Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,999
[h=3]NSSF kujenga Kiwanda cha Korosho[/h]
Na Queen Lema, Arusha
MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), unatarajia kujenga kiwanda cha kubangua zao la korosho mkoani Mtwara ambacho ujenzi wake utagharimu dola za Marekani milioni 35 hadi 40.
Ujenzi huo utaanza mara moja baada ya mazungumzo ya uwekezaji huo kukamilika kwani zao hilo lina soko kubwa ndani na nje ya Tanzania ili kukuza uchumi wa mikoa ya Lindi na Mtwara.
Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo, Dkt. Ramadhan Dau, aliyasema hayo jana wakati akizungumza na wadau wa NSSF katika mkutano wa tatu unaoendelea jijini Arusha.
Alisema hivi sasa mfuko huo unaangalia jinsi ya kuwasaidia wananchi wa mikoa hiyo ambao wanajihusisha zaidi na zao
hilo lakini bado wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu
wa kiwanda cha kubangua korosho ili kukuza kipato chao.
Wakulima wa zao la korosho mkoani Mtwara wanapata shida
kwa sababu ya ukosefu wa kiwanda cha kubangua zao hili hivyo
kama tutawekeza kwa kujenga kiwanda ni wazi kuwa thamani ya
zao hili itaongezeka.
Tunahitaji ushirikiano wa wadau ili tuweze kufanikisha ujenzi
huu pamoja na uongozi wa Wilaya ya Tandahimba ili lengo letu liweze kufanikiwa kwa wakati, alisema Dkt. Dau.
Katika hatua nyingine, Dkt. Dau alisema uwekezaji huo utakuwa na faida kwa sababu wakulima wa zao hilo waliopo mikoa ya Lindi na Mtwara, watauza korosho zao kwa bei kubwa kuliko ilivyo sasa.
Hivi sasa wanauza korosho zao kwa dola moja ya Marekani hivyo kusababisha wapate hasara...uwekezaji huu ukikamilika watauza dola saba baada ya kubanguliwa hivyo kunufaika zaidi, alisema.
Kwa upande wao, wadau wa mfuko huo walisema umefika wakati wa NSSF kuona umuhimu wa kuwekeza katika viwanda hususani vilivyokufa kwa kuvifufua ili kutoa ajira kwa vijana, kukuza
uchumi wa Taifa na kupunguza umaskini nchini.
Walisema hivi sasa, Tanzania kuna viwanda vingi ambavyo vimekufa na vinatumika kama maghara ya kuhifadhia mizingo
na vyakula vya watu binafsi hivyo mfuko huo unaopaswa kubuni
mbinu mpya ya uwekezaji katika viwanda.
Mifuko ya kijamii ina nafasi kubwa sana ya kufufua viwanda vyetu vilivyokufa kwa mfano...kiwanda cha kubangua korosho kilikuwepo Pwani lakini kilikufa na wakulima kupata shida hivyo zao hilo kukosa ubora unaotakiwa, alisema.
MAJIRA