taffu69
JF-Expert Member
- Feb 26, 2007
- 2,094
- 538
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
TAARIFA KWA UMMA
NOTISI YA KUANZISHA MIKOA NA WILAYA
OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
TAARIFA KWA UMMA
NOTISI YA KUANZISHA MIKOA NA WILAYA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mamlaka aliyopewa chini ya Ibara ya 2(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaweza kuigawa Jamhuri ya Muungano katika Mikoa, Wilaya na maeneo mengineyo kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Sheria au kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.
Katika kutekeleza Mamlaka hayo, Rais ametoa notisi ya kusudio la kuanzisha Mikoa minne (4) na Wilaya kumi na tisa (19). Notisi hizo ambazo zimetolewa chini ya kifungu cha 4 cha Sheria ya Uanzishaji wa Mikoa na Wilaya Sura 397 ya Toleo la 2002 ni Tangazo la Serikali Na. 285 la tarehe 9 Septemba, 2011 kwa ajili ya uanzishaji wa Mikoa na Tangazo la Serikali Na. 287 la tarehe 9 Septemba, 2011 kwa ajili ya uanzishaji wa Wilaya.Madhumuni ya Notisi hizi ni kuzialika Taasisi na mtu mwingine yeyote ambaye ataathirika na uanzishaji huo kutoa maoni, mapendekezo au pingamizi iwapo yatakuwepo katika kipindi cha siku 21 kwa Mikoa mipya na siku 30 kwa Wilaya mpya kuanzia tarehe ya Notisi hizi.
Baada ya muda uliowekwa kupita, Rais atachambua maoni, mapendekezo na pingamizi zilizotolewa na kuzitolea uamuzi kabla ya kuanzisha rasmi Mikoa na Wilaya hizo kwa kadri atakavyoona inafaa.
Mikoa mipya inayoanzishwa na Makao Makuu yake ni kama ifuatavyo: -
MKOA | WILAYA ZAKE | MKOA ZINAKOTOKA | MAKAO MAKUU | |
1. | Geita | Geita | Mwanza | Geita |
Nyang'hwale(Mpya) | Mwanza | |||
Chato | Kagera | |||
Bukombe | Shinyanga | |||
Mpya/Mbogwe | Shinyanga | |||
2. | Simiyu | Bariadi | Shinyanga | Bariadi |
Itilima (Mpya) | Shinyanga | |||
Maswa | Shinyanga | |||
Meatu | Shinyanga | |||
Busega (Mpya) | Mwanza | |||
3. | Njombe | Njombe | Iringa | Njombe |
Wanging'ombe(Mpya) | Iringa | |||
Ludewa | Iringa | |||
Makete | Iringa | |||
4. | Katavi | Mpanda | Rukwa | Mpanda |
Mlele(Mpya) | Rukwa |
Wilaya mpya zinazoanzishwa na Makao Makuu yake ni kama ifuatavyo: -
WILAYA MPYA | WILAYA MAMA | MKOA | MAKAO MAKUU | |
1. | Buhigwe | Kasulu | Kigoma | Buhigwe |
2. | Busega | Magu | Mwanza | Igalukilo |
3. | Butiama | Musoma | Mara | Nyamisisi |
4. | Chemba | Kondoa | Dodoma | Chemba |
5. | Gairo | Kilosa | Morogoro | Gairo |
6. | Ikungi | Singida | Singida | Ikungi |
7. | Itilima | Bariadi | Shinyanga | Itilima |
8. | Kakonko | Kibondo | Kigoma | Kakonko |
9. | Kalambo | Sumbwanga | Rukwa | Kalambo |
10. | Kaliua | Urambo | Tabora | Kalua |
11. | Kyerwa | Karagwe | Kagera | Rubwera |
12. | Mbogwe | Bukombe | Shinyanga | Mbogwe |
13. | Mkalama | Iramba | Singida | Nduguti |
14. | Mlele | Mpanda | Rukwa | Inyonga |
15. | Momba | Mbozi | Mbeya | Ndalambo |
16 | Nyang'hwale | Geita | Mwanza | Nyang'hwale |
17. | Nyasa | Mbinga | Ruvuma | Mbamba Bay |
18. | Uvinza | Kigoma | Kigoma | Lugufu |
19. | Wanging'ombe | Njombe | Iringa | Waging'ombe |
Kwa taarifa hii, Wananchi wote wanaalikwa kutumia haki yao ya kisheria kutoa kwa maandishi maoni, mapendekezo na pingamizi kama zipo kwa kuzingatia utaratibu uliwekwa kwa ajili ya maendeleo ya Wananchi wa maeneo husika na maslahi ya Taifa kwa ujumla.
Maoni, pingamizi au mapendekezo hayo yatumwe kwa kutumia anuani ifuatayo: -
Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,
S. L. P 1923,
DODOMA.
E-mail hakattanga@yahoo.com
Fax- 026-2322116
Imetolewa na: -
Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.
Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.
*************************************************
Wakuu kwa kuangalia hali halisi ya uchumi wa Tanzania kwa sasa na jinsi Taifa letu linavyokabiliwa na matatizo mengi ya kiuchumi pamoja na kijamii; ni sahihi kwa wakati huu kuanzisha mikoa mipya na wilaya mpya tena kwa idadi kubwa kama hiyo (Mikoa MINNE na Wilaya KUMI NA TISA).
Lipi jambo la muhimu kwa sasa, kuanzisha wilaya na mikoa mipya ama kuangalia namna ya kutatua matatizo yanayolikabili Taifa kwa sasa?
Swali la kujiuliza, Mbona wakati wa utawala wa awamu ya kwanza hadi ya tatu Marais wa vipindi hivyo hawakuongeza mikoa na wilaya kwa idadi kubwa kama hiyo? Iweje wakati wa awamu ya JK ndiyo tunashuhudia kila kitu kikiongezwa kama Baraza la Mawaziri, Uteuzi wa majaji, na hata Mikoa pamoja na Wilaya Mpya.
Kwa wale wenye kuliona jambo hili na madhara yake naomba tupaze sauti kukemea na kulikataa mapema.
Source: Pmoralg - Prime Minister's Office Regional Administration and Local Government | Tanzania