NSSF ni janga, Rais Samia itazame taasisi hii

NEWSINKP

Member
Sep 26, 2016
77
92
Wasalaam,

Nimeachishwa kazi mwezi wa 3. Nimeenda kuangalia statement yangu ya michango inaonesha haijawasilishwa na mwajiri wangu kwa miezi 16. Nimefuatilia kwa mwajiri ananipiga tarehe tuu aliniambia atazipeleka.

Sasa najiuliza NSSF kazi yao ni nini kama sio pamoja na kuwakagua waajiri na kuwachukulia hatua kwa kutowasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati. Na ukizingatia wafanyakazi wanakatwa pesa zao kila mwezi, ila kwa nini hazipelekwi NSSF, zinaenda wapi? NSSF mko wapi? Au hamna mandatory ya kukagua waajiri wasiopeleka michango ya wanachama wenu?
 
Mkuu hii Nchi mifumo yake ni migumu sana hata hivyo nasi wafanyakazi huwa tunajisahau sana hasa sector binafsi , kazi ya NSSF ni pamoja na kufuatilia michango ya mwanachama ili ikihitajika tu iwe tayari lakini Afrika ni Afrika tuu unakuta michango haijapelekwa au kama imepelekwa Wanasiasa wamechota pesa zote unaanza kuzungushwa tuu.

WATANZANIA KWA UJUMLA WETU TUSIMAMIE MABADILIKO YA MIFUMO YETU NI YA OVYO SANA

Hata hivyo pole sana kwa kupoteza kazi najua maumivu yake maana nilipita njia hiyo miaka 2 iliyopita hakika ni kipindi kigumu sana.
 
Ukiondoa wasanii na MaDC, Maelfu ya vijana- hawana ajira...Speaker na Mawaziri wanasema tu vijana mkajiajiri..But how? #UVCCM -kazi yao ni kupambana na Upinzani? hoja zao za kushawishi vijana ni zipi?

Sasa Wafanyakazi ni lazima waungane na vijana kudai #KATIBAMPYA

Baadhi ya Sera/Sheria mbovu za nchi ni kuwanyang’anya vijana uwezo.

Hapa naongelea vijana kuminywa kwa kuporwa haki zao, kunyimwa haki na kupuuzwa (hawasikilizwi). Naanza kwa Kuongezeka kwa Deni la Taifa na Propaganda mfu za Serikali, zenye lengo la kuhadaa umma ili kubaki madarakani tu. Serikali ya AWAMU YA 5 ilitamka kuwa inajenga miradi mikubwa kwa FEDHA za ndani. Asilimia kubwa ya Watanzania waliamini na kushangilia, na wale wachache wenye uelewa hawakupewa nafasi ya kuhoji. Imekuja kujulikana kuwa, FEDHA za Mifuko ya Jamii zilichukuliwa na Wafanyakazi wakaporwa haki zao za kulipwa #NSSF FAO LA KUJITOA na kuchelewesha malipo ya Wastaafu.

Vijana wasomi, waliosoma sayansi na wenye ujuzi wameajiriwa kwenye Makampuni, Mashirika na Viwanda. Hizi ni talent, na hazina za wasomi kwa nchi, na walivyoajiriwa kwenye haya Makampuni na Viwanda, wamepata fursa ya kuongeza utaalamu na uzoefu. Hii ndio Econonomic interelligency ambayo Serikali ilipaswa kutumia ili kunyanyua uchumi wa nnchi through Innovation. Ajira na mikataba za hawa vijana (wenye utaalamu na uzoefu-Innovation) zilivyokoma, Serikali iliwanyima Akiba zao (PESA za NSSF). Kumbuka Serikali ilifuta fao la kujitoa mwaka 2018 na kuweka Fao la kukosa ajira. Watu wote skilled labour (wataalamu hawa), hawapewi akiba yao, Haki imepotea. Hawa watu wangelipwa fedha zao, wangeweza kujiajiri kwa kufungua makampuni, kujenga viwanda vidogo. Badala yake hawa skilled labour wanaambiwa wasubiri miezi 18 na kama hawataajiriwa, wakae hadi 55 years wastaafu.

Serikali ilitumia pesa za mifuko ya jamii (Kukopa au kupora kienyeji) ili kujenga miradi. Hapo awali serikali imesema inajenga miradi kwa pesa za ndani (propaganda)..Lakini ukweli wenyewe ni kupora haki za wafanyakazi vijana na mafao wastaafu. Pia Serikali ilikopa sana Nje na kwenye mabenki, ndio maana deni la taifa limepaa sana.

Serikali inapaswa kuwapa wafanyakazi akiba zao ili waweze kutumia skill zao na uzoefu waliopata katika makampuni/viwanda ili kufungua biashara mpya. Hii ndio namna ya kutanua wigo wa Kodi (MWugulu NCHEMBA TRA). Mitaji itatoka wapi ya biashara mpya kwa wazawa kama mikopo benki sio rafiki? Suluhisho ni Serikali kurejesha FAO LA KUJITOA NSSF na kulipa wafayakazi akiba zao kwa Haki.

Serikali inatakiwa kuwezesha vijana, kutoa International passport kwa graduate wote, ili wapambane fursa za ajira kokote duniani. Baadae watakuwa diapora kubwa inayotuma pesa Tanzania, kama ilivyo Zimbabwe, Kenya na India walivyoenda wengi Canada na UK. Serikali kurejesha Fao la Kujitoa, Hasa kwa Sekta binafsi, kwa kuzingatia kuwa Sekta binafsi Security ya ajira ni delicate sana.
 
