nokwenumuya
JF-Expert Member
- Jun 29, 2019
- 810
- 2,851
NSSF KWAFUKUTA: MENEJA MPYA WA MAJENGO NSSF ANAFUKUZA WAPANGAJI AMBAO NI WALIPAJI WAZURI WA KODI
- Alipewa cheo na Mkurugenzi Mkuu bila kufuata taratibu.
- Aliletwa kama afisa wa kawaida toka PPF, ambako ndipo alipotokea Mkurugenzi wa sasa pia.
- Anawafukuza wapangaji wanaolipa vizuri kwa kigezo cha kupata nafasi za kuweka ofisi.
- Ofisi zinapewa maeneo makubwa kuliko mahitaji yanayostahili.
- Ofisi nyingi alizoondoa watu ziko wazi.
- Case study hii ni kwa Jengo la Benjamin Mkapa pekee. Mengine nashauri yafuatiliwe.
Siku moja Mkurugenzi Mtendaji alishuka na kufika ofisi ya watu wa Ufundi na akamkuta Augustino yuko peke yake, akatumia kigezo hicho kumpandisha cheo, toka afisa wa chini hadi kuwa Estate Manager, bila kuzingatia katika idara hiyo baada ya kuripoti kazini huwa wana kazi nje ya ofisi kushughulika na mambo ya maintenance, au kwenda kushughulikia majengo mengine yaliyo chini ya NSSF. Hivyo inaonekana kuna mpango uliopangwa na Mkurugenzi Mtendaji na yeye, kwa kuwa wote walitoka PPF basi akamtafutia nafasi ambayo ni dhahiri uwezo wake kuitendea haki ni mdogo.
Katika hilo jengo la Benjamin Mkapa hivi sasa amewaondosha wapangaji wa muda mrefu, ambao wamekuwa wakilipa kodi zao kwa wakati na kwa uaminifu, hadi sasa napoongea amewaondoa wapangaji watatu, mmoja kamuhamishia eneo jingine ambalo ni dogo kuliko la awali (ina maana mapato yanapungua), wengine bado wanavutana katika mchakato wa kuwaondoa.
Hivi sasa zaidi nusu ya majengo ya NSSF hayana wapangaji, mtu huyu badala ya kuweka mkakati wa kupata wapangaji wapya kwanza yeye ndio anafukuza wapangaji ambao wanafanya biashara zao na kulipa kodi, ambayo ndio kipato ambacho kinasaidia kuendesha taasisi, mtu huyu asipoangaliwa ataua baishara ya Real Estate iliyo chini ya NSSF, ni Dhahiri uwezo wake ni mdogo, huenda anastahili kubaki kuwa fundi wa upimaji.
MAKAMPUNI AMBAYO AMEFANIKIWA KUYAONDOA MPAKA SASA NI:-
- PANACOM SOLUTIONS LTD
- WILD DOGS TOURS & TRAVEL
- STELLAH TRAVELS
- SOLOHAGA CO. LTD.
- ETERNAL INTERNATIONAL
- GESTA FINANCE
- TAN ADVERTS
- UNIVERSITY ABROAD REPRESENTATIVE (UAR)
- JUMBO CAMERA HOUSE
- ORIFLAME
- NA MENGINE AMBAYO BADO HAJAYATAJA.
Huyu ni mfano wa wafanyakazi wa taasisi za umma ambao maamuzi yao yasiyo ya busara yamekuwa yakigharimu hizi taasisi kwa kiwango kikubwa. Mfano hao wapangaji anaowandoa kwa ulazima wana mikataba ya miaka mitatu, na kuendelea, je wakiamua kushitaki si mfuko itabidi ulipe fidia? Mimi nimeandika kama raia mwema, jambo hili liangaliwe na watu walio katika vyombo vya maamuzi ili lipatiwe ufumbuzi, na huyu ni Estate Manager wa nchi nzima, haya yote kayafanya Benjamin Mkapa Towers pekee, hatujui katika majengo mengine na mikoa mingine.
NB: CHA AJABU OFISI AMBAZO AMEWAONDOA WATU ZIKO TUPU, HAKUNA KINACHOENDELEA, ZIKO WAZI, UKITAKA ZIONA FIKA MEZZANINE FLOOR NA UZUNGUKE, KAMA ULISHANGAA YA MUSA SASA UTAONA YA FIRAUNI.