NSSF Arusha wanataka rushwa kwangu!

Mwana Kwetu

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2011
Posts
652
Reaction score
607
NSSF Arusha kuna tabia ya usumbufu inaashiria rushwa.

Baada ya kupokea awamu ya kwanza ya fao la uzazi kabla ya kujifungua nimekuwa nikiambiwa nenda rudi ili kupewa awamu ya pili licha ya ku submit document zoote.

Sababu wanazotoa hazina maana kwani Mara wasingizie mhasibu kasafiri nk. Nipeni ushauri hatua ya kuchukua kwani napoteza muda mwingi sana bila mafanikio
 
Pole sasa, muone Manager wao atakusaidia.
 
Hawa jamaa huwa corrupt sana na hawana huruma hata Mzazi wanamtaka rushwa.
 
Kama ulilipwa ukiwa mjamzito ukakamilisha process zote ilitakiwa baada ya kujifungua process iwe very short yaani ku submit document za hospital na kupewa cheque ili kumalizia mafao yako. Wanachokifanya ni dhambi wanamtaka kuchuma. Wakamatishe za Moto waingie 2013 wakilia
 
Hawa watu wanatabia ya kujifanya Miungu watu, ni wasumbufu kuliko maelezo, wanashindwa kutambua kuwa hiyo pesa ni halali yako na ni kutokana na jasho lako!!, Nilipata shida sana kupata fao langu la kujitoa nilipoacha kazi mahalafulani miaka kadhaa iliyopita, mpaka kuna jama nilimkunja shati pale NSSF Ubungo.

Nenda kwa meneja kamuone, ikishindikana onana na meneja wa mkoa. Sababu ya muhasibu kusafiri haina mashiko, kwa kuwa muhasibu kusafiri haimaanishi ofisi ya muhasibu imesafiri. Pole sana, hii ndo Tanzania yetu, lakini na wewe huko unakofanya kazi hakikisha unafanya kazi kwa moyo wote na kwa nguvu zako zote. Mabadiliko yanaanza na wewe, It begins with you!!. Tukishabadilika watanzania, kila mmoja kwa nafasi yake, ndipo tutakapoendelea.
 
Inasikitisha sana mijitu na akili zao kumpa wakati mgumu Mzazi ambaye Ana recover kutokana na kujifungua. Hizo hela zitamsaidia nini Kama hatazipata kipindi cha maternity leave. Najiuliza kwa nini reasoning Yao ni ndogo kiasi hicho kana kwamba hawajakwenda darasa
 
Lazima wajue hizo hela tunazoweka ndo zinawafanya waishi na familia zao. Hii kufanya kazi kwa macho ya rushwa kunawaumiza wa Tz sana
 
Mwana Kwetu

Ina maana unakuwaga hapa A town halafu hatujuliani afya hata kidogo,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,bila shaka hilo lako ni jambo ambalo limekuwa sugu katika sekta hiyo na imekuwa tabia naujue siku zote tabia haina dawa!!!!
Wee washikishe kitu kidogo maana ni ugonjwa wao huo!

Pole sana Mwana Kwetu; Ila ningependa nikikuona katika umoja wa wanaJF wa hapa jijini,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,Karibu sana!
 
Last edited by a moderator:
Unakuja asubuhi unaonyesha appointment unaambiwa subiri kwenye conference Fulani then wanakuwashieni Tv na unasubiri kwa masaa. Then unaitwa jina unapewa tarehe nyingine Wiki 3 mbele then appointment zinaendelea bila kujua unapoteza muda wako.
 
Pole mdau. Hawa jamaa wanakera sana, ndio maana wafanyakazi wa sekta ya migodi tunawakimbia.
 
Nitawatafuta mnipe details
 
Last edited by a moderator:
Siyo Arusha Pekeyake nadhani ni Tanzania nzima. Ukiangalia hata michango huwa haiingizwi miezi yote
 
Kusubiria cheque masaa 6 na kisha kumbiwa mhasibu hayupo njoo siku nyingine ni utendaji wa kawaida Ktk hii ofisi. Wanawaweka watu muda mrefu kwa kitu ambacho hakihitaji hata dk 10. Uongozi wa Nssf Arusha pia unachangia kwani manager alipaswa kufanya assessment kwani malalamiko ni mengi kwa watu wanaosubiri
 

Ndio maana wadau wamesema peleka malalamiko yako kwa manager..inawezekana huu uhuni manager hana taarifa nao...anyway pole sana....nauelewa upuuzi unaoendelea hapo..niligombana nao kwa jambo fulan mpaka sasa mhasibu na staff wengine ni marafiki zangu.
 
niashukuru kwa hii post.... binafsi nilikamilisha kila kitu ktk fao la kujitoa lakini dk za mwisho kila cku ikaanza njoo kesho njoo kext week ilifika hatua hadi wananionyesha cheki ila wanatafuta means ya kwenda kudeposit maana ilikua ni zaidi ya 10m huwez weka cheki mwenyewe kutokana na sheria mpya za mabenki... ikafika hatua unaenda wanakwambia hawakwenda eti walikua na wageni ofcn.... mara walikosa usafiri nikakomaa nao ila baada ya kama 4 months ivi wakanipa!!!! ni wanadai rushwa kwa nguvu sana haki ya mtu haipotei ila shida ni kuchelewa!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…