NSSF na WESTADI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NSSF na WESTADI

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MrNSSF, Sep 28, 2011.

 1. MrNSSF

  MrNSSF Senior Member

  #1
  Sep 28, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  sina mengi ya kusema..tazameni Video hapo chini:

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  Sep 28, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu nimepata wasaa wa kuisikiliza. Sema sasa tatizo ni nini? Mchango mdogo na mafao tele au?
   
 3. MrNSSF

  MrNSSF Senior Member

  #3
  Sep 28, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  NSSF, We protect your future.

  dola 300 kwa mwaka, hakuna longo longo wala nini

  mtu akifa tunamsafirisha, kwa gharama za NSSF toka jimbo lolote lile atakapokuwa, pamoja na ticket ya BURE kwa ajili ya msindikizaji

  sasa haya mambo ya kuchangishana kwenye blogs na kupeana account number kiholela yatakuwa hakuna
   
 4. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #4
  Sep 28, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu wa hapa nchini je Bima yao inasemaje? Najua kuna wanaochangia zaidi ya dola 300 kwa mwaka je nao wanapata faida kama hizo? Hao wenzetu ambao wako ughaibuni si ndio tunawategemea kwamba huenda uchumi wao una ahueni kwa maana hiyo wangechangia zaidi kuliko hawa wenzetu wa hapa TZ au?
   
 5. Silly

  Silly JF-Expert Member

  #5
  Sep 28, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 508
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Labda sijaipata vizuri lakini nimeelewa kama vile ni kwa wale wageni na wanaoishi nje ya Tanzania ndio wlengwa hapa.
   
 6. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #6
  Sep 28, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Hii ni dollar $300 kwa mwaka na unapata Health Care kama ukienda Tanzania wewe na Mke wako, vilevile unaweza kuingiza watu wanne Tanzania kwenye hii Healthcare na wakatibibiwa bila kulipa gharama nyingine. Kama mtu atakufa ughaibuni wanatoa tichecket ya msindikizaji, Wanalipa utunzaji wa maiti na wanasafirisha mwili mpaka Tanzania. Mimi naona ni fair na ina ukweli maana walianza toka mwaka jana.
   
 7. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #7
  Sep 29, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Daraja letu la Kigamboni vp MrNSSF umekimbia kule kwenye major projects in Tanzania tunakuhitaji tunaomba ufafanuzi gharama za ujenzi wa daraja zitarudishwaje?
   
 8. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #8
  Sep 29, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Daraja lina uhusiano gani na hili? Hilo ni swali nzuri kwa wizara ya ujenzi na magufuli kwani ndiyo wafuataliaji!. Kingine cha kuelimishana ni kwamba hii siyo Investment kubwa kwa NSSF kwani pesa inatoka kwa Watanzania waishio nje kabla hata ya kupata huduma yeyote!!. Hii ni Bima ambayo NSSF itatengeneza pesa! na sio kutoa pesa kama kwenye barabara. NSSF wanatakiwa kufanya vitu kama hivi vya kuongeza maisha ya wananchi kwenye afya na uchumi badala ya mambo ya madaraja.
   
 9. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #9
  Sep 29, 2011
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Kuna tatizo kubwa ambalo waanzilishi hawakulifikiria hasa kama wanawalenga watz waishio nje ya nchi.
  1. 300/= kwa mwaka ni nyingi kulinganisha na benefits wanazotoa. Kusafirisha mwili ni 10,000 nauli ya msindikizaji ni 2,500. Hapo inamaana unanunua bima isiozidi 20,000/= kwa karibu 25/= kwa mwezi. Ukiangalia washindani wao wanatoa mpaka bima ya mpaka 800,000 kwa kuchangia 25/= kwa mwezi. Swali je watz ambao ni mawakala wa bima Marekani walishirikishwa.
  2. Kijana mwenye afya njema wa umri wa miaka 24 hawezi kuchangia bima sawa na mzee wa miaka 65.
  3. Ntarudi baadae
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Bambo

  Bambo JF-Expert Member

  #10
  Sep 29, 2011
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 237
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  hongera sana NSSF,karibuni sana UK.hakuna mtu mwenye akili timamu ataacha kujiunga kwani zile hela tunazoombwa kutuma sijui mama anaumwa sasa basi..
   
 11. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #11
  Sep 29, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Hizi huduma ni kwa Watamzania wote nje ya nchi?

  Ili kupata maelezo zaidi na kuunganishwa na huduma tunatumia procedures gani?
   
 12. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #12
  Sep 29, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Mambo mengi umesahau kitu kimoja hii ni bima na kifo na afya pamoja. Vilevile hata kama afya yako ni nzuri weka watu wanne Tanzania na watapata huduma kwenye hospitali yeyote (watu wanne!!). Vilevile hata kama una afya nzuri unaweza kwenda Tanzania na mke wako au mwenyewe na kupata malaria hii bima inaweza kutumika hapo. Mimi nasosema wamefanya vizuri kuingiza bima ya afya na kuweza kuingiza watu 4 Tanzania ni jambo jema chukulia hata wazazi wako na ndugu zako bima lakini wakati huohuo unajikinga na boma ya afya na kifo ughaibuni.
   
 13. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #13
  Sep 29, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mkuu,

  Wadhamini na wajenzi wa Daraja la Kigamboni ni NSSF. MrNSSF alikuja kwa mikikimikiki ila naona amekimbia mjadala kule. Lina faida hilo swali kwani kule jamaa walimuuliza katika thread nyengine je pesa za ujenzi zinazotoka NSSF zitarudishwaje? Na ukisema halina msingi kumbuka NSSF ni taasisi ya fedha na hivyo vidola 300 vyako unavyotoa kila mwaka ndio vinatumika kuzungushia ili NSSF iweze kufanya uwekezaji. Sasa kama daraja la Billion kadhaa linajengwa halafu NSSF washindwe kurudisha gharama zao za ujenzi na faida vile vijidollar vyenu vinayeyuka ndio narudia tuelemishe kwanza kuhusu daraja la Kigamboni mzee NSSF ndio uje katika dola 300.
   
 14. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #14
  Sep 29, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Mimi kwa mawazo yangu NSSF ni kati ya taasisi nzuri kuliko zote Tanzania!. Nimekutana na viongozi wa juu kabisa wa NSSF kwa miaka mitatu sasa na nimekutana na viongozi wengi sana kwenye Dicota lakini hawa jamaa ni wa kweli na ni lazima uelewe kwenye Balance Sheet yao wana zaidi ya $1.5Billion za assets na Liabilities za watu wote ni kana nusu ya hiyo hivyo biashara zote sasa wanafanya na pesa ya faida. Hizi taasisi kama zikipata viongozi wazuri ni nzuri kuliko kutegemea vitu vya serikali. Vilevile pamoja na kwamba kuna ufisadi kwenye mambo mengi Tanzania NSSF ina rank ya kwanza kwa kutokuwa na ufisadi kwasababu wanalipana vizuri sana hawana sababu ya kuiba.
   
Loading...