu za wadau wote kuitia moyo Serikali kutokana na jitihada inazofanya ikiwamo kuwa na njia za dharua za kukabiliana na mgao huo.

"Kwa hiyo tunawoamba wananchi waendee kutuvumilia, tuimarishe mshikamano, utulivu na amani na tuwaepuke wanaobeza juhudi za serikali kwa masilahi binafsi na kwa masilahi yao siasa," alisema Ngeleja.

Akizungumzia mgao huo wa umeme, alisema umesababishwa na upungufu wa maji katika mabwawa ya Mtera, Kidatu, Nyumba ya Mungu, Hale na Kihansi.

Ngeleja alisema bwawa la Mtera ambalo ndilo linalotegemewa zaidi kwa uzalishaji wa umeme nchini, hadi kufikia juzi lilikuwa na ujazo wa meta 690.87 juu ya usawa wa bahari wakati kina cha chini cha kuzalisha umeme katika bwawa hilo ni meta 690 na kina cha juu cha kuzalisha umeme ni meta 698.50.

"Tunapenda kuwakumbusha Watanzania, kwamba upungufu wa maji katika mabwawa yetu umeathiri sana uwezo wa kuzalisha umeme kwa sababu kwa sasa hivi asilimia 55 ya umeme wetu unatokana na maji… kama nilivyokwishasema, asilimia 34 unatokana na gesi asili na asilimia 11 unazalishwa kwa mafuta.

"Ndugu wanahabari, baada ya serikali kubatilisha uamuzi wa kulibinafsisha TANESCO mwaka 2005 na baada ya serikali ya awamu ya nne kuingia madarakani, mwaka 2006 miradi minne mikubwa isiyotegemea maji ilibuniwa kuondoka katika utegemezi wa maji na kutegemea vyanzo vingine visivyoweza kuathiriwa na uhaba wa maji.

"Miradi hiyo minne inayokusudiwa kuongeza kiasi cha megawati 645 katika gridi ya taifa ni mradi wa makaa ya mawe uliko Kiwira Mbeya uliotarajiwa kuzalisha megawati 200 mwaka 2009/2010 na Mradi wa Mnazi Bay unaotumia gesi asili uliotarajiwa kuzalisha megawati 300 uliotarajia kukamilika mwaka jana.

"Mradi mwingine ni uamuzi wa serikali wa kununua mitambo ya kuzalisha umeme kwa gesi asili megawati 100 iliyofungwa Ubungo Dar es Salaam mwaka 2008 na hatua nyingine ni kununua mitambo ya kuzalisha umeme kutokana na gesi asili yenye uwezo wa kuzalisha megawati 45 na kufungwa Tegeta Dar es Salaam na kuanza uzalishaji mwaka 2009 mwishoni.

"Katika hili, dhamira ya Serikali ilikuwa ni kuongeza umeme wa megawati 645 kwenye gridi ya taifa kwa kipindi cha mwaka 2006-2010, lakini kutokana na sababu mbalimbali, kati ya megawati 645 zilizotarajiwa kuzalishwa ni megawati 145 tu ndizo zilizozalishwa.

"Pamoja na hayo, serikali sasa imejielekeza katika mipango ya dharura ya muda mfupi ambako sasa Kampuni ya Symbion imeshaanza kuzalisha megawati 80 kati ya 112.2 inayotarajiwa, Serikali pia imeingia mkataba na Kampuni ya Aggreko ambayo kufikia mwishoni mwa Agosti mwaka huu itakuwa ikizalisha megawati 100.

"Pamoja na mipango ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu, Wizara ya Fedha na Uchumi imeshakubali kutoa fedha za kununulia mafuta ya kuendeshea mitambo ya IPTL itakayozalisha megawati 100 kutoka megawati 10 za sasa," alisema.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, William Mhando, alisema katika mkutano huo, kwamba Bwawa la Mtera ambalo ndilo mhimili wa uzalishaji wa umeme linaweza kufungwa Agosti mwaka huu baada ya kina cha maji kupungua.

