NSSF: 33.3% ya mshahara kwa miezi 6

NSSF: 33.3% ya mshahara kwa miezi 6

Mwenye habari ya kanuni mpya ya NSSF tusaidieni kuweka hapa. Binafsi nimesoma Daily News lakini maelezo ya waziri na gazeti hayaeleweki, 'vague', mara 33.3% ya mshahara italipwa kila mwezi kwa miezi 6, mara ni kuanzia August 1, 2018. Yaani baada ya miezi 6 what next? Kuweza kupokea pension uwe umechangia angalau miaka 15. What happens kwa sisi tuliochangia 6 years and are not planning to be employed again? Iko siku nitawaza kwenda msituni.
Utaishia kuliwa na simba tu
 
Kwanini hakuna maelezo ya waziri kivuli wa sector hii? Zitto pamoja na kuwa ni pretender mzuri angalau anaamsha debate ya masuala muhimu, what is chadema leadership doing so far?
Bro kula ulimpa nani?tuanzie hapo.
Huyo ndo wa kumuomba akusaidie.chadema wala mamlaka gani katika nchi hii?tulitetea makanikia watu wakaanza kumsema lisu anakwamisha maendeleo.na risasi akapigwa.
pambaneni tu na hali yenu.
Mwenyekiti wa wanyonge ATAWATETEA.[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Nenda kwenye Duka la serikali mtaa wa Jamhuri baada ya njia ya kuingilia break point mlango kama watatu hivi utajua kama kategeneza au la. Zaidi ya hapo unategemea hear say kufanya maamuzi.
Tabu yoote hiyo ya nini? Soma hapo chini sheria mpya kinachosubiriwa ni regulations tuu jombaaa...
IMG_20180820_183428.jpeg
 
Kodi INKIND kwenye Pension ya mtumishi,poor formulas..wizi mtupu
 
du ila usiombe likukute..... utalia. tulizoea unapiga kazi mkataba wa miaka mitano unachukua mzigo unajipanga upya.
 
Sijui kwanini mungu haleti Yale madhoruba ya vimbunga apitie wanasiasa wote waliounga na kupendekeza hii sheria nyonyaji.


Binafsi Nina Pesa zangu Nssf na lapf mpaka Leo sijapewa hata mia. Wakati wabunge wakimaliza vipindi vyao wanavuta pensheni zao kama kawaida. Sisi mafukara wanasubiri tujifie waanze kuwazungusha warithi na hela wazipige.


Halafu wanategeme niwe mwananchi Wa kuiombea Neema nchi hii. Tangu ninyimwe hela zangu za nssf na lapf hakuna siku imepita sijaiombea laana hii nchi na viongozi wake.
 
Hivi pension sasa ndio basi maana hakuna mstaafu aliyelipwa mwezi huu huko PPF. Ina maana mambo hayako vizuri huko kwenye mfuko mkuu kupelekea pension za wastaafu kupelekwa huko. Mbona hali hii itaathiri mamilioni. Irine wa SSRA alisema wastaafu 9500 watalipwa January, 2019 ina maana kwa sasa hakuna malipo hadi wakati huo. Hebu tutafakari maelezo ya yule mama na hali inavyo kuwa.
 
Hivi pension sasa ndio basi maana hakuna mstaafu aliyelipwa mwezi huu huko PPF. Ina maana mambo hayako vizuri huko kwenye mfuko mkuu kupelekea pension za wastaafu kupelekwa huko. Mbona hali hii itaathiri mamilioni. Irine wa SSRA alisema wastaafu 9500 watalipwa January, 2019 ina maana kwa sasa hakuna malipo hadi wakati huo. Hebu tutafakari maelezo ya yule mama na hali inavyo kuwa.
Hatwari
 
Ndio faida ya kuua vyama vya upinzani na vyama vya wafanyakazi, wastaafu wanadhurumiwa jasho lao hakuna wa kuwatetea. Ndio sifa ya udikteta taasisi zote zinauawa anabaki dikteta tu.
 
Bro kula ulimpa nani?tuanzie hapo.
Huyo ndo wa kumuomba akusaidie.chadema wala mamlaka gani katika nchi hii?tulitetea makanikia watu wakaanza kumsema lisu anakwamisha maendeleo.na risasi akapigwa.
pambaneni tu na hali yenu.
Mwenyekiti wa wanyonge ATAWATETEA.[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Sawa nimekuelewa, kila mtu apambane na hali yake
 
Kuna mengi mazuri yamefanywa awamu hii, ila wasijione malaika kwenye hili, hapa wamekosea sana. Kwa lugha isiyo ya kupepesa ni wizi wa dhahiri. Mtu ana miaka 30 now, anadai mil 15 unampa mil 2 tena kwa awamu then hio nyingine isubirie miaka 15 ijayo? Je italipwa na riba? Kama mtu hajapata bahati au hataki kuajiriwa tena hio hela itamsaidiaje akishazeeka? Kwani hajakidhi vigezo vya kulipwa pension. Umri wa kujipanga kimaisha ni mid30. Kijana hakopesheki, nssf yake humpi wategemea awe mzalendo kwa lipi?
Kumsomesha mwanae bure sio suluhisho kwani mtoto halali na uniform shule, madawa bure hatuumwi kila siku, barabara nzuri tutatoka nyumbani kwenda wap? Ila tuna mahitaji muhimu zaidi ya madawa na barabara nzuri. Ukimcheki Bashe ameitetea hii as if alishawahi kuburuzwa kwa wadosi na ana hela huko nssf. Ukiacha ile sheria ya ndoa ya miaka ya 70 sheria mbov ifuatayo ni hii ya fao la kujitoa.
#NSSFbadilisheria
 
Back
Top Bottom