Wasalaam,

Nimeachishwa kazi mwezi wa 3. Nimeenda kuangalia statement yangu ya michango inaonesha haijawasilishwa na mwajiri wangu kwa miezi 16. Nimefuatilia kwa mwajiri ananipiga tarehe tuu aliniambia atazipeleka.

Sasa najiuliza NSSF kazi yao ni nini kama sio pamoja na kuwakagua waajiri na kuwachukulia hatua kwa kutowasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati. Na ukizingatia wafanyakazi wanakatwa pesa zao kila mwezi, ila kwa nini hazipelekwi NSSF, zinaenda wapi? NSSF mko wapi? Au hamna mandatory ya kukagua waajiri wasiopeleka michango ya wanachama wenu?
unareemba, babu mpeleke kizimbani! na mjulishe, fasta tuu utaona mpunga unasoma.
 
Hao NSSF ingekua nna uwezo niwaroge,bi mkubwa ana hali ngumu kiafya tunafatilia mafao toka mwezi january adi leo wanamzungusha tu
Ukiangalia hamna ela ya kusema atapata tiba hao NSSF mafao yake hawataki kumpa!
Mungu anawaona hao siku yako itakuja na ndugu zao watapata mateso kama wanayotupa wananchi,
 
Ukiondoa wasanii na MaDC, Maelfu ya vijana- hawana ajira...Speaker na Mawaziri wanasema tu vijana mkajiajiri..But how? #UVCCM -kazi yao ni kupambana na Upinzani? hoja zao za kushawishi vijana ni zipi?

Sasa Wafanyakazi ni lazima waungane na vijana kudai #KATIBAMPYA

Baadhi ya Sera/Sheria mbovu za nchi ni kuwanyang’anya vijana uwezo.

Hapa naongelea vijana kuminywa kwa kuporwa haki zao, kunyimwa haki na kupuuzwa (hawasikilizwi). Naanza kwa Kuongezeka kwa Deni la Taifa na Propaganda mfu za Serikali, zenye lengo la kuhadaa umma ili kubaki madarakani tu. Serikali ya AWAMU YA 5 ilitamka kuwa inajenga miradi mikubwa kwa FEDHA za ndani. Asilimia kubwa ya Watanzania waliamini na kushangilia, na wale wachache wenye uelewa hawakupewa nafasi ya kuhoji. Imekuja kujulikana kuwa, FEDHA za Mifuko ya Jamii zilichukuliwa na Wafanyakazi wakaporwa haki zao za kulipwa #NSSF FAO LA KUJITOA na kuchelewesha malipo ya Wastaafu.

Vijana wasomi, waliosoma sayansi na wenye ujuzi wameajiriwa kwenye Makampuni, Mashirika na Viwanda. Hizi ni talent, na hazina za wasomi kwa nchi, na walivyoajiriwa kwenye haya Makampuni na Viwanda, wamepata fursa ya kuongeza utaalamu na uzoefu. Hii ndio Econonomic interelligency ambayo Serikali ilipaswa kutumia ili kunyanyua uchumi wa nnchi through Innovation. Ajira na mikataba za hawa vijana (wenye utaalamu na uzoefu-Innovation) zilivyokoma, Serikali iliwanyima Akiba zao (PESA za NSSF). Kumbuka Serikali ilifuta fao la kujitoa mwaka 2018 na kuweka Fao la kukosa ajira. Watu wote skilled labour (wataalamu hawa), hawapewi akiba yao, Haki imepotea. Hawa watu wangelipwa fedha zao, wangeweza kujiajiri kwa kufungua makampuni, kujenga viwanda vidogo. Badala yake hawa skilled labour wanaambiwa wasubiri miezi 18 na kama hawataajiriwa, wakae hadi 55 years wastaafu.

Serikali ilitumia pesa za mifuko ya jamii (Kukopa au kupora kienyeji) ili kujenga miradi. Hapo awali serikali imesema inajenga miradi kwa pesa za ndani (propaganda)..Lakini ukweli wenyewe ni kupora haki za wafanyakazi vijana na mafao wastaafu. Pia Serikali ilikopa sana Nje na kwenye mabenki, ndio maana deni la taifa limepaa sana.

Serikali inapaswa kuwapa wafanyakazi akiba zao ili waweze kutumia skill zao na uzoefu waliopata katika makampuni/viwanda ili kufungua biashara mpya. Hii ndio namna ya kutanua wigo wa Kodi (MWugulu NCHEMBA TRA). Mitaji itatoka wapi ya biashara mpya kwa wazawa kama mikopo benki sio rafiki? Suluhisho ni Serikali kurejesha FAO LA KUJITOA NSSF na kulipa wafayakazi akiba zao kwa Haki.

Serikali inatakiwa kuwezesha vijana, kutoa International passport kwa graduate wote, ili wapambane fursa za ajira kokote duniani. Baadae watakuwa diapora kubwa inayotuma pesa Tanzania, kama ilivyo Zimbabwe, Kenya na India walivyoenda wengi Canada na UK. Serikali kurejesha Fao la Kujitoa, Hasa kwa Sekta binafsi, kwa kuzingatia kuwa Sekta binafsi Security ya ajira ni delicate sana.
Mkuu ifungulie Uzi wake ujumbe uwafikie Wahusika....
 
Katiba mpya ni muhimu ili fedha za wafanyakazi NSSF zisimamiwe na TUCTA

RUDISHA FAO LA KUJITOA
 
Back
Top Bottom