Hata hivyo, alisema iwapo kina cha ujazo wa kuzalisha umeme kitafikia mwisho kabla mvua hazijanyesha, shirika hilo linaweza kuomba kibali cha Serikali ili bwawa hilo liendelee kuzalisha umeme kama ilivyowahi kutokea mwaka 2006 baada ya maji kupungua.

Naye Debora Sanja anaripoti kuwa wabunge jana waliibana serikali kuhusu upatikanaji wa umeme likiwamo tatizo la mgao wa umeme, mikataba mibovu na gharama kubwa ya nishati hiyo.

Akichangia katika semina ya nishati na madini iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati na Madini mjini Dodoma, Mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene (CCM) alisema watanzania hawahitaji maelezo wala utafiti wowote zaidi ya umeme wa uhakika na wa bei nafuu.

Alisema hata kama Tanzania ya leo ikiweza kuzalisha umeme wa ziada bado haitaweza kuleta mapinduzi ya viwanda kwa kuwa nishati hiyo ni ghali sana.

"Hizo kelele za umeme tumeanza kuzisikia tangu Ngeleja ameingia madarakani lakini hadi leo hakuna maendeleo mimi sioni hatua yoyote tuliyoifikia, miaka yote ni matatizo ya umeme, huo usomi wetu unatusaidiaje kuondokana na tatizo hili," alisema Simbachawene.

Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi) alisema mfumo wa sasa wa ulipaji wa gharama za umeme kwa makampuni yanayouzia umeme ni mbovu.

"Mfumo wetu wa ‘Capacity Charge' wa kulipia umeme uwe umezalisha au haujazalisha ni mbovu tuachane nao. Zipo nchi ambazo hawafanyi hivyo mfano mzuri ni Malaysia,"alisema.

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA) alisema Shirika La Umeme Tanzania (TANESCO) likitumia asilimia 70 ya mapato yake kuyalipa makampuni ya kuzalisha umeme ambayo yanazalisha asilimia 40 tu ya umeme.

Lissu alisema hali hiyo inatokana na mikataba mibovu ikiwamo ya Dowans, Richmond na IPTL na kuitaka serikali kuiingilia upya mikataba hiyo.

Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema (TLP), aliitaka serikali iwahahakikishie kuhusu ubora wa mitambo ya Dowans kwa kuwa awali wakati serikali walipotaka kuinunua walisema mitambo hiyo mibovu na haifai kuzalisha umeme.

"Leo hii kaja huyo Mmarekani kainunua mnasema mitambo ya kisasa wakati tuliambiwa haifai tunataka kujua huu ni mchezo gani au ni mtu ndiyo alikuwa hatakiwi," alisema Mrema.

Waziri Ngeleja akijibu hoja hizo alisema ni bora watanzania wakasahau historia ya Dowans na kuwa mitambo hiyo ni bora na ya kisasa.

Kuhusu mikataba, alisema wameshaliona hilo na wameanza kulishughulikia kwa vile mingi ilikuwa ya ufisadi.
Mkurungezi Mtendaji wa TANESCO, William Mhando alisema mgao wa umeme utapungua makali Agosti na utaisha Desemba.

Alisema hata hivyo mgao wa umeme utakwisha mwaka 2014/15 ambako shirika litaanza kuzalisha ziada kutokana na miradi mbalimbali kutekelezwa.
 
Suala la kununua mitambo kwa sheria iliyokuwepo lilikuwa haliwezekani na uamuzi wa kukataa kwa wakati ule ulikuwa sahihi kwani ulikuwa unakinzana na sheria na kufungua mianya ya watu kutumia dirisha hilo kutuletea tena manunuzi ya vifaa chakavu. It was a right decision na kama Tanesco walikuwa na dhamira, toka 2008 hadi leo wangekuwa wameshanunua mitambo mipya ya kwao. Lakini kwa sababu msukumo ulitoka kwa watu wenye maslahi, wametufikisha hapa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom