NSSF kwafukuta: Meneja mpya wa majengo NSSF anafukuza wapangaji ambao ni walipaji wazuri wa kodi

nokwenumuya

JF-Expert Member
Jun 29, 2019
805
2,843
NSSF KWAFUKUTA: MENEJA MPYA WA MAJENGO NSSF ANAFUKUZA WAPANGAJI AMBAO NI WALIPAJI WAZURI WA KODI
  • Alipewa cheo na Mkurugenzi Mkuu bila kufuata taratibu.
  • Aliletwa kama afisa wa kawaida toka PPF, ambako ndipo alipotokea Mkurugenzi wa sasa pia.
  • Anawafukuza wapangaji wanaolipa vizuri kwa kigezo cha kupata nafasi za kuweka ofisi.
  • Ofisi zinapewa maeneo makubwa kuliko mahitaji yanayostahili.
  • Ofisi nyingi alizoondoa watu ziko wazi.
  • Case study hii ni kwa Jengo la Benjamin Mkapa pekee. Mengine nashauri yafuatiliwe.
Hivi karibuni Mkurugenzi Mtendaji wa NSSF alimteua Bwana Augustino K. Paul kuwa meneja wa majengo (Estate Manager). Augustino K. Paul alihamishwa toka PPF baada ya sheria ya kuunganisha mifuko ya hifadhi ya Jamii. Na alikuwa ni afisa mdogo anayehusika na upimaji wa maeneo katika majengo ili kugawa kwa square meters pamoja na kushughulika na mambo ya ufundi na repair, ambako katika ofisi yao kuna watu wengi.

Siku moja Mkurugenzi Mtendaji alishuka na kufika ofisi ya watu wa Ufundi na akamkuta Augustino yuko peke yake, akatumia kigezo hicho kumpandisha cheo, toka afisa wa chini hadi kuwa Estate Manager, bila kuzingatia katika idara hiyo baada ya kuripoti kazini huwa wana kazi nje ya ofisi kushughulika na mambo ya maintenance, au kwenda kushughulikia majengo mengine yaliyo chini ya NSSF. Hivyo inaonekana kuna mpango uliopangwa na Mkurugenzi Mtendaji na yeye, kwa kuwa wote walitoka PPF basi akamtafutia nafasi ambayo ni dhahiri uwezo wake kuitendea haki ni mdogo.

Katika hilo jengo la Benjamin Mkapa hivi sasa amewaondosha wapangaji wa muda mrefu, ambao wamekuwa wakilipa kodi zao kwa wakati na kwa uaminifu, hadi sasa napoongea amewaondoa wapangaji watatu, mmoja kamuhamishia eneo jingine ambalo ni dogo kuliko la awali (ina maana mapato yanapungua), wengine bado wanavutana katika mchakato wa kuwaondoa.

Hivi sasa zaidi nusu ya majengo ya NSSF hayana wapangaji, mtu huyu badala ya kuweka mkakati wa kupata wapangaji wapya kwanza yeye ndio anafukuza wapangaji ambao wanafanya biashara zao na kulipa kodi, ambayo ndio kipato ambacho kinasaidia kuendesha taasisi, mtu huyu asipoangaliwa ataua baishara ya Real Estate iliyo chini ya NSSF, ni Dhahiri uwezo wake ni mdogo, huenda anastahili kubaki kuwa fundi wa upimaji.

MAKAMPUNI AMBAYO AMEFANIKIWA KUYAONDOA MPAKA SASA NI:-
  • PANACOM SOLUTIONS LTD
  • WILD DOGS TOURS & TRAVEL
  • STELLAH TRAVELS
  • SOLOHAGA CO. LTD.
KAMPUNI AMBAYO IMEHAMISHWA
  • ETERNAL INTERNATIONAL
BAADHI YA MAKAMPUNI AMBAYO TAYARI AMEANZA MCHAKATO WA KUYAONDOA NI:-
  • GESTA FINANCE
  • TAN ADVERTS
  • UNIVERSITY ABROAD REPRESENTATIVE (UAR)
  • JUMBO CAMERA HOUSE
  • ORIFLAME
  • NA MENGINE AMBAYO BADO HAJAYATAJA.
Sababu anayotumia ni kuwa anatafuta maeneo kuweka ofisi za wafanyakazi wa NSSF, kwanza unashindwa kuelewa hao wafanyakazi ambao inabidi idadi kubwa ya wapangaji lazima waondolewe ili wakae wako wapi? Kwa mtu ambaye angeangalia ugumu wa kupata wapangaji na jinsi ambavyo sehemu kubwa ya majengo ya NSSF hayana wapangaji, basi kama kweli kuna watu wanahitaji nafasi za kufanyia kazi kuna department angepeleka katika majengo ambayo yako wazi, kwanza unataka uweke ofisi ground floor na mezzanine imekuwa duka la nguo? Anashindwaje kutumia rasilimali alizonazo bila kuathiri mapato ya mfuko, ambayo hayo mapato yanahitajika ili kuendesha mfuko, kuwalipa wastaafu MAFAO, na kuweza kurejesha pesa za uwekezaji?

Huyu ni mfano wa wafanyakazi wa taasisi za umma ambao maamuzi yao yasiyo ya busara yamekuwa yakigharimu hizi taasisi kwa kiwango kikubwa. Mfano hao wapangaji anaowandoa kwa ulazima wana mikataba ya miaka mitatu, na kuendelea, je wakiamua kushitaki si mfuko itabidi ulipe fidia? Mimi nimeandika kama raia mwema, jambo hili liangaliwe na watu walio katika vyombo vya maamuzi ili lipatiwe ufumbuzi, na huyu ni Estate Manager wa nchi nzima, haya yote kayafanya Benjamin Mkapa Towers pekee, hatujui katika majengo mengine na mikoa mingine.

NB: CHA AJABU OFISI AMBAZO AMEWAONDOA WATU ZIKO TUPU, HAKUNA KINACHOENDELEA, ZIKO WAZI, UKITAKA ZIONA FIKA MEZZANINE FLOOR NA UZUNGUKE, KAMA ULISHANGAA YA MUSA SASA UTAONA YA FIRAUNI.
 
Attachments

  • MENEJA MPYA WA MAJENGO NSSF ANAFUKUZA WAPANGAJI AMBAO NI WALIPAJI WAZURI WA KODI.pdf
    110.8 KB · Views: 7
Mbona rahisi mapato yanapanda au yanashuka kutokana na strategy yake?

Kama hujui umehukumu mapema sana, na watu wa pwani watauita huu ni wivu au umbea.
 
Naanza kuamini maofisini wachawi wapo,
Una hoja sawa, lakini jinsi story ulivyoandika yaani umemshambulia jamaa binafsi hasa hiyo nafasi hamna kingine inaonyesha unaitaka/unaona wivu kupata hiyo nafasi.!
Kwa Uchu ulionao wa nafasi hiyo unaweza kufanya lolote endapo utaahidiwa kupewa hiyo nafasi.hata kumdhuru mhusika.
N.B Watanzania tujifunze kukubaliana na Matokeo tusiwe kama Haji Manara Mkuki kwa Nguruwe kwa binadamu mchungu.!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nokwenumuya,
Du hata Jumbo Camera,wapangaji wakubwa na wa miaka mingi, kwanza hilo jengo limekuwa kama mahame ni jengo chafu na bado lina maeneo mengi yaliyo wazi,angekuwa mjanja angelifanya kama China Plaza kwa kuligeuza na kuweka viwamba vingi na kupunguza tozo hapo wangeweza kutengeneza biashara.Inaonekana jamaa ana mipango ya kuweka watu wake.
 
Bila data za mapato kushuka your story can be spinned in any direction hiyo ndio point yangu.
mbona jambo hili linahitaji uelewa mdogo sana, unapoondoa wapangaji waliokuwa wanalipa mamilioni kila mwezi, hapo unakuwa unaongeza kipatp? kama nia ni kuwatafutia wafanyakazi ofisi, je kwanini asitumie zilizopo, au asiwapeleke katika majengo mengine ambayo yako wazi?
 
Nimesoma kwa umakini mkubwa huu uzi ; nilichogundua huyu mwandishi cyo mwananchi wa kawaida ila nimfanyakazi wa nssf

Lakini pia, nimegundua mleta uzi nimuhusika mkubwa wa hii mada , yawezekana kuna masrahi yake kwa wapangaji wanao ondolewa au alitarajia hicho cheo apewe yeye!

Jambo jingine ninacho ona hapo nssf watakuwa wamebanwa sana sasa hivi na urio! Maana ukiona manyoya jua kaliwa! Nssf palioza sana hakuna mtu asiyejua aliye wahi kuwa mwanachama wa mfuko huu.

Hata serikari ilipoyaunganisha mashirika haya wanachama tulifurahi, Nssf walikuwa wezi wote kuanzia mlinzi hata km alitolmka kampuni za ulinzi hadi mkurugenzi Nssf mlikuwa wezi sana! Mimi mmekula tsh. 600000/= mwaka 2011 yaani kwa nguvu kabisa. Nssf mlikuwa wezi acha mbanwe! URIO BANA KABISA HAO WOTE ULIOWAKUTA NSSF MAJIZI MAKUBWA.

Mliiba kuanzia miradi mpaka michango yetu ya wanachama!

URIO WAFUMUE WOTE HAO HUYO ALIELETA HII MADA NDO WALE WAPIGAJI WA Mpangaji analipa shirika laki3 yeye analipwa laki6.

Urio kufa nao hao safisha shirika nenda mwaza, geita , na kwingine.
 
NSSF KWAFUKUTA: MENEJA MPYA WA MAJENGO NSSF ANAFUKUZA WAPANGAJI AMBAO NI WALIPAJI WAZURI WA KODI
  • Alipewa cheo na Mkurugenzi Mkuu bila kufuata taratibu.
  • Aliletwa kama afisa wa kawaida toka PPF, ambako ndipo alipotokea Mkurugenzi wa sasa pia.
  • Anawafukuza wapangaji wanaolipa vizuri kwa kigezo cha kupata nafasi za kuweka ofisi.
  • Ofisi zinapewa maeneo makubwa kuliko mahitaji yanayostahili.
  • Ofisi nyingi alizoondoa watu ziko wazi.
  • Case study hii ni kwa Jengo la Benjamin Mkapa pekee. Mengine nashauri yafuatiliwe.
Hivi karibuni Mkurugenzi Mtendaji wa NSSF alimteua Bwana Augustino K. Paul kuwa meneja wa majengo (Estate Manager). Augustino K. Paul alihamishwa toka PPF baada ya sheria ya kuunganisha mifuko ya hifadhi ya Jamii. Na alikuwa ni afisa mdogo anayehusika na upimaji wa maeneo katika majengo ili kugawa kwa square meters pamoja na kushughulika na mambo ya ufundi na repair, ambako katika ofisi yao kuna watu wengi.

Siku moja Mkurugenzi Mtendaji alishuka na kufika ofisi ya watu wa Ufundi na akamkuta Augustino yuko peke yake, akatumia kigezo hicho kumpandisha cheo, toka afisa wa chini hadi kuwa Estate Manager, bila kuzingatia katika idara hiyo baada ya kuripoti kazini huwa wana kazi nje ya ofisi kushughulika na mambo ya maintenance, au kwenda kushughulikia majengo mengine yaliyo chini ya NSSF. Hivyo inaonekana kuna mpango uliopangwa na Mkurugenzi Mtendaji na yeye, kwa kuwa wote walitoka PPF basi akamtafutia nafasi ambayo ni dhahiri uwezo wake kuitendea haki ni mdogo.

Katika hilo jengo la Benjamin Mkapa hivi sasa amewaondosha wapangaji wa muda mrefu, ambao wamekuwa wakilipa kodi zao kwa wakati na kwa uaminifu, hadi sasa napoongea amewaondoa wapangaji watatu, mmoja kamuhamishia eneo jingine ambalo ni dogo kuliko la awali (ina maana mapato yanapungua), wengine bado wanavutana katika mchakato wa kuwaondoa.

Hivi sasa zaidi nusu ya majengo ya NSSF hayana wapangaji, mtu huyu badala ya kuweka mkakati wa kupata wapangaji wapya kwanza yeye ndio anafukuza wapangaji ambao wanafanya biashara zao na kulipa kodi, ambayo ndio kipato ambacho kinasaidia kuendesha taasisi, mtu huyu asipoangaliwa ataua baishara ya Real Estate iliyo chini ya NSSF, ni Dhahiri uwezo wake ni mdogo, huenda anastahili kubaki kuwa fundi wa upimaji.

MAKAMPUNI AMBAYO AMEFANIKIWA KUYAONDOA MPAKA SASA NI:-
  • PANACOM SOLUTIONS LTD
  • WILD DOGS TOURS & TRAVEL
  • STELLAH TRAVELS
  • SOLOHAGA CO. LTD.
KAMPUNI AMBAYO IMEHAMISHWA
  • ETERNAL INTERNATIONAL
BAADHI YA MAKAMPUNI AMBAYO TAYARI AMEANZA MCHAKATO WA KUYAONDOA NI:-
  • GESTA FINANCE
  • TAN ADVERTS
  • UNIVERSITY ABROAD REPRESENTATIVE (UAR)
  • JUMBO CAMERA HOUSE
  • ORIFLAME
  • NA MENGINE AMBAYO BADO HAJAYATAJA.
Sababu anayotumia ni kuwa anatafuta maeneo kuweka ofisi za wafanyakazi wa NSSF, kwanza unashindwa kuelewa hao wafanyakazi ambao inabidi idadi kubwa ya wapangaji lazima waondolewe ili wakae wako wapi? Kwa mtu ambaye angeangalia ugumu wa kupata wapangaji na jinsi ambavyo sehemu kubwa ya majengo ya NSSF hayana wapangaji, basi kama kweli kuna watu wanahitaji nafasi za kufanyia kazi kuna department angepeleka katika majengo ambayo yako wazi, kwanza unataka uweke ofisi ground floor na mezzanine imekuwa duka la nguo? Anashindwaje kutumia rasilimali alizonazo bila kuathiri mapato ya mfuko, ambayo hayo mapato yanahitajika ili kuendesha mfuko, kuwalipa wastaafu MAFAO, na kuweza kurejesha pesa za uwekezaji?

Huyu ni mfano wa wafanyakazi wa taasisi za umma ambao maamuzi yao yasiyo ya busara yamekuwa yakigharimu hizi taasisi kwa kiwango kikubwa. Mfano hao wapangaji anaowandoa kwa ulazima wana mikataba ya miaka mitatu, na kuendelea, je wakiamua kushitaki si mfuko itabidi ulipe fidia? Mimi nimeandika kama raia mwema, jambo hili liangaliwe na watu walio katika vyombo vya maamuzi ili lipatiwe ufumbuzi, na huyu ni Estate Manager wa nchi nzima, haya yote kayafanya Benjamin Mkapa Towers pekee, hatujui katika majengo mengine na mikoa mingine.

NB: CHA AJABU OFISI AMBAZO AMEWAONDOA WATU ZIKO TUPU, HAKUNA KINACHOENDELEA, ZIKO WAZI, UKITAKA ZIONA FIKA MEZZANINE FLOOR NA UZUNGUKE, KAMA ULISHANGAA YA MUSA SASA UTAONA YA FIRAUNI.
Ukiisoma hii story unaona inatokea sehemu moja.

Kutowafurahia watu waliotoka PPF na kuja NSSF, hii isiwe shida kwako ni kampuni ya umma.

Kuna kachuki dhidi ya mkurugenzi mkuu kutoka kwa huyu memba ambaye ni timu NSSF ya zamani, hajui NSSF mpya ndio mpango mzima.

Na kubwa zaidi, kuna kaupigaji fulani kwenye mikataba ya majengo.... Ambayo imebidi ifanywe upya, kwani wale maafisa wa zamani ni washikaji au walikuwa wanakula pamoja na hao waliobadilishwa.

Kukimbilia kuja kwenye media kama hii kwa mtoa malalamiko ni wazi , kisu kimegusa mfupa.

Ndugu fahamu zama zimebadilika na kila jiwe litapinduliwapinduliwa na kutikiswa ... Kama mapato yatashuka , hilo ni jukumu la mkurugenzi mkuu atawajibika nalo, mbona unaonyesha kama unamtakia mema wakati kwa bandiko lako unamtakia anguko??? Hapo vipi?
 
Naanza kuamini maofisini wachawi wapo,
Una hoja sawa, lakini jinsi story ulivyoandika yaani umemshambulia jamaa binafsi hasa hiyo nafasi hamna kingine inaonyesha unaitaka/unaona wivu kupata hiyo nafasi.!
Kwa Uchu ulionao wa nafasi hiyo unaweza kufanya lolote endapo utaahidiwa kupewa hiyo nafasi.hata kumdhuru mhusika.
N.B Watanzania tujifunze kukubaliana na Matokeo tusiwe kama Haji Manara Mkuki kwa Nguruwe kwa binadamu mchungu.!

