nssf to ppf

mkonowapaka

JF-Expert Member
Feb 19, 2010
1,493
767
wadau..habari za leo...

naomba kujuzwa kama inawezekana pale mtu unapohama kutoka mfuko wa nssf kwenda ppf kuhama na fedha zako....i mean kuhamishia fedha zilizopo kwenye akaunt yangu kwenda huko nnakohamia kiofisi....


hope nimeeleweka
 
Mimi nilitaka kuhama PPF kwenda NSSF,nikafika NSSF kupata muongozo lkn walichonambia ni kuwa kama nataka kuhamisha mafao yangu PPF basi niende kule nifunge account yangu,then niyabebe hayo maduhuli kuwapelekea wao,hawana mutual agreed means btn themselves.
 
aisee mi naomba msaada wa jinsi ya kuzichukua hela zangu sitaki wakae nazo..

wanakaa na hela halafu hawatoi riba baadae
 
N S S F
N = Not
S = Supportive for
S= Small ownership
F= Families

PPF
P = Preference is not for
P = Poor
F = Families
 
Jamani naomba nijuzwe kama hawa ppf na nssf hua wanatoa riba kulingana na fedha ulizowekeza huko kwao.
 
Sheria za sasa za mifuko hii haziruhusu mtu kuhama ila labda uchukue hela yako ukaanze nayo katika mfuko mwingine.Kuhama kunawezekana kutoka GEPF kwenda PSPF na vice versa kama mazingira yaliyokatika sheria yakatokea.Mdhibiti wa mifuko ya hifadhi ya jamii yuko katika mchakato akishirikiana na mifuko wa kubadili taratibu za malipo ili malipo ya kiinua mgongo yasitofautiana ila mifuko itofautiane kutokana na mafao wanayotoa.Pia karibuni hapa,watumishi wote wanapoanza ajira mara ya kwanza wataruhusiwa kuchagua mfuko waupendao ila ukiingia tu..hakuna kuhama.Lakini wewe mwenye kutaka kuchukua hela yako nakushauri ukiipata uende ukajiwekee akiba katika mfuko wa GEPF kwani wameanzisha scheme nyingine ya voluntary ambayo inamwezesha mfanyakazi au aliyejiajiri kujiwekea akiba zaidi zaidi zitakazomfaa huko mbeleni.uangalie tovuti yao www.gepf.or.tz kwa maelezo zaidi
 
Back
Top Bottom