Sent using Jamii Forums mobile app
uko sahihi kabisa, ila ukweli ni kwamba mimi sio mfanyakazi wa NSSF. ila unaweza take trouble kama uko Dar es Salaam, fika jengo la Benjamin Mkapa, mezzanine floor, zunguka uone ofisi ambazo watu wameondolewa, pia fika ofisi nilizotaja wameambiwa waondolewe au wahamishiwe majengo mengine ya NSSF utajua nisemacho. una haki kutoamini taarifa yangu moja kwa moja ili kumtendea haki mlalamikiwa, ila ni vyema kufuatilia ili kujiridhisha, na jambo hili lipo kwa maslahi mapana ya huu mfuko, na pia kwa maslahi ya wapangaji ambao kwanza wana mikataba na pili hawashindwi kulipa kodi.
 
Juzi nimeona afisa wao mwingine anasema watatoa 5 billion/sh kusaidia ukuaji wa viwanda na hizo hela zitapitia AZANIA bank ambako wanamiliki hisa.

Watu wenyewe wanaokopeshwa ni wajasiriami wadogo kutoka SIDO na VETA; etc with nonsense.

Chakushangaza kuna international frameworks baada ya financial crisis za 2008 pamoja na BoT regulations zinazozuia ‘pension funds’ kuwekeza kwenye high risk areas; hizo hela zikipotea ni mzigo wa serikari.

Sasa kitakwimu duniani on average 70% ya biashara mpya ufa ndani ya mwaka, 20% ndani ya miaka 5 na hizo zinazobaki only 5% ndio ukuwa zaidi ndani ya miaka 10 toka kuanzishwa.

Wao high risk area ndio wameona sehemu ya kwenda kuwekeza huko au tuseme kuchezea kamali hela za wachanhiaji.

Kuna mawili either AZANIA bank in cashflow problems NSSF inatumia njia ya kuwaongezea hela kijanja au mkurugenzi wa sasa ndio walewale hasara ikija wakishindwa kulipa pension za watu on time serikari ipo ya kuwalipia madeni besides what’s 5 billion kwa taasisi yenye asset zenye value of trillion.

Na BoT sijui SSRA wapo wanaangalia huu upuuzi wakati unaanza kutokea.
 
Nimesoma kwa umakini mkubwa huu uzi ; nilichogundua huyu mwandishi cyo mwananchi wa kawaida ila nimfanyakazi wa nssf

Lakini pia, nimegundua mleta uzi nimuhusika mkubwa wa hii mada , yawezekana kuna masrahi yake kwa wapangaji wanao ondolewa au alitarajia hicho cheo apewe yeye!

Jambo jingine ninacho ona hapo nssf watakuwa wamebanwa sana sasa hivi na urio! Maana ukiona manyoya jua kaliwa! Nssf palioza sana hakuna mtu asiyejua aliye wahi kuwa mwanachama wa mfuko huu.

Hata serikari ilipoyaunganisha mashirika haya wanachama tulifurahi, Nssf walikuwa wezi wote kuanzia mlinzi hata km alitolmka kampuni za ulinzi hadi mkurugenzi Nssf mlikuwa wezi sana! Mimi mmekula tsh. 600000/= mwaka 2011 yaani kwa nguvu kabisa. Nssf mlikuwa wezi acha mbanwe! URIO BANA KABISA HAO WOTE ULIOWAKUTA NSSF MAJIZI MAKUBWA.

Mliiba kuanzia miradi mpaka michango yetu ya wanachama!

URIO WAFUMUE WOTE HAO HUYO ALIELETA HII MADA NDO WALE WAPIGAJI WA Mpangaji analipa shirika laki3 yeye analipwa laki6.

Urio kufa nao hao safisha shirika nenda mwaza, geita , na kwingine.
hehehehe, hii atitude yako nayo kama saa mbovu, kwa hiyo unaamini wote walio NSSF wabovu? hakuna mpangaji NSSF mwenye mikataba kama usemavyo. ila nachosema jaribu kukifuatilia. hata ukifika sehemu ukaambiwa watu wale wabaya fuatilia utajua uhalisia, usikurupuke kuhukumu mkuu.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom